- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Na Daniel Mbega
BINAFSI
nimefanikiwa kuizunguka Tanzania Bara kwa kiwango kikubwa kwa miaka zaidi ya 25
nikiwa katika shughuli mbalimbali za kihabari na hata kibinafsi, zaidi
nikitumia njia ya reli na barabara.
Ninaifahamu
Tanzania Bara ile ya wakati tukitumia siku tatu kutoka Dar es Salaam kwenda
Mwanza kwa kulazimika kupitia Nairobi nchini Kenya wakati safari yetu ni ya
humu ndani.
Au wakati
tukisafiri kwa siku tatu kutoka Dar es Salaam hadi Sumbawanga mkoani Rukwa kwa
sababu ya ubovu wa barabara.
Ninakumbuka
namna ambavyo wananchi wa mikoa ya Kusini mwa Tanzania - Lindi na Mtwara -
walivyokuwa wakitumia mpaka siku tano kuvuka katika Mto Rufiji!
Leo hii mtu akitaka kwenda Sumbawanga, hahitaji kutumia siku mbili kama
ilivyokuwa zamani, bali atatumia siku moja tu kwa sababu kuna gari la moja kwa
moja kutoka Dar es Salaam hadi Sumbawanga – umbali wa takriban kilometa 1,109.3 kwa siku moja badala ya mbili.
Wasafiri wa kwenda Mwanza, umbali wa kilometa 1,387.3, ambao zamani walitumia siku mbili, tena wakipitia katika nchi jirani ya
Kenya ambako walilazimika kuwa na passport na viza, leo hii wanatumia saa 14 tu
kutoka Dar es Salaam, wakati wale wa kwenda Kigoma na Kagera wanatumia siku
moja na nusu tu badala ya siku tatu hadi nne za zamani.
Siyo hivyo
tu, leo hii unasafiri kutoka Dar es Salaam hadi Mtwara kwa kutumia muda wa saa
saba tu badala ya siku tano zilizokuwa zikitumika wakati ule barabara ilipokuwa
mbovu pamoja na kivuko dhaifu.
Sasa
unaweza kufika Lindi kwa saa tano tu kwa kuwa kwenye Mto Rufiji kuna Daraja la
Mkapa lililowakomboa Watanzania wengi na adha ya usafiri.
Leo
unaweza kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza, au Dar es Salaam hadi Sumbawanga na
hata ukatoka Mbinga hadi Dar es Salaam kwa siku moja tu, yaani usizidishe saa
24.
Hii ni kwa
sababu kuna 'nyoka mweusi', yaani barabara zote ni lami, zinateleza tu bila
shida.
Aidha, leo hii mtu anaweza kutoka Dar es Salaam
kwenda Mbinga (kilometa kama 1,400) kwa siku moja kwani kuna basi la moja kwa
moja kupitia Masasi hadi Songea kwa mwendo wa saa 14 tu.
Nimesafiri
katika kipindi hiki kutoka Iringa kwenda Arusha kupitia
Dodoma-Singida hadi Manyara; kutoka Dar es Salaam-Kiteto-Kondoa hadi Babati;
nimepita Babati-Kondoa-Mayamaya hadi Dodoma; nimepita Mwanza-Shinyanga-Tabora-Mpanda
hadi Sumbawanga mpaka Mbeya; nimetoka Dar es Salaam-Njombe-Songea hadi
Mbambabay mkoani Ruvuma; nimetoka Mwanza-Musoma hadi Sirari; nimezunguka
Mwanza-Sengerema-Geita hadi Bukoba.
Si hivyo tu, nimetoka Bukoba kupita Kahama hadi Dar es Salaam; nimetoka
Shinyanga-Maswa-Bariadi hadi Lamadi; pia nimesafiri kutoka Dar es
Salaam-Lindi-Masasi-Songea hadi Mbambabay na maeneo mengine mengi bila usumbufu
wowote kwa kipindi kifupi tu.
Bado
sehemu ndogo tu ya kutoka Kondoa hadi Babati ambayo inakamilika punde na baada
ya hapo itakuwa ni lami tupu.
Ni maeneo machache tu ambayo bado hayajaunganishwa kwa lazimi ambapo
miradi hiyo ilikuwa imekwama kwa sababu ya ukosefu wa fedha.
Huu ni
mtandao mkubwa wa barabara zenye urefu wa kilometa
6,276.82 ambazo zilitiwa lami kwa gharama ya Dola 102,654.98 milioni.
Tunajivunia yote haya kwa sababu ya jitihada za Serikali ya Chama cha
Mapinduzi (CCM) katika kipindi cha miaka takriban 15 sasa, lakini lazima tuseme
wazi kwamba, yupo mtu aliyekuwa ameaminiwa na serikali hiyo kusimamia
miundombinu ya barabara.
