Featured Post

TANAPA WAMKABIDHI MNYETI ZAHANATI YA GIJEDABUNG

IMG-20180531-WA0094
 Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti akipanda mti kwenye eneo la zahanati ya Kijiji cha Gijedabung Wilayani Babati Mkoani Manyara, iliyojengwa kwa shirilingi milioni 83 ambpo shirika la hifadhi za Taifa (TANAPA) imechangia shilingi milioni 65 na nguvu za wananchi wa eneo hilo shilingi milioni 18.
SHIRIKA la hifadhi za Taifa nchini ( TANAPA ) limemkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti, zahanati itakayowasaidia wananchi wa Kiijiji cha Gijedabung kata ya Endakiso Wilbayani Babati, kupata huduma ya afya hivyo kuondokana na adha ya kutembea umbali mrefu wa kilomita 15 kufuata huduma hiyo eneo la Endakiso.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi mkuu wa TANAPA, Allan Kijazi, Meneja  wa ujirani  mwema Ahmed Mbugi wakati akimkabidhi mkuu huyo wa Mkoa alisema ujenzi wa jengo la zahati hiyo hilo ni wakati wa makabidhiano ya zahanati hiyo ni ushirikiano kati ya hifadhi za Taifa Tanzania kupitia  hifadhi ya Tarangire na wananchi wa kijiji cha Gijedabung.

Mbugi alisema Halmashauri ya wilaya ya Babati chini ya mkurugenzi wake Hamis Malinga ni miongoni mwa wilaya nne zinazopakana na Hifadhi ya Taifa ya Tarangire, ambapo wamekua wakishirikiana katika mambo mbalimbali  yakiwemo ya uhifadhi  wa maliasili na mazingira pamoja na maendeleo ya wananchi.

"Naomba nikujulishe kwamba mpango wa ujirani mwema katika shirika la hifadhi za Taifa Tanzania kuwa ulianzishwa mwaka 1988 katika hifadhi ya Taifa Serengeti  kama mradi wa majaribio ukiwa na malengo makuu manne, moja kuweza na kuanzisha uhusiano mzuri kati ya hifadhi na jamii inayoizunguka, pili kuwezesha mpango wa kufikisha Faida za uhifadhi kwa jamii kwa urahisi zaidi, tatu kusaidia jamii kuweza kupata elimu  ya uhifadhi kwanjia rahisi, nne kubuni mpango wa kitaalam wa ushirikishwaji wadau wote wa uhifadhi kwa pamoja," alisema Mbugi.

Aidha alisema kwa kipindi chote hiko hifadhi imekuwa ikiunga mkono jitihada  za kuendeleza jamii ili kufikia malengo waliyojiwekea katika eneo husika.

Akizungumza ujenzi wa zahanati hiyo Mbugi alisema umegharimu  jumla ya shilingi mil.83,700,000, ambapo kati ya kiasi hiko TANAPA imechangi shilingi milioni 65,000,000 ikiwa ni sawa na asilimia 77.7, huku wananchi wakichanga shilingi 18,700,000 ambayo ni nguvu kazi ya makusanyo ya mchanga, mawe, kokoto na maji ambayo ni sawa  na asilimia 22.3 ya gharama zote za mradi huo wa zahanati.

Aidha alifafanua kuwa pamoja na ujenzi wa zahanati hiyo, Tanapa imeweka thamani zilizohitajika katika jengo hilo ikiwa ni pamoja na meza tatu, viti vitano, kabati moja, mabenchi matatu kwa ajili ya kukalia ama kupumzikia wagonjwa, mapanzia pamoja na ubao wa matangazo vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 5,790,000.

Alisema jitihada zao dhidi ya kutoa hamasa juu ya mazingira imekuwa ikitiliwa mkazo kupitia makongamano, warsha, mikutano mbalimbali ambayo wamekua wakiifanya ili kuinusuru dunia na mabadiliko ya tabia nchi ambayo yamekua yakipelekea majanga kasha kuikumba dunia ikiwemo wilaya ya Babati.

"Ni imani yetu  kuwa jengo hili la zahanati unqlolifungua leo itakuwa ni mfano mzuri wa faida za moja kwa moja  za uhifadhi  kwa jamii nakuepuka uharibifu usiokuwa  wa lazima katika maeneo yetu, pia jengo hili litawasaidia wananchi kuondokana na kutemvea umbali mrefu wa kufuata huduma za Afya katika kata ya Endakiso" alifafanua Mbugi.

Aliongeza kuwa TANAPA ni shirika la umma ambalo lilianzishwa  kwa sheria naomba 459 ya sheria za Tanganyika ya  mwaka 1959 na kufanyiwa marejeo kwa sheria namba 282 ya sheria za Tanzania ya mwaka 2002.

