Featured Post

KWA NINI WAKENYA WANA WASIWASI KUHUSU MERCURY NA SUKARI



NAIROBI, KENYA
WAKENYA wamekuwa wakitafuta habari mtandaoni kuhusu shaba nyekundu (Copper), Mercury na hamira baada ya serikali kusema sukari feki imekuwa ikiuzwa nchini humo ikiwa na sumu.

Ukaguzi uliofanyiwa sampuli za mabagi 1400 ya sukari haramu iliokamatwa na maafisa wa polisi katika operesheni tofauti, umefichua kuwa baadhi ya sukari ilikuwa na vitu hivyo ambavyo vilikuwa haviwezi kuyeyuka ndani ya maji.
Vipimo hivyo vilivyochukuliwa na serikali na ambavyo matokeo yake yametajwa kuwa ya kushangaza na vimefichua hatari ambazo zimekuwa zikikabili viungo vya ndani vya Wakenya kwa kuwa sukari hiyo inaweza kusababisha saratani mbali na kuathiri viungo vya ndani vya mwili.
Licha ya magunia hayo ya sukari kuwekwa alama za kutokuwa salama kwa matumizi ya binadamu, baadhi ya wafanyibiashara haramu walipanga kilo moja na kilo mbili na kuweka chapa za baadhi ya kampuni za sukari zinazotumika nchini humo kabla ya kuwauzia Wakenya.
Shirika la Afya duniani linasema kwamba Mercury iliomo katika sukari hiyo ni hatari kwa mfumo wa neva wa binadamu.
Vilevile shirika hilo limedai kwamba matumizi ya mercury katika mwili wa binaadamu yanaweza kusababisha athari mbaya katika mfumo wa neva wa binadamu, kinga, mapafu na figo na inaweza kuua.
Vilevile chumvi ya Mercury ni hatari kwa ngozi ya binadamu macho, mfumo wa kusaga chakula na huenda ikweka sumu katika figo iwapo itatumika, kulingana na shirika la WHO.
Siku ya Jumatano waziri Matiangi alikagua magunia 1,365 ya sukari haramu ambayo yalikamatwa katika bohari moja mjini Eastleigh, Ruiru na eneo la viwanda jini Nairobi.
Mashine zilizotumika kutengeza pakiti za sukari hiyo pia zilikamatwa.


Comments