Wakati Chris Gardner na mtoto wake wa kiume walikuwa wakilala kwenye
sakafu ya choo cha umma, hakuwa kamwe na ndoto kuwa siku moja maisha
yake yangebadilika na hata kufikia kiwango cha kuchezwa kwenye sinema na
kuwa maarufu katika sinena za Hollywood.
Ilikuwa miaka ya 80
wakati bwana Gardner akiwa na umri wa miaka 27, pamoja na mtoto wake
mdogo wa kiume, walikuwa hawana nyumba ya kuishi kwa karibu mwaka mmoja
huko San Francisco nchini Marekani.
Alikuwa akifanya kazi ya mshahara kidogo kama wakala, na hivo hakuwa na na pesa za kutosha kuweza kukodi chumba cha kuishi..
Kwa
hiyvo bwana Gardner ambaye alikuwa ametengana na mpenzi wake,
alilazimika kulala popote pale angefanikiwa kulala akiwa na mtoto wake.
Kando
na kulala kwenye choo ya kituo cha reli, pia walilala kwa bustani za
umma, makanisani na kwenye sakafu ya ofisi alikokuwa akifanya kazi baada
ya kila mtu kuondoka kwenda nyumbani.
Chris Gardner na Will Smith, ambaye alicheza sinema ya maisha yake
Walikula kwenye maeneo ya kupika michuzi na zile
pesa kidogo alikuwa nazo, alimlipia mtoto wake kujiunga na shule ya
chekechea angalau apate nafasi ya kuenda kazini.
Licha ya hayo
yote bwana Gardner alinawiri katika kazi yake, alipomaliza kipindi cha
mafunzo kama wakala, kampuni yake ya Dean Witter Reynolds (DWR) ilimpa
mkataba.
Alipata uwezo ya kutafuta nyumba ya kuishi na mtoto
wake ndipo taaluma yake ikakua kwa haraka. Mwaka 1987 alianzisha kampuni
yake ya Gardner Rich.
Sasa hivi bwana Gardner mwenye umri wa
maiaka 62, anamiliki utajiri wa takriban dola milioni 60, na husafiri
kote duniani kama mzungumzaji wa kuwatia moyo watu, na pia hufadhili
mashirika yanayoshughulikia watu wasio na makao na yale yanayopinga
dhuluma dhidi ya wanawake.
Ukweli kuwa bwana Gardner alikuwa ametatizwa na
maisha alipokuwa mtoto na kutumikia kifungo jela baada ya kukamilisha
mafunzo katika kampuni ya DWR, ni baadhi ya mambo yaliyochangia maisha
yake kuchezwa kwenye sinema wakati alikuwa akiandiska historia ya maisha
yake "The Pursuit of Happyness".
Sinema yenye kichwa kama hicho
ilitolewa mwaka 2006 na msanii Will Smith , akateuliwa kuwa mcheza
sinema bora ya kumuiga Gardner.
Kwa sasa Gardner hutumia siku 200 za mwaka kusafiri kote duniani na kuwahutubia watu.
Comments
Post a Comment