Featured Post

SERIKALI KUPITIA WIZARA YA UJENZI,UCHUKUZI NA MAWASILIANO YAOMBWA KUJENGA BARABARA YA BAGAMOYO,MAKURUNGE HADI SAADAN


Afisa Utalii Hifadhi ya Taifa ya Saadan Athuman Mbae akizungumza na waandishi wa habari

AFISA Utalii Hifadhi ya Taifa ya Saadan Athuman Mbae ameiomba Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano kuijenga barabara ya Bagamoyo,Makurunge hadi kuingia Hifadhini ili kuondoa kero kwa watalii hasa nyakati za mvua.

Hayo ameyazungumza kwenye maonyesho ya sita ya biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwahako  Jijini Tanga na kusema ubovu wa barabara hiyo umekuwa kikwazo kwa wageni wengi.

Mbae alisema Hifadhi hiyo imekuwa ikipokea wageni wengi kutokea Jijini Dar es salaam na nje ya nchi kupitia barabara hiyo huku miundombinu hiyo ikiwa haiwezi kupitika kwa nyakati zote.

"Wageni wetu wamekuwa wakitumia barabara hiyo kufika katika hifadhi yetu na tuna idadi kubwa ya wageni hofu yetu ubovu wa barabara unaweza kukwamisha wageni na labda kupungua"Alisema Mbae.

Aidha alisema uwepo wa miundombinu mizuri utarahisisha kwa wananchi toka Mikoa ya Tanga,Dar na Pwani kutembelea katika hifadhi hiyo na kujionea vivutio vilivyopo kwa siku moja.

Alisema ipo haja kwa Serikali kuelekeza nguvu kwenye ujenzi wa barabara hiyo ili kuirahisishia  hifadhi hiyo kupokea wageni wengi kwa nyakati zote na kuongeza pato la Taifa.

Hata hivyo alisema Hifadhi hiyo imeweka mfumo wa matumizi ya master card visa card katika maswala ya ulipaji wa gharama za ulipaji ili kudhibiti mapato yaingiayo kama aerikali inavyoagiza.

"Tunamfumo wa kieletronics kwenye maswala yetu ya malipo na hii itatusaidia kupunguza vitendo vya kihalifu kwa wageni wetu kutokana kutokutembea na fedha nyingi"Alisema Mbae (Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)

Comments