Featured Post

TPA TANGA YAJIVUNIA KASI YA UTOAJI HUDUMA

 MENEJA wa Bandari ya Tanga (TPA) Percival Salama kulia akimueleza Waziri wa Viwanda, Biashara  na Uwekezaji Charles Mwijage  mipango ya bandari hiyo na namna walivyoboresha huduma zao kwa wafanyabiashara wanayoitumia.

 Waziri wa Viwanda, Biashara  na Uwekezaji Charles Mwijage akisalimia na Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga alipokwenda kufungua maonyesho ya sita ya biashara ya kimataifa
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage kushoto akisisitiza jambo kwa Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama mara baada ya kufungua maonyesho ya sita ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella

MENEJA wa Bandari ya Tanga (TPA) Percival Salama amesema wanajivunia kuboreshwa huduma zao kwa kiwango kikubwa ikiwemo uandaaji wa nyaraka kwa kasi na usalama wa kutosha kwa wateja na hivyo kutumia muda mfupi kutokana na taasisi zinazohusika kuwepo sehemu moja hivyo kuwawia rahisi kuweza kufanya shughuli zao kwa wakati mmoja.

Salama aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga kunakoendelea maonyesho ya kimataifa ya sita ya biashara ambapo alisema kutokana na hali hiyo hakuna sehemu ambayo mteja anaweza kupita akikwama bila wao kujua mara kila hatua wanazokuwa wakipitia wanatambua mara moja.

Alisema kuwa sehemu ambazo mteja anaingia kwenye bandari hiyo anapata taarifa moja kwa moja hiyo ikiwa wanakumbana na vikwazo vya namna yoyote zikijitokeza inawawia rahisi kuweza kuona na kuvishughulia kwa muda mfupi ili kuweza kuondoa usumbufu ambazo unaweza kuwakabili wafanyabiashara.

“Kwa kweli huduma za bandari ya Tanga tumeziboresha kwa kiasi kikubwa kutokana na kasi ya uandaaji wa nyaraka lakini hata usalama wa kutosha kwa wateja ambao wamekuwa wakiitumia hali iliyofanya kutumia muda mfupi kutokana na taasisi zinazohusika kuwepo sehemu moja hivyo kuwawia rahisi kuweza kufanya shughuli zao kwa wakati mmoja “Alisema.

Akizungumzia ujenzi wa gati,Meneja Salama alisema gati hilo litakalokuwa la usafirishaji wa mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga hakutakuwa na uchimbaji eneo hilo kwani lina kina zaidi ya mita 20 linajisholeza na meli zinazotarajiwa kubeba tani laki moja hadi laki mbili na nusu kuingia na kufanya upakuaji.

“Sehemu ambayo serikali na TPA inataka kuchimba eneo ambalo kuna gati ya sasa kwa muda wa miaka 129 wanahudumia meli nangani kwani wanaona msingi wake uwezo wa Bandari ya Tanga ni shehena 750,000 lakini mwaka 2016 Bandari hiyo ilizidi kiwango cha uhudumiaji na kufikia tani 843,000 hivyo kutokana na matokeo hayo wakaona ipo haja ya kuboresha Bandari hii”Alisema.

Alisema mwaka Agosti 8 mwaka jana Rais Dkt John Magufuli akiwa mkoani Tanga alitoa maagizo kuwa anataka bandari ya Tanga inayohudumia mizigo sasa ichimbwe na meli zifike kwenye gati ambapo wao tayari wamekwisha kuanza utekelezaji wa agizo hilo.

Meneja huyo alisema wameanza kutekeleza maagizo hayo tayari mkandarasi wa BICO ameingia kazini na amesaini mkataba wa miezi minne kuanza kufanya kazi ya utafiti kwenye eneo la sasa la Bandari ili kujua chini ya bahari kuna udongo wa namna gani ili hatua nyengine ya kumpata mkandarasi kwa ajili ya ujenzi na ushauri zifanyike (Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)

Comments