Featured Post

MAJALIWA AZINDUA MAADHIMISHO YA MIAKA 15 TANGU KUANZISHWA KWA MFUKO WA DHARURA WA RAIS WA MAREKANI WA KUPAMBANA NA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI (PEPFAR)


Ubalozi wa Marekani
Dar es Salaam
TANZANIA
30 Mei 2018
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Marekani na Tanzania waadhimisha miaka 15 ya ushirikiano katika kupambana na VVU/UKIMWI

KAMPENI YA #PEPFAR15

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikaribishwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu kuongea na kuzindua maadhimisho hayo. Kaimu Balozi wa Marekani nchini, Dkt. Inmi Patterson.

Dar es Salaam, TANZANIA. Jumatano, tarehe 30 Mei, Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania Inmi K. Patterson na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhesimiwa Kassim Majaliwa walizindua rasmi kampeni ya maadhimisho ya miaka 15 ya ubia kati ya Marekani na Tanzania katika kupambana na janga la VVU/UKIMWI chini ya Mpango wa Rais wa Marekani wa Kupambana na UKIMWI (PEPFAR).  Katika hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Kaimu Balozi alitangaza pia kuwa hivi karibuni PEPFAR imevuka lengo muhimu katika utoaji huduma hapa nchini ambapo hivi sasa inatoa matibabu yanayookoa maisha kwa zaidi ya Watanzania milioni moja wanaoishi na VVU. Toka kuzinduliwa kwa PEPFAR na Rais George W. Bush hapo mwaka 2003, Serikali ya Marekani imewekeza zaidi ya Dola za Kimarekani bilioni 4.5 (takriban Shilingi trillion 10.26) katika kudhibiti maambukizi ya VVU/UKIMWI nchini Tanzania.  

Kampeni mpya ya #PEPFAR15 itaendelea kwa mwaka wote wa 2018 ili kuadhimisha mafanikio yaliyofikiwa na nchi zetu mbili katika mapambano dhidi ya VVU na kuendelea kuchukua hatua stahili za kudhibiti kuenea kwa VVU nchini Tanzania.  Ili kudhibiti janga hili, ni muhimu sana kwa Watanzania wote wanaoishi na VVU kupima na kujua hali za afya zao na kisha kuanza matibabu yatakayookoa maisha yao. Katika kufikia azma hiyo, kampeni ya #PEPFAR15 inalenga kupunguza unyanyapaa, kuongeza upatikanaji na matumizi ya huduma zitolewazo za kukabiliana na VVU. Kila mtu atakayepimwa na kugundulika kuwa na maambukizi ya VVU ataanzishiwa matibabu mara moja. Watu wengi walio katika matibabu haya huwa na kiasi kidogo sana cha virusi hivi kiasi kwamba ni vigumu kwao kuwaambukiza wengine, ikiwemo wenza na watoto wao.

“Wakati wa kampeni hii, tutafanya kazi nanyi nyote, pamoja na watu wanaoishi na VVU nchini kote Tanzania ili kusimulia hadithi na habari nzuri (positive stories): habari za watu wanaoishi na VVU ambao wakati mmoja walikuwa dhaifu na wagonjwa lakini sasa wakiwa wenye nguvu na afya, habari za watu waliopima mapema na kuanza matibabu hata kabla hawajaanza kuumwa, habari za watu wanaoishi na VVU walioanza matibabu ya kuokoa maisha ili pia kuwalinda wenza wao na habari za akina mama wanaoishi na VVU wanaopata matibabu ili kuwalinda watoto wao,” alisema Kaimu Balozi Inmi Patterson.

Kwa taarifa zaidi kuhusu PEPFAR nchini Tanzania, tafadhali tembelea tovuti ya Ubalozi wa Marekani: https://tz.usembassy.gov/our-relationship/pepfar/.

