Featured Post

KWA NINI WABUNGE WA TANZANIA WANAPIMWA HIV


Wabunge nchini Tanzania watapimwa virusi vya HIV siku ya Alhamisi ikiwa ni mfano wa kuwa katika mstari wa wa mbele katika jitihada za kupambana na ugonjwa wa ukimwi, kwa mujibu wa gazeti la Citizen la nchini humo.
Mwenyekiti wa kamati ya bunge inayohusika na masuala ya HIV, Oscar Mukasa, alisema Jumanne kuwa kundi hilo litaandaa shughuli kadhaa kuunga mkono kampeni ya serikali ya nchi nzima ya kupima virusi vya HIV, wakati wa kampeni iliyozinduliwa na waziri mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa siku ya Jumanne.

Kampeni hiyo inayofahamika kama 'Furaha Yangu' inafanywa kwa ushirikiano kati ya serikali ya Tanzania na shirika la maendeleo ya kimataifa la Marekani la USAID, mradi ya afya wa Tugole na washikadau wengie katika sekta ya afya.
Majaliwa awaonya walioweka mafuta na sukari kwenye mabohari
Kati ya shughuli zingine ambazo zitachukuliwa na bunge kwa mujibu wa Mukasa ni pamoja na kongamano kuhusu wajibu wa viongozi katika kupambana na virusi vya ukimwi.
Pia kutakuwa na maonyesho kuhusu shughuli zinazofanywa na mashirika yasiyo ya serikali katika kupambana na virusi vya ukimwi kuanzia Ijumaa hadi Jumamosi.

Comments