Featured Post

MWANAMUME ALIYETOWEKA ARUDI NA KUKUTA FAMILIA IKIOMBOLEZA MWILI IKIDHANI NI WAKE



ASUNCIÓN, PARAGUAY
MWANAMUME kutoka kijiji kidogo cha Santa Teresa nchini Paraguy alirudi nyumbani baada ya siku tatu na kukuta familia yake ikiomboleza mwili ambao ilidhani ni wake.
Juan Ramón Alfonso Penayo, 20, alikuwa ameonekana mara ya mwisho siku ya Alhamisi akiondoka nyumbani kwao karibu na mpaka wa Brazil.

Eneo hilo linakumbwa na mzozo mkali kati ya magenge ya madawa ya kulevya, na Penayo aliposhindwa kurudi nyumbani, familia ilidhani alikuwa ameuawa.
Polisi walipookota mwili uliokuwa na majeraha makubwa siku ya Jumapili, familia iliamua kuuchukua ikidhani ni wa ndugu yao.
Familia iliandaa mazishi kijijini lakini Penayo alitokea ghafla na kuwakuta wakiomboleza mwili uliokuwa kwenye jeneza wakidhani ni wake.
Baada ya Penayo kurudi mwili huo ambao bado haukuwa umetambuliwa ulirudishwa chumba cha kuhifadhi maiti.
Haijulikani Penayo alikuwa wapi au alikuwa anafanya nini kwa siku hizo tatu ambazo hakujulikana aliko.


Comments