Mhe. Mhandisi Stella Manyanya Naibu Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji akifuatilia Mkutano wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji la Afrika Mashariki uliokuwa ukiendelea.
Mkutano huu ulilenga kujadili na kutolea ufumbuzi masuala mbalimbali yakiwemo ya kiforodha, ambayo yamekuwa kikwazo katika ufanyaji wa biashara za kuvuka mipaka katika Jumuiya.
Mkutano huu uliofanyika kuanzia tarehe 25 hadi 30 Mei, 2018 na kuhudhuriwa na nchi zote wanachama za Jumuiya ya Afrika Mashariki ulifikia tamati tarehe 30 Mei, 2018 jijini Arusha.
|
Prof. Adolf Mkenda Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, akizungumza kwenye Mkutano wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji uliofanyika jijini Arusha.
|
Kutoka kushoto ni Mhe. Dkt. Pindi Chana Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Prof. Adolf Mkenda Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Mhandisi Stella Manyanya (Mb) Naibu Waziri wa Biashara, Viwanda na Uwekezaji, na Bw. Benard Haule Kaimu Mkurugenzi wa Biashara, Uwekezaji, na Sekta za Uzalishaji wakifuatilia mkutano |
|
|
Comments
Post a Comment