Featured Post

SERIKALI: HISA NA HATI FUNGANI NI UTAJIRI


Na Mutta Robert, Geita
SERIKALI  kupitia mamlaka ya masoko ya dhamana na mitaji nchini,Capital Markert and Securities Authority (CMSA)  iliyo chini ya Wizara ya Fedha na Mipango ,imesema kuwa Ununuzi na uuzaji wa Hisa na Hati fungani za makampuni au serikali ni mbinu nzuri za kujiwekea akiba na kupata faida  kukuwezesha kuwa  tajiri.

Hayo yamesemwa na  Meneja Mahusiano ya Umma CMSA  Charles Shirima katika   mafunzo ya siku moja yailiyofanyika katika ukumbi wa Romani Katoliki maarufu kama maarifa ya nyumbani yaliyo shirikisha  wananchi ,wajasiriamali na wanafunzi wa shule za sekondari na vyuo mjini Geita mkoani hapa.
Alisema kuwa,wajasiriamali na wananchi nchini wakiwa na tabia ya kuweka akiba zao kwa kununua Hisa za makampuni mbalimbali ya kibiashara wanaweza kupata utajiri  kwa njia ya kupata gawio kila mwaka baada ya kampuni husika kupata faida na kugawa faida kwa Wanahisa wake.
Ametaja baadhi ya makampuni amabayo yanafanya vizuri zaidi hadi sasa kwenye soko la Hisa na kutoa gawio la faidi kwa wanahisa wake kuwa ni pamoja na Tanzania Breweries Limited(TBL),TOL Gases Limited,NMB Bank,CRDB Bank,Tanzania Tea Packers Limited,Tanzania Cigarette Company na Tanga Cement Company Limited.
Shirima amewasihi wafanya biashara na wanachi wanao nunua Hisa kwenye makampuni ya kibiashara kuwa wanafuatilia mwenendo wa bei za soko la Hisa ili kutambua ni wakati upi bei imepanda ili waweze kuuza na kupata faida ikiwa ni moja ya mbinu ya kujiongezea faida.
“Faida za kuuza hisa za Kampuni ni kwamba Kampuni inapata mtaji wa kuendesha na kupanua shughuli za uwekezaji wakati huo huo mnunuzi wa Hisa anapata faida ya kuwa sehemu ya wamilki wa kampuni hiyo na kupata faida kutoka kwenye fedha aliyowekeza bila yeye kuhangaika kufanya kazi” anasema Shirima.
Amesema, mbali na gawio la faida ya kila mwisho wa mwaka baada ya kampuni kupata faida,mmiliki wa Hisa anaweza kuuza hisa zake muda wowote na kupata faida baada ya kugundua kuwa kipindi hicho Hisa za kampuni hiyo zimepanda bei kwenye soko la hisa.
Aidha ,aliongeza kuwa mwananchi au mjasiriamali anaweza kununua Hati fungani za serikali au za kampuni kwa makubaliano ya kulipwa kiwango alichonunulia Hati fungani hizo kwa faida au riba ya asilimia iliyokubalika.
Alishauri wafanya biashara na wananchi kutumia akiba zao wanazo jiwekea kuziwekeza kwenye Hisa na Hati fungani ili akiba hizo ziweze kuwaongozea kipato kwasababu zinatengeneza faida.
Akifunga mafunzo hayo Kiongozi kutoka kwenye Taasisi ya maendeleo ya vijana na ushirikiano Tanzania  Aloyce Masana,aliishukuru sana CMSA kwa kutoa mafunzo hayo kwani wafanya biashara wengi walikuwa hawajui kama Hisa na Hati fungani ni uatijiri uliofichika.
Aliwashauri wafanyabishara ,wananchi na wanafunzi kujenga tabia ya kununua Hisa kwenye makampuni ili kupata faida kwani unapata faida bila kupata usumbufu wowote.
Baadhi ya wananchi waliohudhuria mafunzo hao walishauri CMSA kuendelea kutoa mafunzo hayo mara kwa mara   ili elimu hiyo ifike kwa watu wengi zaidi.
Mamlaka ya masoko na mitaji iko katika Mkoa wa Geita ikiendesha mafunzo maalum kwa wanchi ,wanafunzi na wajasiriamali ili kuwa na tabia ya kuwekeza kati Hisa na Hati fungani.

Comments