Featured Post

KIKAO CHA KUJUANA CHAFANYIKA PEMBA KUTOKANA NA UGATUZI ULIOFANYWA NA SMZ

01
 Kaimu Mkurugenzi wa Baraza la Mji Wete Bi Salma Abuu Hamad akifungua kikao cha Madiwani na walimu wakuu wa skuli za msingi za Mkoa wa Kaskazini Pemba kilichofanyika katika Ofisi za Baraza la Mji Wete.
Na Masanja Mabula, Pemba
 KAIMU Mkurugenzi wa Baraza la Mji Wete Bi Salma Abuu Hamad amewataka walimu wa wakuu wa skuli za msingi kuongeza uwabikaji katika kusimamia maendeleo ya elimu katika skuli zao ili kuongeza ufaulu wa wanafunzi.

Akizungumza na walimu wakuu wa skuli za msingi ambazo zimeinga kwenye mpango wa Serikali wa Ugatuzi , Kaimu Mkurugenzi amesema ni vyema walimu wakuu kuwa makini katika kuwasimamia walimu wao kwani kuongezeka ufaulu wa wanafunzi ni sifa kwa mwalimu.

Amefahamisha kwamba kazi ya uwalimu ni wito , hivyo wanatakiwa kuweka mbele maslahi ya taifa kwanza kwa kuhakikisha walimu wanaowasimamia wanatimiza wajibu  wao kwa wanafanzi.

’’ Pamoja na Serikali ya awamu ya saba kuoongeza mshahara kwa wafanyakazi wake ,lakini natambua walimu kuna malipo mengine huku tuendako , hivyo mnatakiwa kusimamia vyema suala la uwajibikaji sehemu za kazi kwa mnaowaongoza’’ alifahamisha.

Naye Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Fundi Msingi Maulid Ali Salim amuomba uongozi wa Baraza la Mji Wete kuandaa utaratibu wa kuwalipa posho walimu wanaojitolea ili wasivunjike moyo na waendelea kuwasaidia  wanafunzi.

Ameeleza kwamba skuli nyingi zinakabiliwa na upungufu wa walimu na hivyo kulazimika kuwatumia walimu wa kujitolea , ili kuweza kusaidia wanafunzi kuhakikisha wanakamilisha vipindi vyao vya masomo.

‘’Baadhi ya skuli mwalimu akiumwa na wanafunzi wanaumwa , mwalimu akijifungua na wanafunzi wanajifungua , maana yangu ni kwamba mwalimu akiuumwa na wanafunzi hawaji skuli’’alieleza.

Afisa Elimu na Mafunzo ya Amali Mkoa wa Kaskazini Pemba Mohammed Nassor Salim amesema dhamira ya Serikali wa kuzigatua baadhi ya taasisi ni kuleta usimamia imara wa utoaji wa huduma bora .

 ‘’Lengo la serikali ya kufanya ugatuzi ni kurahisisha kupatikana huduma bora kwa wananchi , na kwa upande wa Wizara ya elimu utoaji wa huduma bora umepatikana kwa kipindi hichi cha ugatuzi’’alifahamisha.

Hata hivyo wakichangia katika mkutano huo baadhi ya madiwani wameahidi kuendelea kufanya ufuatiliaji maskulini kwa lengo la kihimiza uwajibikaji wa walimu .
02
 Baadhi ya walimu wakuu wakimskiliza Kaimu Mkurugenzi wa Baraza la Mji Wete Bi Salma (hayupo pichani ) wakati wa mkutano wakujuana kufuatia mfumo uliopo wa ugatuzi.
03
 Afisa Elimu na Mafunzo ya Amali Mkoa Kaskazini Pemba Muhammed Juma Ali akichangia kitu katika Mkutano wa kujuana katikati ni Mwenyekiti wa Baraza la Mji Wete Asaa Juma Ali (kusho) Kaimu Mkurugenzi wa Baraza la Mji Wete Bi Salma Abuu Hamad.

Picha na Makame Mshenga Pemba.

Comments