Featured Post

TCRA YASISITIZA MATUMIZI SAHIHI NA SALAMA YA MITANDO NCHINI

Katika kupambana na makosa ya uhalifu wa kimtandao nchini TCRA kwa kushirikiana na kampuni ya Kingdom Heritage ilifanya semina kwa vijana yenye lengo la kuwajengea uelewa wa namna nzuri ya matumizi na usalama Mtandao.

Semina hiyo ilifanyika mwishoni mwaka wiki iliyopita katika ukumbi wa Buni Hub tume ya Sayansi Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na vijana kutoka vyuo na taasisi mbalimbali za serikali na binafsi.
Mwanasheria mwandamizi kutoka TCRA, Dk Philip Filikunjombe alipokuwa akizungumza katika warsha hiyo alisema  kulingana na ukuaji wa miundombinu ya TEHAMA inakuwa kwa kasi na kusababisha matokeo chanya na hasi katika jamii zetu.
“Katika majira haya ya maendeleo ya TEHAMA waharifu wanatumia mwanya huo kufanya uharifu katika mifumo mbali mbalimbali ya Kompyuta hivyo tunatakakiwa kuwa makini kwa watumiaji wa mitandao na wadau wa TEHAMA nchini,” alisema Dk Filikunjombe.

Alisema kama TCRA wanazidi kusisitiza kuhusu matumizi sahihi na salama ya mitandao tena yenye maadili ili kupunguza uhalifu huo, Kwa kushirikiana na Jeshi la polisi kitengo cha uhalifu wa kimtandao.
Mwanzilishi wa Jamii Forums na muwasilishaji mada katika warsha hiyo, Maxence Melo alizungumzia fursa mbalimbali zinazopatikana katika mitandao na miundombinu ya TEHAMA kwa kuwasihi vijana waliokuwa hapo kuwa wabunifu katika majira haya na kuja na mifumo suluhisho itakayoweza kutumika katika jamii zetu.

“Serikali pia kupitia wizara au mamlaka zinazohusika kusapoti juhudi za vijana wabunifu katika TEHAMA  kwa miundombinu na kanuni na taratibu rafiki ili waweze kujifanikisha katika ubunifu wao mpaka kijipatia kipato binafsi na tafa zima kwa ujumla.” Alisema Melo.

Mtaalamu wa masuala ya ulinzi katika mfumo ya Kompyuta na TEHAMA nchini kutoka Kampuni ya Kabolik, Robert Matafu alizungumzia  namna ya kujilinda dhidi ya mashambulizi ya kimtandao na kuwa salama mtandaoni.

“Nchi nyingi za Afrika tunakosa uelewa wa maarifa ya kujilinda na mashambulizi ya kimtandao na kupelekea kupata hasara sana katika taasisi au watu binafsi kutokana na mashambulizi hayo,” alisema Matafu.

Aliongeza: “Takwimu zinaonyesha taasisi nyingi Afrika na Tanzania tukiwepo hatuwekezi vya kutosha katika mifumo ya kiulinzi na usalama mtandao, kwa kufanya hivyo tunaongeza asilimia kubwa za kupata mashambulizi ya kimtandao katika taasisi zetu,” alisema.
Awali, Mkurugenzi wa Kampuni ya Kingdom Heritage waandaaji wa semina hiyo Tunu  Bashemela alisema wao kwa sehemu yao wanaunga mkono juhudi za serikali kupitia TCRA katika kupambana na makosa ya uharifu wa kimtandao kwa kutoa elimu kwa umma hasa vijana ambao ndio rika linalotumia sana mitandao.

“Ili kujua matumizi sahihi na salama vijana mliopo hapa lazima mtambue kuwa sheria ya makosa ya uhalifu wa kimtandao ipo na inafanya kazi lazima tuheshimu na kutii vitu inavyotuzuia kufanya bali tutumie mitandao kwa namna za ubunifu zenye kutuletea fedha na kujiingizia kipato,” alisema Bashemela.



Mwanansheria mwandamizi kutoka TCRA, Dk Philip Filikunjombe

Mwanzilishi wa Jamii Forums mmoja kati ya wawasilishaji mada katika warsha hiyo, Maxence Melo
Mkurugenzi wa Kampuni ya Kingdom Heritage ambao ndio waandaaji wa semina hiyo Tunu  Bashemela
Vijana na mbalimbali watumiaji wa mitandao na wadau wa TEHAMA walioudhulia semina hiyo wakifuatilia kwa makini







Mtaalamu na Mshauri wa masuala ya ulinzi katika mfumo ya kompyuta na TEHAMA nchini kutoka Kampuni ya Kabolik, Robert Matafu katika mjadala na nini kifanyike ili kupunguza na kukomesha matukio ya uhalifu wa mtandao nchini.
  Mtendaji Mkuu wa tzNIC  Abibu Ntahigiye katika mjadala wa katika mjadala na nini kifanyike ili kupunguza na kukomesha matukio ya uhalifu wa mtandao nchini.
Mwanzilishi wa Jamii Forums katika mjadala na nini kifanyike ili kupunguza na kukomesha matukio ya uhalifu wa mtandao nchini.

Comments