Featured Post

KATIBU TAWALA MKOA WA KILIMANJARO, MHANDISI AISHA AMOUR AONGOZA WAJUMBE WA KAMATI YA MAAFA KUTEMBELEA BWAWA LA NYUMBA YA MUNGU

Katibu Tawala Mkoa wa Kilimanjaro,Mhandisi Aisha Amour akiwa ameongozana na wajumbe wengine wa Kamati ya Maafa kutembelea Bwawa la Nyumba ya Mungu lililopo wilayani Mwanga ambalo linatajwa ujazo wake wa  maji  wa kawaida umepitiliza na kusababisha  Mafuriko kwa wakazi waishio kando ya Bonde la Mto Pangani.

Mhandisi ,Aisha Amour akitizama kina cha Maji katika Bwawa la Nyumba ya Mungu kilichofikia Mita za ujazo 689.88 .
Sehemu ya Bwawa la Nyumba ya Mungu.
Baadhi ya wakazi wa vijiji vya jirani na Bwawa la Nyumba ya Mungu wakitumia usafiri wa Mitumbwi kusafiri kutoka upande mmoja kwenda upande wa Pili.
Sehemu ya Mapitio ya Maji baada ya kujaa katika Bwawa la Nyumba ya Mungu ,maji haya yanaelekea katika maeneo ambayo yapo makazi na mashamba ya watu yaliyopo pembezoni mwa Bonde la Mto ,Pangani.
Maji yakiendelea kuenea katika uwanda wa Tambarare baada ya kujaa Bwawa la Nyumba ya Mungu.

Na Dixon Busagaga wa Gobu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.

Comments