Featured Post

MWANAMKE ANAYENYONYESHA WATOTO WA WANAWAKE WENGINE



DOULA, SOUTH WALES
MWANAMKE yeyote ambaye amewahi kuhukumiwa kwa kutonyonyesha mtoto wake angeweza kuunga mkono kauli ya chuo cha wakunga juma hili.
Siku ya Jumanne, shirika hilo lilisema kama mwanamke akiamua kumpa mtoto wake maziwa mbadala, ni maamuzi yake na lazima yaheshimiwe.

Lakini kabla ya kuanzishwa kwa chupa za kunyonyeshea katika karne ya 19, wanawake ambao hawako tayari au hawawezi kunyonyesha maziwa yao walitumia njia mbadala nayo ni wanawake wengine kuwanyonyeshea watoto.
Hapa, mwanamke mmoja mama wa watoto watatu anatoa ushuhuda wa kunyonyesha watoto wa wanawake wengine.
Samantha Gadsden, mkazi wa mjini Doula, South Wales, anajua kunyonyesha ni suala linalokanganya-hasa wakati watoto unaowanyonyesha ni wa wanawake wengine.
Amekuwa akijitolea muda wake na matiti yake kwa ajili ya watoto wa wanawake wengine tangu alipokuwa mama miaka kumi iliyopita.
''Siwezi hata kukumbuka tena idadi ya watoto wa kike na wa kiume walioshirikiana na wanangu kunyonya, alisema mama huyu mwenye miaka 47.
Kwanza alijifanya kama mama anayemsaidia rafiki ambaye mtoto wake alikuwa hospital.Mama huyo hakuruhusiwa kukaa wodini na hakuwahi kutumia chupa ya maziwa
"Alinipigia simu kwa sababu alitaka nimchukue mtoto, nikasema sawa lakini nitampaje chakula?"
''Akasema nina matumaini kuwa utamlisha.'' hivyo ndivyo nilivyofanya''.
Pia alimnyonyesha mtoto wa rafiki yake wakati analea. "Aliniuliza kwa kuwa alijua ningemnyonyesha mtoto wake. Ni rahisi kwa kuwa watoto wanaonyonyeshwa maziwa hawajazizoea chupa."
Wakati mwingine alimjibu mama aliyekuwa anamtafuta mtu wa kumsaidia kunyonyesha kwa njia ya mtandao: Alikuwa na watoto mapacha walikuwa wana njaa... alikuwa hospitali, alikuwa amefanyiwa upasuaji hivyo hakuweza kuwanyonyesha na hakuweza kukamua maziwa..walikuwa wakiwapa maziwa ya kopo.
"Nilisema sijapata pampu ya maziwa kama unataka hasa nitawanyonyesha watoto wako."
Alisema hajawahi kuonewa wivu na wazazi ambao anawanyonyeshea watoto wake: "Mtu akiomba umnyonyeshee watoto wake ni kwa sababu wanahitaji msaada."
Bi Gadsden huwasaidia wanawake kwa ushauri wakati wakiwa wajawazito na hata baada ya kujifungua.
Lakini anasema kazi yake hii ni tofauti na ajira anayoifanya na anasema hawezi kupokea fedha anapomsaidia mama mwingine unyonyesha.
"Sio weledi, ni suala la kusaidiana kama wazazi," alisema.
Amekuwa akipata maoni tofauti ya watu walipogundua kuwa alikuwa akinyonyesha watoto wa wanawake wengine baada ya kukutana nao mtandaoni: wananiambia "hawakujui hao pengine unaweza kuwa na ugonjwa wowote hata virusi vya ukimwi."
Wanawake wanaonyonyesha hupitia taratibu za vipimo kwanza kabla ya kuingia kwenye mpango huo.

Comments