Featured Post

KIKAO CHA KUWAJENGEA UWEZO KONGA ZA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA UKIMWI NA UTEKELEZAJI WA SHERIA CHAFANYIKA JIJINI DODOMA

Pix 1 Kaimu Mkurugenzi
Kaimu Mkurugenzi-TACAIDS Bw.Jumanne Isango akifungua kikao cha kuzijengea uwezo konga za watu wanaoishi na virusi va ukimwi na utekelezaji wa sheria katika ukumbi wa maktaba Jijini Dodoma.Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Tathmini Dkt.Jerome Kamwela na Kulia kwake ni Mratibu wa Kanda ya Dar es Salaam baraza la watu wanaoishi na VVU Tanzania Bi Edna Edson.
Pix 2 Jerome kamwela
Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Tathmini Dkt.Jerome Kamwela akielezea historia ya UKIMWI na taarifa kuhusu matokeo ya utafiti wa kitaifa wa viashiria na Matokeo ya UKIMWI wa mwaka 2016/2017 katika ukumbi wa maktaba Jijini Dodoma.
Pix 3 Bw Richard
Mkurugenzi Idara ya Sera,Mipango na Utafiti-TACAIDS Bw.Richard Nywira akielezea mkakati wa nne wa taifa wa udhibiti wa UKIMWI nchini na Mfuko wa udhamini wa kudhibiti UKIMWI katika ukumbi wa maktaba Jijini Dodoma
Pix 4 mshirki
Mmoja wa Washiriki wa kikao cha kuzijengea uwezo konga za watu wanaoishi na virusi va ukimwi na utekelezaji wa sheria akiuliza swali wakati wa kikao hicho kilichofanyika leo Jijini Dodoma.
Pix 5 washiriki 2
Washiriki wa kikao cha kuzijengea uwezo konga za watu wanaoishi na virusi va ukimwi na utekelezaji wa sheria wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa na wataalam kutoka Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania(TACAIDS) leo Jijini Dodoma.

Comments