Featured Post

KIBITI YATEKELEZA AGIZO LA SERIKALI KWA KUUZA UFUTA KWA MFUMO WA STAKABADHI GHALANI KWA MKOA WA PWANI

03
 Afisa Kilimo wa Wilaya ya Bwenda  Bahinda akionesha zao la Ufuta na jinsi linavyoandaliwa kwa ajili ya soko

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii, Kibiti
Ufuta ni miongoni mwa mazao ya biashara katika Mkoa wa Pwani ambapo wakulima wamekuwa wanauza kwa wachuuzi na kufanya zao hilo kudumaa kutokana na kuuza kwa bei ya chini.
Wilaya ya Kibiti imekuwa ya kwanza kwa Wilaya za Mkoa wa Pwani kuuza zao la Ufuta kwa mfumo wa stakabadhi ghalani.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Kibiti,  Alvera Ndabagoye amesema kuwa kutokana  na zao hilo kuwa na soko kwa  ndani na nje serikali imeagiza zao hilo kuuzwa kwa mfumo wa stakabadhi ghalani ili kuweza kuwanufaisha wakulima wa zao hilo ikiwa ni pamoja na serikali kupata mapato ya uhakika ambapo Kibiti imeweza kufanikiwa kuuza ufuta kwa mfumo wa stakabadhi ghalani.

Amesema kuwa mara tu baada ya kupata maagizo waliweza kutekeleza na kuweza kufanya minada miwili kwa bei ya sh.2700 kwa kilo moja na kuwa  tofauti na bei ya wachuuzi ambao walikuwa wakinunua kwa sh.1200 kwa kilo.

Ndabagoye amesema kuwa mfumo wa stakabadhi ghalani wametumia ule wa korosho kupitia vyama vya Ushirika ikiwa ni kuhamasisha wananchi kuuza katika mfumo huo.

Amesema kuwa zao hilo lilikuwa likilimwa na wakulima wachache kutokana na baadhi ya wakulima kukata tamaa kwa bei waliokuwa wakiuza ya hasara 

Aidha  Ndabagoye amesema kuwa ni ya serikali ni kuwanyanyua wakulima wasipate hasara na kuamua kuja na mfumo wa sitakabadhi ghalani katika mazao ya Ufuta , Pamba pamoja na kahawa.

Amesema kuwa wemekamata  magari   nane aina ya Fuso yakiwa  na ufuta kutoka wilaya ya jirani wakazikamata Kibiti na kukagua na kubaini wenye ufuta katika magari hayo hawana nyaraka hali ambayo inawapa shaka kuwa baadhi ya wakulima wamezunguka na kwenda kuuza katika wilaya ambayo inapakana nayo.
01
 Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Kibiti,  Alvera Ndabagoye akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na zao la Ufuta na  hatua walizozichukua baada ya serikali kuagiza uzwaji mazao ya Korosho, Kahawa na Ufuta kuuza kwa mfumo wa stakabadhi ghalani katika wilaya ya Kibiti mkoaani Pwani.
02
 Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Kibiti,  Alvera Ndabagoye akionesha zao la Ufuta kwa waandishi habari
04
Sehemu ya magari walioyakamata yakiwa na ufuta na hakuna nyaraka

Comments