Featured Post

NAIBU WAZIRI WA MADINI MHE BITEKO KUUNDA TUME MAALUM KUCHUNGUZA MIGODI YOTE ILIYOPO WILAYA YA ULANGA


Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko akiongea na wananchi wa kijiji cha Ipanko juu ya changamoto ambazo wanakabiliwa nazo na kuunda tume maalum kwa ajili ya kuchunguza migodi yote na aina ya madini yanayopatika katika migodi iliyopo halmashauri ya wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro kwa lengo la kuhakikisha kuwa Tanzania haiendelei kuibiwa na wawekezaji katika seckta ya madini. 
 baadhi ya wananchi wakimsikiliza kwa umakini Naibu waziri wa madini mheshimiwa Doto Bitoke alifanya ziara ya kutatua mgogoro baina ya wawekezaji na wananchi kwenye sekta ya madini


NA FREDY MGUNDA, MOROGORO
Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko kuunda tume maalum kwa ajili ya kuchunguza migodi yote na aina ya madini yanayopatika katika migodi iliyopo halmashauri ya wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro kwa lengo la kuhakikisha kuwa Tanzania haiendelei kuibiwa na wawekezaji katika seckta ya madini.

Akizungumza wakati wa ziara mkoani Morogoro mh Biteko alisema kuwa amdini yote yaliyopo katika ardhi ya Tanzania ni mali ya watanzania hivyo inapaswa kuwanufaisha watanzania kwanza ndipo watu wengine wafuate.

“Naombeni watanzania wote mjue kuwa madini haya ni mali ya watanzania wote hiyo tunapaswa kuyalinda na kutoa taarifa sahihi kwa serikali kama kuna mtu anaiibia serikali kwa namna moja au nyingine hivyo watanzania tuache uoga tuseme ukweli kama Rais wetu anataka kuwa na serikali ya uwazi na uwajibikaji” alisema Bitoke

Bitoke alisema kuwa ni marufuku wawekezaji kutumia pesa zao kuwanyanyasa wananchi waliopo kwenye maeneo ambayo kuna migodi kwa ajili ya kuwaibia watanzania ambao bado wanakipato cha chini katika maeneo yanakopatikana madini.

“Najua hawa wawekezaji wanapesa nyingi sana hivyo isiwe sababu ya kuwarubuni baadhi nya wananchi na kuwatesa wananchi wengi haswa waliopo kwenye maeneo ya madini na niwaambie ukweli wawekezaji wote nchini najua ambavyo mnatumia pesa zenu kuwanyanyasa wananchi,sasa ndio mwisho wenu maana serikali ya awamu ya tano inataka haki kwa kila mwananchi” alisema Bitoke

Bitoke alifanya ziara katika kijiji cha Ipanko kilichopo katika wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro na kugundua kuwa kuna wawekezaji wanaidanganya serikali na wananchi kwa kutoweka wazi kiasi gani ambacho wanakipata kwenye migodi iliyopo katika kijiji hicho.

“Jamani wana Ipanko nchi hii tumeibiwa sana sasa ifike mwisho tusema hapana haiwezekani tena kwenye serikali ya awamu ya tano chini ya Rais wetu Dr John Pombe Magufuli tuendelee kuibiwa madini yetu na kuwanufaisha watanzania ambao wapo nje ya nchi yetu,Rais kasema tayari sasa mwisho kuchezewa kwa mali asili zetu nami nasema pia ni marufuku kuibiwa madini yetu” alisema Bitoke

Akiwa bado anaongea na wananchi wengi waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara kwa ajili ya kumsikiliza naibu waziri wa Madini Mh Bitokealisema kuwa viongozi dhaifu, wanafiki na wasaliti ndio wanaosababisha wawekezaji kuendelea kuiba madini ya watanzania.

“Chonde chonde nyie viongozi wetu wa ngazi za vijiji,kata,tarafa, wialaya na mkoa tunaomba msituangushe kwa kupokea rushwa kutoka kwa wawekezaji na kuisaliti nchi yako kuendelea kuibia kirahisi namna hii” alisema Bitoke

Bitoke alieleza kuwa kuwa serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dr John Pombe Magufuli inawapenda sana kuwa na wawekezaji wengi wenye tija ambao sio wababaisha na ambao wamekuja nchi kuiba rasilimali za watanzania.

“Serikali hii haita mvumia muwekezaji yoyote kwenye sekta ya madini ambaye amekuja kwa ajili ya kuiba madini ya watanzania ambao uchumi wetu ndio unakuwa na mimi nasema kama naibu waziri wa madini hapa nchi sitakubali watanzania tuchezewe kwenye sekta hii ya madini” alisema Bitoke

Aidha Bitoke alisema kuwa haiwekani muwekezaji akawekeza billioni 42 halafu akachangia madawati na sumenti katika jamii kama ndio mchango wake ,haiwezekani wanapaswa kuchangia kulingana na kiasi ambacho wamewekaza kwa faida ya wananchi.

“Mimi binafsi hainiingi akili kuonga muwekezaji amewekeza pesa nyingi kama hizo halafu kwenye shughuli za kiamendeleo amechangia kiasi kidogo namna hivyo kwangu nasema haiwezekani na nchi hii kwa sasa sio yakuchezewa tena” alisema Bitoke

Lakini pia mheshiwa naibu waziri Bitoke alimpongeza mbunge wa jimbo la Ulanga Goodluck Mlinga kwa kuwapigania wananchi wake kwa kuzifikisha kero mahali husika na kutafutiwa ufumbuzi kama ambavyo amefanikisha kumpeka naibu waziri kusikiliza kero za wananchi wa kijiji cha Ipanko.

Nao baadhi ya wananchi Pangarasi Kanyali,Cyprian Kanyali,micky Sengo Doedatus Moholeli,Hilda Linoma na Fredrick Kazimoto  waliohudhuria mkutano huo wa hadhara walimpongeza naibu waziri wa madini mh Bitoke kwa kufika kijiji hapo na kusiliza kero zao wanaamini zitatafutiwa ufumbuzi kwa kufuata sheria na katiba ya nchi hii

“Toka sisi tuzaliwe hatujawahi kutembelewa na waziri na kusikiliza kero zetu kama ambavyo wewe umefika kijijini kwetu leo hii tunajisikia wenye amani na furaha kwa kuwa tunajua kero zetu tunazifikisha moja kwa moja kwa kwa Rais wetu kupitia wewe waziri” walisema wananchi

Awali ya Mbunge wa jimbo Ulanga Goodluck Mlinga alisema kuwa lengo la waziri kufika katika kijiji hicho ni kutazama na kuangalia jinsi gani nchi inavyopoteza mapato kwenye sekta ya madini hapa nchini na jinsi gani wawekezaji wanavyowanyanyasa wananchi.

“Huku ni mbali sana mheshimiwa naibu waziri lakini kuna madini mengi ambayo ndio utajili wa nchi hii hivyo tunapaswa kuwa makini na hawa wawekezaji maana wamekuwa wakiibia sana serikali yetu” alisema Mlinga

Comments