Featured Post

MO SALAH KUSHIRIKI KATIKA KOMBE LA DUNIA URUSI


Mshambuliaji wa Misri na Liverpool Mohamed Salah ataweza kushiriki katika michuano ya kombe la dunia , tafa lake limetangaza.

Daktari wa timu ya taifa hilo amesema kuwa matibabu ya kiungo huyo wa mashambulizi hayatachukua zaidi ya wiki tatu huku taifa lake likitarajiwa kucheza mechi yake ya kwanza dhidi ya Uruguay mnamo tarehe 15 mwezi Juni.
Salah, 25, alikutana na daktari huyo pamoja na rais wa shirikisho la soka nchini Misri Hany Abu Rida nchini Uhispania siku ya Jumatano.
Shirikisho hilo baadaye lilituma ujumbe wa Twitter likisema: Baada ya kukutana na Abu Rida pamoja na daktari wa timu ya taifa nchini Uhispania leo, Shirikisho la soka linathibitisha kuwa Salah atashiriki katika kombe la dunia, Mungu akipenda.
Awali mshambuliaji huyo hakuwa katika hali ya kuweza kuzungumza zaidi na wanahabari wakati alipowasili nchini Uhispania kwa matibabu ya bega lake.
Mshamuliaji huyo aliyevunja rekodi za ufungaji wa mabao katika klabu yake ya Liverpool alipata jeraha katika mechi ya fainali ya vilabu bingwa ambapo timu yake ililazwa 3-1 na hatimaye mabingwa wa kombe hilo Real Madrid wiki moja iliopita.
Salah alipata jeraha hilo alipokuwa aking'ang'ania mpira na beki wa Real Madrid Sergio Ramos.
Alilazimika kutolewa huku kukiwa na hofu ya iwapo ataweza kuichezea Misri katika fainali za kombe la dunia nchini Urusi mwezi ujao.
Shirikisho la soka nchini Misri FA lilithibitisha siku ya Jumatatu kwamba Salah ataelekea Valencia kwa matibabu ambapo ataandamana na maafisa wa matibabu wa klabu ya Liverpool.
Salah aliwasili mjini humo siku ya Jumanne alfajiri ambapo mwanahabari mmoja wa Uhispania alijaribu kutafuta majibu kuhusu hali yake ,na iwapo ataweza kusafiri kuelekea Urusi na iwapo anamlaumu Ramos kwa jeraha hilo.

Comments