Featured Post

WIZARA YA ARDHI KUPITIA PROGRAMU YA LTSP YATOA HATIMILIKI ZA KIMILA ZA MASHAMBA KATIKA KIJIJI CHA MPOFU WILAYA YA KILOMBERO MKOA WA MOROGORO

Charles Chunga Msimamizi katika zoezi la uandaaji Hatimili za Kimila kupitia mradi wa Land Tenure Support Programme (LTSP) akiangalia moja ya hati wakati wa kuandaa hatimiliki za kimila Wilaya ya Kilombero mkoa wa Morogoro.

Mjumbe wa Kijiji cha Mpofu Wilaya ya Kilombero mkoa wa Morogoro Emiliana Francis akigawa hatimiliki za Kimila za mashamba wakati wa zoezi la kugawa hati hizo katika kijiji cha Mpofu kitongoji cha Sanje wilaya ya Kilombero mkoa wa Morogoro.
Mwenyekiti wa kijiji cha Mpofu Asukenie Mwanjenje (kushoto) na Mtendaji wa kijiji Emanuel Francis wakipitia hatimiliki za kimila za mashamba wakati wa zoezi la kugawa hati hizo katika kijiji cha Mpofu wilayani Kilombero mkoa wa Morogoro.
Mkulima katika kijiji cha Mpofu Mzee George Mdoti akiangalia jina lake wakati wa zoezi la ugawaji hatimiliki za Kimila katika kijiji cha Mpofu, kitongoji cha Sanje Wilaya ya Kilombero mkoa wa Morogoro.
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Mpofu wilaya ya Kilombero mkoa wa Morogoro wakiangalia majina yao wakati wa zoezi la kugawa hatimiliki za kimila za mashamba katika kijiji hicho.
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Mpofu wilaya ya Kilombero mkoa wa Morogoro waliojitokeza kuchukua hatimiliki za kimila za mashamba wakati wa zoezi la ugawaji hati hizo. (Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi)





Comments