Featured Post

JAMII FORUMS WA TANZANIA WASEMA HAWAHUSIKI NA MTANDAO ULIOIBUKA KENYA

Mwanzilishi mwenza wa Jamii Forums Maxence Melo amesema hawana uhusiano na mtandao huo wa KenyaHaki miliki ya pichaJAMII FORUMS
Image captionMwanzilishi mwenza wa Jamii Forums Maxence Melo amesema hawana uhusiano na mtandao huo wa Kenya
Mtandao maarufu nchini Tanzania wa Jamii Forums ambao ulisitisha huduma zake kutokana na sheria za serikali za kudhibiti mitandao taarifa zake zimepakiwa na mtandao wa Kenya ambao una sehemu iliyoitwa Jamii Forums.

Mtandao huo wa Tanzania ni maarufu kwa kufichua mambo tofauti na kama jukwaa la watu kutoa maoni haswa wale walio nchini Tanzania na nchi za kigeni.
Taarifa zake zimeanza kupatikana katika mtandao wa kenyatalk.com licha ya kwamba mtandao huo bado umefungwa.
Waliokuwa wakiutumia mtandao wa Jamii Forums kabla ufungwe, wameanza kutoa maoni kwenye mtandao huo wakifurahia kupata jukwaa jingine la kushiriki kwenye mijadala na kupashana habari mtandaoni.
Mwanzilishi mwenza wa Jamii Forums Maxence Melo amesema hawana uhusiano wowote na mtandao huo wa Kenya.
Jamii ForumsHaki miliki ya pichaINSTAGRAM
Mmoja wa wachangiaji anayejiita Mwifwa ameandika: "Karibu sana mkuu, nafurahi kuwaona mkija na ID zenu za JF kuliko na wale wanaokuja kwa kubadili ID zao."
"Na mimi pia nimefurahi, nilikuwa nafikiria sana jinsi gani mtaweza kuja huku naona matumaini yameanza kurejea, washtue basi na jirani zako. Nasikitika sana sikuwa na mawasiliano na watu wengi ya nje ya jamvini isipokuwa tuliishia PM tu."
Hata hivyo idadi ya watu ambao wanatembela mtandao huo bado ni ya chini.
Jamii Forums hiyo ya Kenya imeibuka siku tatu baada kufungwa nchini Tanzania kufuatia sheria zilizotangazwa na halmashauri ya mawasiliano nchini Tanzania (TCRA) ambazo waanzilishi wa Jamii Forums walizioana kama zilizowalenga.
Mambo muhimu kuhusu kanuni za mitandao Tanzania
Image captionMambo muhimu kuhusu kanuni za mitandao Tanzania
Sheria hizo mpya za TCRA ziliwahitaji wachapishaji wa mitandao na wanablogi kufichua wachangiaji na wamiliki kitu ambacho Bw Melo anasema kuwa ni kizingiti kwa kazi yao.
Kupitia mtandao wa Kenya wa KenyaTalk, watumiaji wa Jamii Forums waliojiandikisha wanaweza kuchangia maoni yao vile walivyokuwa wanachangia awali.
Siku ya mwisho iliyotangazwa na TCRA ya kuwataka wamiliki wa mitandao kujiandikisha na kupata leseni ni Ijumaa tarehe 15 mwezi huu lakini halmashauri hiyo imesema kuwa haitafunga mitando ambayo itakosa kutimizia sheria hiyo hapo kesho.
Lakini mitandao hiyo itapigwa mafuruku kuchapisha taarifa zozote mpya hadi ikamilishe shughuli ya kujiandikisha.

Comments