Featured Post

BEYONCE NA MUMEWE JAY-Z WATOA ALBAMU YA PAMOJA KWA JINA EVERYTHING IS LOVE, WAIMBA KUHUSU MAPENZI NA TRUMP

Jay-Z and BeyonceHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Kumekuwepo na tetesi kwa muda mrefu lakini hatimaye nyota wa muziki - Beyonce na mumewe Jay-Z - wametoa albamu yao ya pamoja.
Albamu hiyo imepewa jina Everything is Love (Kila Kitu ni Mapenzi).

Albam hiyo inapatikana katika huduma ya kusikiliza na kununua nyimbo mtandaoni inayomilikiwa na Jay-Z kwa jina Tidal.
Beyonce alitoa tangazo la kutolewa kwa albamu hiyo akiwa kwenye jukwaa London na wawili hao waliwashukuru mashabiki wao kwa kujitokeza kuwatazama wakati wa tamasha yao ya kuizuru dunia.
Alisema: "Kwa sababu twawapenda sana, tuna kitu cha kipekee sana kwa ajili yenu."
Beyonce and Jay-Z in their new music video in front of the Mona LisaHaki miliki ya pichaBEYONCE/YOUTUBE
Image captionBeyonce na Jay-Z katika video yao mpya ya muziki, nyuma yao ni picha ya Mona Lisa
Video ilichezwa kwenye skrini na mwishowe kukatokea ujumbe kwamba 'ALBAMU IMETOKA SASA'.
Video ya muziki ya dakika sita ilitolewa punde baadaye, ambayo iliandaliwa katika makumbusho maarufu duniani ya Louvre mjini Paris.
Inaanza kwa wawili hao wakiwa mbele ya Mona Lisa.
Tahadhari: Video hii huenda ikakirihisha baadhi ya watu.
Presentational white space
Hiyo ndiyo albamu yao ya kwanza wakiwa pamoja na imeelezwa kama video ya kusherehekea ndoa ya na asili yao kama watu weusi.
Katika abamu ya karibuni zaidi aliyokuwa ameitoa Beyonce akiwa peke yake kwa jina Lemonade mwaka 2016, alikuwa amezungumzia kutoaminika katika ndoa.
Mwaka mmoja baadaye, Jay-Z alitoa albamu yake kwa jina 4:44.
Kwenye albamu hiyo, alizungumzia kuomba msamaha.
Mashabiki wa wawili hao wamefurahishwa na tangazo la albamu hiyo, baadhi wakilinganisha maisha yao na mchezo wa kuigiza, na kwamba hii ni sura ya tatu.
Presentational white space
Wengine wamefurahia kwamba wawili hao walifanikiwa kuandalia video hiyo katika moja ya makumbusho maarufu zaidi duniani.
Presentational white space
Lakini baadhi hawajafurahia kwamba albamu hiyo inapatikana katika Tidal pekee.
Presentational white space
Presentational white space
Katika albamu hiyo ya nyimbo tisa, wawili hao wanazungumzia uhusiano wao, na pia wanamtaja Rais Trump.
Jay-Z anaimba: "Your president tweeting about Hov like he knows us, my road to the top was to take what you owe us." (Rais wenu anaandika kwenye Twitter kuhusu Hov [njia ya kutumiwa na magari yenye kuwabeba watu wengi Marekani, Jay-Z pia huitwa Hov, kutokana na J-Hova, ambalo limetokana na Jehovah. Jay-Z mwenyewe mara kwa mara amejiita 'miungu' wa rap], barabara yangu ya kuelekea kileleni ilikuwa ya kuchukua kile tunachokudai.@
Aidha, anasema alikataa nafasi ya kutumbuiza katika Super Bowl.
"I said no to the Super Bowl, you need me, I don't need you." (Niliwakataa Super Bowl, nyie mwanihitaji, siwahitaji).
Mwanamuziki huyo wa mtindo wa rap pia amemuunga mkono mchezaji wa NFL Colin Kaepernick, ambaye kwa sasa hana klabu baada yake kulalamika kuhusu ubauzi wa rangi Marekani kupitia kupiga goti wimbo wa taifa ukichezwa.
Beyonce on stage at CoachellaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionBeyonce akiwa Coachella
Baadhi wanaamini kwamba Beyonce alitoa kidokezo kwamba albamu hiyo ingetolewa wakati akitumbuiza Coachella.
Wakati akisubiri hesabu ya muda kabla ya utumbuizaji kuanza, alitoa ishara ya 6 na 3 kwa kutumia vidole vyake.
Albamu hiyo imetolewa siku 63 baadaye.
Novemba 2017, Jay-Z aliambia New York Times kwmaba yeye na Beyoncé walikuwa wameanda kuandaa kitu walipokuwa wanachomoa albamu zao za 4:44 na Lemonade.
"Tulikuwa tunaitumia muziki karibu kama tiba hivi, kujituliza," alisema.
CHANZO: BBC Swahili.

Comments