Haki miliki ya pichaREUTERSImage captionShangwe iliyosababisha tetemeko la ardhi
Mashabiki wa kandanda wa Mexico hawakuweza kuzuia furaha yao wakati Hirving Lozano alifunga bao dhidi ya Ujerumani wakati wa mechi ya ufunguzi wa Kombe la Dunia.
Lakini ni kweli kuwa shangwe hizo zao zilisababisha tetemeko la ardhi jinsi baadhi ya vyombo vya habari vimeripoti?
Ujumbe wa twitter kutoka taasisi ya jiolojia umesema hivyo.
Ujumbe huo kutoka taasisi inayochunguza mitetemeko ya ardhi unasema, "Tetemeko la ardhi mjini Mexico kutokana na shangwe kufuatia bao la timu ya Mexico dhidi ya Ujerumani wakati wa kombe la dunia mwaka 2018 nchini Urusi."
Kipi haswa kilitokea?
Taasisi hiyo inasema kuwa vifaa vyake viwili vya kupima mitetemo ya ardhi vilitambua kutetemeka kwa ardhi mara tu baada ya goli la ushindi kufungwa.
Haki miliki ya pichaREUTERSImage captionHirving Lozano hakuamini alifunga bao la ushindi
Inasema kuwa ni vifaa vyenye uwezo wa juu wa kutambua vilivyokuwa karibu na mashabiki vinaweza kutambua shughuli kama hiyo.
Moja ya maeneo ambapo masahabiki walikusanyika haliko mbali sana na moja ya vifaa hivyo zilivyonakili tetemeko hilo la ardhi.
Mashabiki walishangilia kwa njia gani?
Jionee mwenyewe:
Haki miliki ya pichaEPAImage captionMashabiki wakiruka kwa shangweHaki miliki ya pichaREUTERSImage captionMaelfu walikusanyika huko Zocalo bustani kuu mjini MexicoHaki miliki ya pichaREUTERSImage captionMashabiki CHANZO: BBC
Comments
Post a Comment