Featured Post

RMO, DMO TENGENI SIKU ZA UCHUNGUZI WA SARATANI-WAZIRI UMMY

WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akizungumza leo Jijini Tanga wakati alipozindua kampeni ya chanjo ya saratani ya shingo ya kizazi na uchunguzi wa saratani kwa wakina mama katika kituo cha Afya cha Ngamiani jijini hapa.

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Clemence Marcell akizungumza katika uzinduzi huo ambapo alisema kuwa takribani wanawake 38,000 wanatarajiwa kupatiwa huduma ya chanjo ya saratani ya kizazi mkoani Tanga.
Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Alhaji Mustapha Selebosi akizungumza katika uzinduzi huo
Mratibu wa Shirika la AGPAHI mkoani Tanga Dkt Ben Nahayo Simon akizungumza wakati wa uzinduzi huo
WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akisalimiana na Mganga Mkuu wa Jiji la Tanga (CMO)Jairy Khanga mara baada ya kuwasili kwenye kituo cha Afya cha Ngamiani alipokwenda kuzindua chanjo hiyo

WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kulia akiwa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga Thobias Mwilapwa ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga wakiangalia ngoma ya Msanja wakati wa uzinduzi huo
WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiteta jambo kabla ya kufanya uzinduzi huo kushoto ni Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Tanga Monica Kinala
Mratibu wa Shirika la AGPAHI mkoani Tanga Dkt Ben Nahayo Simon katikati akiteta jambo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga Daudi Mayeji wakati wa uzinduzi huo ksuhoto ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Thobias Mwilapwa ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga
WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kushoto akisalimiana na Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Alhaji Mustapa Selebosi katikati ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga Thobias Mwilapwa ambaye pia ni Mkuu wa wilaya hiyo.
WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akifurahia jambo mara baada ya kuzindua kampeni hiyo ya chanjo
WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akimpongeza mwanafunzi wa shule ya Sekondari mara baada ya kuchanjwa chanjo hiyo kushoto ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga ,Thobias Mwilapwa ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Tanga na katikati ni Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga
WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akitazama namna mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Masiwani Hanifa Juma anavyopatiwa chanjo wakati wa uzinduzi wake leo kushoto ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga ,Thobias Mwilapwa ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Tanga
WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kulia akifurahia jambo mara baada ya kumaliza uzinduzi huo
WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiangalia kadi walizopatiwa wanafunzi hao baada ya kupitiwa chanjo
WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu katika akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa mkoa wa Tanga na wanafunzi mbele waliopatiwa chanjo wakati wa uzinduzi huo
Wanafunzi waliopatiwa chanjo wakionyesha kadi zao
Mratibu wa Shirika la AGPAHI mkoani Tanga Dkt Ben Nahayo Simon kulia akiteta jambo na Dkt Hamisi mara baada ya kufanyika uzinduzi huo

WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amewataka waganga wakuu wote wa mikoa na wilaya nchi nzima kutenga siku moja kwa mwezi kwa ajili ya uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi na matiti kwa wanawake na tezi dume.

Waziri huyo ametoa agizo hilo mkoani Tanga leo wakati akizindua kampeni ya chanjo ya saratani ya shingo ya kizazi na uchunguzi wa saratani kwa wakina mama katika kituo cha Afya cha Ngamiani jijini hapa.

Amesema kuwa hali ya saratani kwa nchi zinazoendelea haswa zilizopo kusini mwa jangwa la Sahara ikiwemo Tanzania wagonjwa wa saratani wamekuwa wakiongezeka kila mwaka.

Amesema kuwa Tanzania kunakuwa na wagonjwa 50,000 waliogunduliwa na tatizo la saratani.

Amesema kuwa katika wagonjwa hao asilimia 33 wanakutwa na saratani ya shingo ya kizazi na asilimia 12 wanagundulika na saratani ya matiti.

Amebainisha kuwa kila katika wagonjwa 100,wagonjwa 80 wanakuwa katika hatua za mwisho za ugonjwa na kufanya matibabu kuwa magumu.

" Narudia kutoa agizo kuwa waganga wakuu wa mikoa na wilaya kutenga siku moja kila mwezi kwa ajili ya uchunguzi wa saratani kwa wanawake na wanaume" alisema.


Kuhusu chanjo amesema kuwa mwaka huu wamelenga kutoa kwa wanawake laki sita na elfu kumi sita kwa mabinti wenye umri wa miaka 14 kutokana na uchache wa chanjo.

" Kwa kuanzia mwaka huu tutatoa chanjo laki sita na elfu kumi na sita kutokana dozi ya chanjo tuliyoipata ni laki sita na elfu ishirini" alisema.

Aidha alitoa wito chanjo itolewe kwa mabinti hali ya kuwa wazazi au walezi wao wameridhia.

" Ninatoa wito kwa watoa huduma za afya hii chanjo mnapoitoa hakikisheni wazazi au walezi wameridhia" alisema

Awali kaimu mganga mkuu wa Mkoa wa Tanga Clemence Marcell alisema kuwa takribani wanawake 38,000 wanatarajiwa kupatiwa huduma ya chanjo ya saratani ya kizazi mkoani Tanga.

Kati ya hao 30,000 ni wanafunzi wa shule mbalimbali na 8,000 kutokana nyumbani watapatiwa katika hospitali na vituo vya Afya 18 vilivyoteuliwa.(Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)

Comments