- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Takriban kila siku nchini Afrika Kusini, kampuni za kusafirisha hela hulengwa na majambazi wanaowavamia na kuwapora. Hata baadhi ya matukio huhusisha utumiaji wa vilipuzi.
Mamilioni ya fedha hutoweka kila siku chini ya mikononi mwa majambazi sugu baadhi yao wakiwa gerezani. Aidha, Maafisa wa polisi wametajwa kuhusika katika baadhi ya wizi.
Kipikinaendela?
Kumekuwa na visa 378 vya uporaji wa pesa ikimaanisha ongezeko la asilimia 104% kati ya mwaka 2016 na 2017.
Huenda hali ikawa mbaya zaidi mwaka huu kwani, kati ya mwezi Mei mwaka uliopita hadi Januari mwaka huu pekee, visa 153 vya uporaji vimeripotiwa ikiwa ni zaidi ya tukio moja kila siku.
Usafirishajii wa pesa kutumia magari yasiyopenya risasi haujaboresha hali kwani wezi hao huyalipua magurudumu kabla ya kutumia vilipuzi kufungua milango ya magari yanayosafirisha pesa.
Baadhi ya walinzi hulengwa pindi wanapotoka wakibeba pesa kutoka ofisi zao wakielekea kuziingisha kwenye gari.
Anneliese Burgess, ni mwandishi wa habari ambaye ametumia miaka ya hivi karibuni kufanya uchunguzi kwa minajili ya kitabu chake, 'Heist! South Africa's cash-in-transit epidemic'.
"Visa hivi vinashtua kabisa: Wanawavamia watu, na kuwatupia risasi," Anneliese ameiambia BBC.
"Majambazi hawa hawathamini uhai wa watu katika taifa hili," anakiri Brig Hangwani Mulaudzi, Msemaji wa polisi Afrika Kusini.
"Viwango vya uhalifu vinaogofya - wanatumia vilipuzi. Ni kundi la watu wanaotumia silaha za hali ya juu." Ameongeza.
Wezi hawa ni kina nani?
Kujiunga na makundi haya, lazima uonyeshe uhodari wako katika uhalifu. Uongozi wa makundi haya unawashirikisha 'mababe 200' wanaohusika kufanya uvamizi katika maeneo mbalimbali kwa ustadi.
Majambazi hao wako kwenye kundi la kati ya watu 10 hadi 20. Kulingana na Yusuf Abramjee Yusuf, anayepinga visa vya uhalifu. Magenge hayo hayana woga kutekeleza uhalifu mchana kwenye miji na hata vijiji. Ameongeza bwana Abramjee.
"Tunakabiliana na uhalifu wa kupangwa," Ameongeza Abramjee.
Polisi wanahusika?
Maafisa wa polisi wanadaiwa kuwatorosha wezi hawa pindi wanapotiwa mbaroni.
Afisa mmoja wa kitengo maalum cha polisi 'Hawks' kinachopambana na majambazi sugu, amekamatwa kwa kupatikana na hatia baada ya kushirikiana na wezi katika tukio moja. Alitarajia kupokea mamilioni ya pesa kama ada ya kazi hiyo!
Hata hivyo tatizo sio polisi pekee.
"Ufisadi unahusika - Kuanzia usafirishaji wa pesa, utoaji wa taarifa za siri, na hawa wakora wanapata taaifa hizo," anafafanua Brigedia Mulaudzi.
"Tunapambana na wahusika wa ndani. Matukio haya sio ya kawaida. Wanafahamu sanduku za pesa ziko wapi." Bwana Abramjee anakubaliana naye.
Mamlaka zinafanyaje?
Kanda za wizi ulioshuhudiwa wiki chache zilizopita, zikiendelea kusambaza, maswali yanaongezeka juu ya kwa nini serkali imezembea kiwango hiki.
Kulingana na Bi Burgess, operesheni za kuwakamata wahalifu zilizoanzishwa wiki chache zilizopita na juma lililopita, zimepelekea kuwanasa washukiwa 13 wa wizi wa pesa zinazosafirishwa akiwemo mwizi mmoja sugu.
Hilo pia limetajwa kutokuwa na mchango wowote kwani kuna madai kuwa baadhi ya wizi hupangwa na wafungwa wanaosaidia kuwaelekeza wenzao kutekeleza ujambazi wa hali ya juu.
Mfungwa mmoja amejigamba kwa jarida la Africa Kusini la Sunday Times kuwa, licha ya kuwa gerezani, yeye hupokea maelfu ya rand kwa kuandaa silaha, kusaidia kwenye mawasiliano na kuwapa ushauri 'wenzake'.
Ingawa siku chache zilizopita, walinzi wa kibinafsi walijitokeza kuandamana dhidi ya ongezeko la visa vya aina hii, haijaweza kuwalinda dhidi ya wizi huu wa hali ya juu.
Wataalam wa usalama wametathmini kuwa, hali hii imefikia kiwango kinachoiwezesha kutambulika kuwa 'janga la kitaifa'.
CHANZO: BBC/SWAHILI
Comments
Post a Comment