- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani,mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri Wiliam,Mbunge wa jimbo la Mafinga Mjini Cosato Chumi pamoja na mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wilaya ya Mufindi wakiwa nafungua na kuwasha umeme kwa mara ya kwanza katika kijiji cha Lumwago kata ya Upendo wilayani Mufindi mkoani Iringa.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani na Mbunge wa jimbo la Mafinga Mjini Cosato Chumi wakishangilia baada ya kuona kweli umeme umewaka katika kijiji cha Lumwago
Mbunge wa jimbo la Mafinga Mjini Cosato Chumi akiwa Kwenye furaha ya ajabu baada ya kuona wananchi wake wamefanikiwa kupata umeme katika eneo hilo ambazo minasekana linakuwa kwa kasi kubwa
Mbunge wa jimbo la Mafinga Mjini Cosato Chumi akiongea mbele ya wapiga kura wake wa jimbo hilo
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akiwaonyesha wananchi wa jimbo la Mafinga Mjini kifaa cha Umeme Tayari (UMETA).
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
Waziri
wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amewasha umeme kwa mara ya kwanza katika Kata
ya Upendo mtaa wa Lumwago uliyopo wilayani Mufindi, Mkoa wa Iringa.
Uzinduzi huo uliofanyika mbele ya mamia ya wananchi wa mtaa wa
Lumwago ambao walikuwa na furaha baada ya kuona umeme huo umewaka kwa mara ya
kwanza
Waziri Kalemani alifanya uzinduzi huo akiwa katika ziara ya kazi mkoani
Iringa wakati wa kukagua miradi ya umeme inayotekelezwa na REA awamu ya tatu.
Awali, akiongea na wananchi Dkt. Kalemani alisema kuwa wananchi
zaidi ya 200 wataanza kupata umeme kufuatia tukio la kurasimishwa kuwashwa kwa
nishati hiyo Lumwago.
“Tunatoa kipaumbele chetu kwa sasa kwani ni kuhakikisha kwamba
wananchi wengi wanapata umeme na huduma hiyo inakuwa ya uhakika,” alisema Dkt.
Kalemani.
Akifafanua zaidi, alisema kuwa, Serikali imeanzisha harakati za
kufanya ukaguzi kwenye utekelezaji wa Miradi yote ya umeme mkoani humo.
Aidha, alitumia fursa hiyo kuwataka viongozi wa Halmashauri
mbalimbali za vijiji kote nchini, kuhakikisha wanajiandaa kwa ajili ya
kuunganishiwa umeme katika taasisi zote za umma zikiwemo Shule, Vituo vya Afya,
Miradi ya Maji, Masoko na nyinginezo.
Vilevile, alikumbushia umuhimu wa kila mmoja kuhakikisha baada ya
kuunganishiwa umeme katika eneo lake anakumbuka kulipa bili za huduma hiyo
muhimu.
“Usipolipa,Serikali itakukatia umeme hivyo kurudisha nyuma
maendeleo yako,” alisisitiza.
Jambo jingine ambalo Waziri Kalemani alisisitiza ni kwa
wakandarasi kuhakikisha wanawagawia bure wateja 200 wa kwanza watakaojitokeza
kuunganishiwa umeme wa REA, kifaa cha Umeme Tayari (UMETA) kama ilivyoelekezwa
na Serikali na siyo vinginevyo.
Hapo awali,mbunge wa jimbo la Mafinga Mjini Cosato Chumi pamoja na
kupongeza jitihada ambazo Wizara ya nishati imekuwa ikifanya nchi nzima katika
kuhakikisha huduma ya umeme inapatikana katika maeneo mbalimbali, pia alimwomba
Waziri Kalemani kulipa upendeleo jimbo hilo kwa kuwa ndio kitovu cha uchimi wa
viwanda mkoani Iringa.
“Mheshimiwa nikuombe utusaidia kwenye vijiji vilivyobaki katika
jimbo langu kwasasababu wananchi wangu niwachapakazi na wapenda maendeleo”
alisema Chumi
Chumi aliwamwambia waziri kuwa jimbo la Mafinga Mjini ni moja kati
ya maeneo ambayo yanaviwanda vingi ambavyo vinasaidia kukuza uchumi wa nchi
pamoja na kuongeza ajira kwa watanzania wanaoishi katika jimbo hilo.
“Hapa tunazaidi ya viwanda arobain vya mazao ya miti na
tunaviwanda vingine vingi na viwanda vyote hivi vinatumia nisharti ya umeme
hivyo naomba nitoe rai kuwa mji wa mafinga unahitaji sana huduma ya nishati hii
kwa kiasi kikubwa” alisema Chumi
Comments
Post a Comment