Kwa taarifa zaidi, tafadhali wasiliana na Ofisi ya Habari ya Ubalozi wa Marekani Dar es Salaam kwa simu namba: +255 22 229-4000 au kwa barua pepe:  DPO@state.gov.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipeana mkono na Dkt. Leonard Maboko, Mkurugenzi Mtendaji wa Tume yaTaifa ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS)baada ya kuzindua Maadhimisho ya Miaka 15 Tangu Kuanzishwa kwa Mfuko wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kupambana na Kudhibiti Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (PEPFAR) Kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha  Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam, Mei 30, 2018.  Kulia ni Kaimu Balozi wa Marekani nchini, Dkt. Inmi Patterson. 

Sehemu ya washiriki wakitembelea mabanda yaliandaliwa sanjari na maaadhimisho hayo. 


Sehemu ya washiriki wakitembelea mabanda yaliandaliwa sanjari na maaadhimisho hayo.

Sehemu ya washiriki wakitembelea mabanda yaliandaliwa sanjari na maaadhimisho hayo.


Sehemu ya wahudhuriaji wa maaadhimisho hayo wakifuatilia matukio.

Mwenyekiti Mtendaji Mstaafu wa TACAIDS, Dk. Fatma Mrisho akiongea na washiriki wa maadhimisho ya waliohudhuria maadhimisho ya miaka 15 tangu kuanzishwa kwa PEPFAR.

WAZIRI MKUU Mhe. Kassim Majaliwa (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali walioshiriki uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 15 tangu kuanzishwa kwa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kupambana na Kudhibiti Maambukizi ya Virusi vya UKIMWI (PEPFAR) kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam leo Mei 30 2018. Kulia kwake ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, Balozi wa Kaimu Balozi wa Marekani Nchini, Dkt. Inmi Patterson, Mratibu wa PEPFAR, Brian Rettmann na Mshauri wa maswala ya HIV/AIDS, Walter Reed Army Institute of Research Dkt, Janet Mwambona.
Mratibu  wa PEPFAR nchini Tanzania, Brian Rettmann akiongea kuwakaribisha wageni waliohudhuria maadhimisho ya miaka 15 tangu kuanzishwa kwa PEPFAR. 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Kaimu Balozi wa Marekani Nchini, Dkt. Inmi Patterson wakati alipowasili kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam kuzindua   Maadhimisho ya Miaka 15 Tangu  Kuanzishwa kwa Mfuko wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kupambana na Kudhibiti Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (PEPFAR), Mei 30, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (kulia)  na Kaimu Balozi wa Marekani Nchini, Dkt. Inmi Patterson kabla ya Kuzindua  Maadhimisho ya Miaka 15 Tangu  Kuanzishwa kwa Mfuko wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kupambana na Kudhibiti Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (PEPFAR) kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Mei 30, 2018. 

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumza  katika Uzinduzi wa Maadhimisho ya Miaka 15 Tangu  Kuanzishwa kwa Mfuko wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kupambana na Kudhibiti Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (PEPFAR) kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam,  Mei 30, 2018.Uzinduzi huo ulifanywa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipozindua Maadhimisho ya Miaka 15 Tangu Kuanzishwa kwa Mfuko wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kupambana na Kudhibiti Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (PEPFAR) kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam,  Mei 30, 2018. 


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Brian Rettmann, Mratibu  wa PEPFAR nchini baada ya kuzindua Maadhimisho ya Miaka 15 Tangu Kuanzishwa kwa Mfuko wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kupambana na Kudhibiti Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (PEPFAR) Kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha  Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam, Mei 30, 2018. Kutoka (kulia) ni Dkt. Janet Mwambona wa Taasisi HIV/AIDS Treatment Advisory, Walter Reed Army Institute Of Research, Dkt. Leonard Maboko, Mkurugenzi Mtendaji wa Tume yaTaifa ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) na Kaimu Balozi wa Marekani nchini, Dkt. Inmi Patterson (wa nne kulia). (Picha na Robert Okanda na OWM)

Sehemu ya wahudhuriaji wa maaadhimisho hayo wakifuatilia matukio.

Comments