Featured Post

KUTANA NA EFEME TEMIENOR DOGO ANAYEFANANA NA PAUL POGBA KAMA MAHARAGE

Paul Pogba
Image captionEfeme Temienor (kulia) alipiga selfie na Paul Pogba
Mwanafunzi mmoja kusini mwa London, Uingereza anafanana na nyota wa Ufaransa na Manchester United Paul Pogba kiasi kwamba ametumiwa kumuigiza katika tangazo.

Pogba kwa sasa anacheza Kombe la Duni Ufaransa.
Efeme Temienor alikuwa mara nyingi ameambiwa na jamaa na marafiki kwamba anafanana sana na mchezaji huyo.
Sasa kushabihiana huko kumemfaa kifedha kwani amepewa fursa ya kumwakilisha Pogba katika tangazo la kampuni ya Adida.
Efeme ana miaka 17 na ni mwanafunzi wa kidato cha sita katika shule ya Kikatoliki ya Christ the King.
Anatarajia kutumia pesa atakazolipwa kugharimia karo shuleni na kutimiza ndoto yake ya kujiunga na chuo kikuu.
Yeye ni mchezaji soka pia.
'Hata mamangu aliniamba tulifanana'
Efme alilipwa kwenda Manchester na kisha Madrid kupigwa video za kutumiwa katika video hiyo, ambapo alikutana na Pogba mwenyewe.
Anasema alijaribu kutoonesha kushangazwa kwake na fursa hiyo ya kipekee ya kukutana na nyota huyo.
Mwanafunzi huyo amesema anataka kutumia aliyoyaona na kuyapitia kwa sasa kujifaa kitaaluma.
Ndugu wawili Florentin Pogba na Paul PogbaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionPogba ana ndugu yake kwa jina Florentin ambaye ni mchezaji soka
"Nilijua kwamba nilihitaji kuitumia fursa hii vyema. Sikutaka kiwe kisa cha 'Ni mimi nilifanya hivi," anasema.
Lakini fursa yake ya kushiriki katika video hiyo ya tangazo karibu itibuke njiani.
Alikuwa awali ameombwa na wakala mmoja wa matangazo kumuigiza Pogba mwana mmoja awali.
"Hata mamangu alisema tunafanana sana," anasema.
Lakini babake alimwambia asikubali ofa hiyo na badala yake aangazie masomo na mtihani wake wa GCSE.
Kombe la Dunia lilipokaribia, alipewa fursa hiyo tena na alijipata akiwa nyota tena chuoni, watu walipoona tangazo lake.
"Kila mtu hunitazama. Nafikiri watu hawakuwa wameniamini nilipozungumzia tangazo hilo."
BBC

Comments