- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
BAMAKO, MALI
MHAMIAJI raia wa Mali, Mamoudou Gassama, ambaye alipata
umaarufu kote duniani mwezi uliopita wakati alikwea jengo mjini Paris, Ufaransa
kumukoa mtoto, amesema amefurahishwa sana kurudi kwao Mali kutembea.
"Nina furaha sana. Nina furaha sana sana kwa sababu
kila mtu alikuja uwanja wa ndege na kisha nikamuona baba yangu na watu wote wa
familia yangu. Sikuwa nimemuona baba yangu kwa miaka tisa," aliiambia BBC.
Video ya Mamoudou Gassama akimuokoa mtoto ilisambaa sana
kwenye mitandao ya kijamii.
Alivuka kutoka kwenye ubaraza mmoja hadi mwingine kwa muda
wa chini ya dakika moja akamvuta mtoto huyo aliyekuwa amekwama na kumsalimisha.
Gassama, 22, alivuka bahari ya Mediterranean kwa mashua ya
wahamiaji mwezi Septemba 2014.
Alijiunga na ndugu yake nchini Ufaransa na kufanya kazi
sehemu ya ujenzi kama kibarua.
Tarehe 26 mwezi Mei, alimuona mtoto mdogo akining'inia
kutoka ghorofa ya nne kwenye jengo moja mjini Paris.
Alichukua hatua na kukwea jengo hilo na kumuokoa mtoto huyo
kwa miaka mine. Alinaswa kwenye video na watu waliokuwa chini na kupewa jina
"Spiderman".
"Sikuogopa. mimi ni kama mtu yeyote yule. Nililipata
ujasiri. Ulitoka kwa Mungu. Mungu aliniokoa," alisema.
Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, binafsi alimshukuru Gassama
na kumuahidi kuwa atapa uraia wa Ufaransa.
Wiki ijayo anatarajiwa kuanza mafunzo kwenye idara ya zima
moto mjini Paris.
"Nimefanya uchunguzi wa kiafya. Nitasaini mkataba wangu
tarehe 28. Kisha nitaanza mafunzo ya miezi 10," Gassama aliiambia BBC.
Gassama anayetoka kijiji karibu na Kayes magharibi mwa Mali,
atakaa nchini Mali kwa muda wa siku tatu na atakutana na Rais Ibrahim Boubakar
Keita.
Meya wa Paris, Anne Hidalgo, pia alisifu sana ushujaa wa
mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 22, na akasema alimpigia simu kumshukuru.
Alimuelezea kama "Spiderman wa 18", akimaanisha
wilaya nambari 18 ambako uokoaji huo ulifanyika mjini Paris.
"Hongera kwa Mamoudou Gassama kwa tendo lake la ujasiri
la kumuokoa mtoto," ulisema ujumbe wa Twitter wa Hidalgo.
"Alinielezea kwamba alikuwa amewasili kutoka nchini
Mali miezi michache iliyopita akiwa na ndoto ya kujenga maisha yake hapa.
"Nilimjibu kwamba ishara yake hii ya ushujaa ni mfano
kwa raia wote na kwamba Jiji la Paris bila shaka litakuwa tayari kumuunga mkono
katika juhudi zake za kuishi Ufaransa.
Comments
Post a Comment