Featured Post

HALIMA MDEE: UPINZANI KUWASILISHA BAJETI MBADALA TANZANIA

Bunge la Tanzania
Image captionBunge la Tanzania
Upinzani nchini Tanzania umesema kuwa utawasilisha bajeti yake mbadala bungeni siku ya Jumatatu, waziri kivuli wa fedha na mipango Halima Mdee amesema.

Hii itakuwa mara ya kwanza kwa upunzani kuwasilisha maoni yake tangu mkutano wa bajeti bungeni kuanza miezi miwili iliopita.
Siku ya Alhamisi waziri wa fedha na mipango Dkt. Phillip Mpango aliwasilisha bajeti iliogharimu trilioni 32.5 za Tanzania kwa kipindi cha fedha cha 2018/19.
Kulingana na gazeti la mwananchi , mnamo mwezi Aprili, 2018 kambi ya upinzani iliazimia kutowasilisha hotuba za bajeti na nyingine za upinzani hadi watumishi wa sekretarieti yao ambao mikataba yao hutolewa na Bunge watakaporejeshwa kazini.
Akizungumza na waandishi wa habari, jijini Dodoma, Mdee amesema watasoma bajeti yao ili kuwaonyesha Watanzania bajeti mbadala ya upinzani.
"Kama mnavyojua, tumekuwa hatusomi bajeti zetu, lakini kwa mara ya kwanza tutasoma bajeti ya upinzani bungeni Jumatatu," amesema Mdee.
Mdee ambaye ni Mbunge wa Kawe (Chadema), amesema bajeti hiyo itabainisha masuala mbalimbali ambayo Serikali imeshindwa kuyapa kipaumbele.
Upinzani ulisema siku ya Jumamosi kwamba Tanzania inahitaji bajeti yenye maono matano pekee.
Maono hayo ni Elimu, kilimo, Maji , afya .
Kiongozi wa upinzani Freeman Mbowe aliambia waandishi kwamba huku serikali ikiweka nguvu zake zote katika reli ya kisasa ya SGR , Uimarishaji wa mradi wa stima wa Stiegler Gorge na ukarabati wa kampuni ya ndege ya Air Tanzania, upinzani utaangazia maswala matano ambayo ina hakika yatachangia ukuaji wa uchumi.
Kwa sasa kila mtu anayejiweza kiuchumi anapeleka mtoto wake katika shule ya kibinafsi kutokana na hali mbaya ya miundo mbinu katika shule za umma.Hii ndio seshemu inayohitaji uwekezaji, alisema.
Aliongezea kwamba sh.bilioni 700 zilizotengewa mradi wa stima wa Stiegler katika kipindi cha bajeti cha 2018/19 zilifaa kutengewa kilimo ili kupata ufanisi kwa muda mfupi.
CHANZO: BBC/SWAHILI

Comments