Featured Post

TANZANIA ITAENDELEA KUSHIRIKI KATIKA ULINZI WA AMANI DUNIANI, BALOZI MAHIGA

1H7A0806
Mhe.Waziri Mahiga akisalimiana na Askari walioshiriki katika Misheni za Ulinzi wa Amani za Umoja wa Mataifa. 1H7A0758
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akihutubia katika maadhimisho ya miaka 70 ya Siku ya Walinda Amani Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Mashujaa vya Mnanzi Mmoja Jijini Dar es Salaam tarehe 29 Mei 2018. 

Siku ya Walinda Amani Duniani huadhimishwa tarehe 29 Mei ya kila mwaka ambapo kaulimbiu ya maadhimisho hayo kwa mwaka huu ni "Ulinzi wa Amani wa Umoja wa Mataifa: Miaka 70 ya huduma na kujitoa (UN Peacekeeping: 70 Years of Service and Sacrifice).

Katika hotuba yake, Mhe. Waziri Mahiga alieleza kuwa yapata miaka 12 tangu Tanzania ianze kushiriki katika ulinzi wa amani chini ya bendera ya Umoja wa Mataifa. 

Pia akasisitiza Tanzania itaendelea kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha inasaidia kupatikana kwa amani katika mataifa mengine kwakuwa hakuna taifa linaloweza kufanikiwa katika maendeleo pasipo kuwepo na amani ya uhakika. " Sio jambo rahisi kukubali kutoa uhai wako kwa ajili ya mtu mwingine lakini Tanzania itaendelea kuungana na mataifa mengine duniani katika kusaidia kupatikana kwa amani ya mataifa hayo" alisema Mhe. Mahiga.

Aidha, Katika kuwakumbuka Walinda Amani wote Duniani waliopoteza maisha wakati wakitekeleza majukumu yao, pamoja na kutoa heshima kwa wale ambao bado wanaendelea na jukumu la kulinda amani, Tanzania imepoteza jumla ya askari wapatao 30 ndani ya miaka 10, pia dunia imepoteza zaidi ya askari 3500 na kwa sasa Tanzania inajivunia kuwa na jumla ya askari wapatao 2,600 wanaohudumu katika misheni sita (6) za ulinzi wa Amani za Umoja wa Mataifa.
1H7A0744
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez akihutubia katika maadhimisho ya siku ya Walinda Amani Duniani ambapo alieleza pamoja na kuendelea kusimamia utekelezaji wa shughuli za maendeleo, Umoja wa Mataifa utaendelea kuhakikisha Dunia inakuwa mahali salama pa kuishi ili kuweza kuyafikia malengo ya maendeleo endelevu. 
1H7A0705
Mhe. Waziri Mahiga akiweka shada la maua katika Mnara wa Mashujaa uliopo Viwanja vya Mnazi Mmoja ikiwa ni sehemu ya kuenzi mchango wa Walinda Amani Duniani. 
1H7A0699
Wakitoa heshima kwa ajili ya kuwakumbuka Walinda Amani, waliosimama mbele kutoka kushoto ni Mhe. Waziri Mahiga akiwa na Mwakilishi kutoka Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Maj. Gen. Henry Kamunde, Bw. Alvaro Rodriguez na Mwakilishi kutoka Jeshi la Polisi Tanzania, Kamishna Nsato Marijani. 
1H7A0821
Mhe. Waziri Mahiga akisalimiana na sehemu nyingine ya Askari walioshiriki katika Misheni za Ulinzi wa Amani za Umoja wa Mataifa. 
1H7A0723
Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Deusdedit Kaganda pamoja na askari kutoka Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) na Jeshi la Polisi Tanzania wakifuatilia hotuba ya Mgeni Rasmi. 
1H7A0736
Sehemu nyingine ya Askari na wageni waalikwa wakifuatilia hotuba ya Mgeni Rasmi. 
1H7A0727
Waheshimiwa Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa nchini wakifuatilia matukio mbalimbali katika maadhimisho hayo. 
1H7A0784
Sehemu nyingine ya Waheshimiwa Mabalozi, Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa nchini na wageni waalikwa wakifuatilia matukio mbalimbali katika maadhimisho hayo. 
1H7A0732
Waheshimiwa Mabalozi na Wageni waalikwa wakifuatilia maadhimisho ya Siku ya Walinda Amani Duniani. 
1H7A0694
Gwaride la heshima kwa Mgeni Rasmi. 
1H7A0679
Askari wa JWTZ wakiingia viwanja vya Mnazi Mmoja. 

Comments