"Shirika hili limepewa dhamana ya kusimamia, kuendelea maeneo yote yaliyotangazwa kuwa ni hifadhi za Taifa, mpaka sasa shirika lina jumla ya hifadhi za Taifa 16 zilizoko katika mikoa mbali mbali ya Tanzania, uwepo wa r hifadhi hizi na rasilimali zake imeipa nchi yetu heshima kubwa kimataifa, pia hifadhi hizi zimechangia kiasi kikubwa cha pato la Taifa na maendeleo ya sekta nyingine nchini," alisema Mbugi.

Mkuu wa mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti aliipongeza TANAPA kwa ujenzi wa zahanati hiyo na kuwa tayari zahanati hiyo imekamilika kwa kuwepo na vitanda na huduma zimeshaanza kutokana, hivyo wananchi wametakiwa kuitunza zahanati hiyo, kwa like alichodai kuwa TANAPA haitahusika wala kutoa hata senti  kwa ajili ya kutengeneza chochote, kwani watakua wanapeleka huduma katika vijiji  vingine vinavyozunguka hifadhi ili nao wapate maendeleo.

Alimtaka mwenyekiti wa kijiji cha Gijedabung kuhakikisha anaunda kamati ya kusimamia zahanati hiyo kupitia wananchi wenyewe ambao watasimamia shughuli za kila siku katika zahanati hiyo, pia kamati hiyo ijilizishe uingiaji na utokaji wa dawa, kumekua na  matatizo ya kupotea kwa dawa huku wananchi wakilalamika kutokuwepo kwa dawa, wakati serikali ilishafikisha dawa mahali husika

" Sasa hivi serikali imetoka kwenye sh.bil.40 bajeti  kwa mwaka kwenye uagiziaji wa dawa na kufikia bil.268 na kuwafikia wananchi moja kwa moja, kwa hiyo nategemea hata hapa kuwa dawa zipo za kutosha na wananchi hawakosi dawa labda dawa ziishe nguvu kwa kukosa watumishi, na nesi amenihakikishia kuwa dawa zipo za kutosha, zitarajii kusikia dawa hazipo kwenye vituo vyote vya afya na zahanati zote" alisema Mnyeti.

Akizungumzia suala la uhakiki wa mipaka, Mnyeti alisema hifadhi hizo zinazopakana na wananchi zimekua na migogoro mbalimbali lakini migogo mingine haina tija, kwani wananchi wamekua wakilazimisha kuongia na kugombana na hifadhi pasipokua na sababu kwa kile alichodai kuwa  mipaka wanaifahamu kuwa mipaka ya hifadhi inaishia wapi.

Alisema  wapo wanaofanya kwa makusudi na wengine kwa kutokufahamu, isipokua kwa walio wengi wanafanya kwa kufahamu na makusudi kwa kudai ni mashamba ya babu zao, watambue kuwa ramani zipo ( GN ) zinaonyesha  mipaka yote, hivyo itaonyesha kila kitu.

Aliwaonya wanasiasa wanaowarubuni wananchi kuendeleza migogoro hiyo kama mtaji wa kisiasa, mwenyekiti ama diwani wanaodai kuwa wakipata kura watarudishiwa hilo eneo la hifadhi, hivyo mwenyekiti au diwani aliyewahi kuwadanganya wananchi kwa lugha hiyo ajiandae kupoteza  uongozi huo kwenye uchaguzi ujao.
IMG-20180531-WA0095
 Mbunge wa viti maalum wa Mkoa wa Manyara, Esta Mahawe akipongezwa na Mkuu wa Mkoa huo Alexander Mnyeti na viongozi wengine wa Wilaya ya Babati, baada ya mbunge huyo kumkabidhi mkuu huyo wa mkoa mashuka 10 yatakayotumika kwenye zahanati ya kijiji cha Gijedabung iliyozinduliwa na Mnyeti.
IMG-20180531-WA0096
 Meneja  ujirani mwema wa shirika la hifadhi za Taifa (TANAPA) Ahmed Mbugi, akisoma kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA, Allan Kijazi, taarifa ya ujenzi wa zahanati ya Kijiji cha Gijedabung kwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti, ambapo TANAPA ilitumia shilingi milioni 65 kujenga zahanati hiyo na nguvu za wananchi zikathaminishwa kwa shilingi milioni 18 hivyo jumla kutumika kiasi cha shilingi milioni 83 hadi kukamilika kwake.
IMG-20180531-WA0097
 Kikundi cha ngoma cha Kijiji cha Gijedabung Wilayani Babati Mkoani Manyara, wakicheza ngoma wakati shirika la hifadhi za Taifa (TANAPA) lilipokabidhi zahanati ya kijiji hicho kwa Mkuu wa Mkoa huo Alexander Mnyeti.
IMG-20180531-WA0098
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti akimkabidhi Mkuu wa hifadhi ya Taifa ya Tarangire, Herman Batiho cheti cha kutambua mchango wake wa kusimamia maendeleo baada ya TANAPA kumkabidhi zahanati waliyojenga kwenye Kijiji cha Gijedabung Wilayani Babati.

Comments