- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Na
Lilian Lundo – MAELEZO, Dodoma
Serikali
ya Awamu ya Tano kupitia kaulimbiu yake ya kujenga uchumi wa viwanda imeanzisha
jumla ya viwanda 3,306 kufikia Februari mwaka huu.
Hayo
yameelezwa leo Bungeni Mjini Dodoma na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, alipokuwa akitoa hotuba ya mapitio na mwelekeo
wa kazi za Serikali na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha za ofisi ya
Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2018/2019.
“Serikali
inahamasisha uwekezaji katika viwanda kwa kutoa vivutio vya kodi na
visivyo vya kodi kwa wawekezaji mahiri, kuendeleza na kuboreshsa
miundombinu wezeshi kama vile barabara, reli, bandari, umeme na maji,” alisema
Mhe. Majaliwa.
Aidha
amesema, sera, sheria na kanuni pamoja na kufuatilia utendaji wa viwanda
vilivyobinafsishwa na kuchukua hatua stahiki kwa wamiliki walioenda kinyume na
mikataba ya mauzo.
Aidha,
Mikoa na Halmashauri zote nchini zimeelekezwa kutenga maeneo ya uwekezaji wa
viwanda.
Vilevile
amesema Serikali imechukua hatua thabiti kuhakikisha kunakuwepo na umeme wa
kutoshsa na wa uhakika kwa ajili ya uchumi wa viwanda. Hatua zilizochukuliwa
zinalenga kuongeza uzalishaji wa umeme na kuongeza kasi ya usambazaji wa umeme
vijijini na mijini.
“Katika
mwaka 2017/2018, Serikali imeendelea kutekeleza miradi mikubwa ya Kinyerezi I
(MW 185), Kinyerezi II (MW 240) na mradi wa umeme wa Mto Rufiji (Rufiji Hydro
Power Project – RHPP – at Stiegler’s Gorge) utakaozalisha MW 2,100,” alisema
Mhe. Majaliwa.
Amesema,
Serikali inatekeleza Awamu ya Tatu ya Mradi wa Usambazaji Umeme Vijijini (REA)
ambao umepangwa kufikisha huduma ya umeme kwenye vijiji 7,873 ambavyo
havijapata umeme nchini.
Ameendelea
kueleza kuwa Serikali imeamua kuweka mkazo maalum wa kuyaendeleza kwa kasi
mazao matano ya biashara ambayo ni chai, kahawa, korosho, pamba na tumbaku.
Lengo
ni kuongeza mapato ya wakulima, kuwa chanzo cha kuaminika cha malighafi katika
uchumi wa viwanda na kuendelea kuwa chanzo kikuu cha ajira na fedha za kigeni.
Katika
hotuba hiyo, Ofisi ya Waziri Mkuu na Taasisi zilizo chini yake imeliomba Bunge
liidhinishe jumla ya shilingi 124,954,230,698 kwa mwaka 2018/2019. Kati ya
fedha hizo shilingi 66,162,789,698 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na
shilingi 58,791,441,000 kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.
Pia
Bunge liidhinishe jumla ya shilingi 125,521,100,000 kwa ajili ya mfuko wa
Bunge.
Kati ya
fedha hizo, shilingi 117,205,487,000 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na
shilingi 8,315,613,000 kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.
Comments
Post a Comment