Huyu si
mwingine bali ni Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania ambaye anaendelea kuhakikisha kwamba kila kitu kinakwenda sawa.
Utendaji
wa Dk. Magufuli unajieleza wenyewe katika kipindi chake cha miaka 20 akiwa
ndani ya Baraza la Mawaziri, na zaidi anafahamika namna alivyoisimamia vyema na
kwa mafanikio makubwa Wizara ya Ujenzi (Miundombinu) ambapo katika kipindi
alichokaa kwenye wizara hiyo alifanikiwa kusimamia miradi mbalimbali ya ujenzi
wa barabara.
Pamoja na
kutokamilika kwa baadhi ya vipande hivyo, ambavyo kwa sasa vimeanza
kutengenezwa ili kuikamilisha miradi hiyo, lakini leo hii unaweza kuizunguka
Tanzania Bara bila shida tofauti na miaka ya nyuma.
Mtakubaliana nami kwamba, juhudi za Dkt. Magufuli katika kuimarisha
mtandao wa barabara nchini umeipa nguvu Serikali ya CCM na hakuna mtu anayeweza
kubeza hilo.
Chini ya Dkt. Magufuli barabara zilizojengwa kwa
kiwango cha lami ni pamoja na: Singida-Iguguno (76km); Sekenke-Shelui (33km);
Mwandiga-Manyovu (60km); Kigoma-Kidahwe (35.7km); Bonga-Babati (19.20km);
Tabora-Urambo (42km); Kyaka-Bugene (59.1km); Dareda-Minjingu (84.6km);
Kidahwe-Uvinza-Ilunde (76.6km); Isaka-Ushirombo (132km); Kilwa Road Phase III
(1.5km); Nyanguse-Musoma (85.5km); na Kagoma-Lusahunga (154km ).
Nyingine ni Isuna-Singida (63km);
Tarakea-Rongai-Kamwanga (32km); Iringa-Migori (95.1km); Migori-Fufu Escarpment
(93.8km); Nangurukuru-Mbwemkuru (95km); Shelui-Nzega (112km);
Kyamorwa-Buzirayombo (120km); Manyoni-Isuna (54km); Arusha-Namanga (104.2km);
Chalinze-Tanga Phase I (125km); Daraja la Umoja (10.7km) linalounganisha
Tanzania na Msumbiji; Sengerema-Usagara (40km); Buzirayombo-Geita (100km);
Geita-Sengerema (50km); Dodoma-Mayamaya (43.65km); Manyoni-Itigi-Chaya (89.3km);
Puge-Tabora (56.1km); Handeni-Mkata (54km); Korogwe-Handeni (65km);
Katesh-Dareda (73.8km); Singida-Katesh (65.1km); Tanga-Horohoro (65km); na
Peramiho Junction-Mbinga (78km).
Barabara nyingine ni Sam Nujoma jijini Dar es Salaam
(4km); Magole-Turiani (48.6km); Tabora-Urambo (52km); Dumila-Rudewa (45km);
Mbeya-Lwanjilo (36km); Lwanjilo-Chunya (36km); Mwigumbi-Maswa-Bariadi-Lamadi
(71.8km); Nzega-Puge (58.8km); Fufu Escarpment-Dodoma (70.9km);
Sumbawanga-Kanazi (75km); Kanazi-Kizi-Kibaoni (76.6km); Sumbawanga-Matai-Kasanga
(112km); Ikana-Laela (64.2km); Masasi – Mangaka Phase I (15km); Masasi –
Mangaka Phase II (17.6km); Masasi – Mangaka Phase III (22.5km); Dodoma –
Manyoni (127km); Barabara ya Kilwa Phase II (5.1km); Tinde – Mpaka wa
Shinyanga/Mwanza (96km); Nzega-Tinde-Isaka (73km); Morogoro – Dodoma (256km);
Marangu – Rombo Mkuu (32km); Rombo Mkuu – Tarakea (32km); Barabara ya Mandela
(15.6km); Tabora – Nyahua – Chaya (85km); Ushirombo – Lusahunga (110km);
Namtumbo – Kilimasela Lot A (60.7km); Matemanga – Tunduru Lot C (58.7km);
Kilimasela – Matemanga Lot B (68.2km); Iyovi-Iringa-Mafinga (149.6km); Laela –
Sumbawanga (95.31km); Chalinze – Tanga Phase II (120km); Tanga Magharibi PMMR
(224.8km); Tanga Mashariki (116.8km); Ndundu – Somanga (60km); Mbwemkuru –
Mingoyo Lindi (95km); Arusha – Minjingu (98km); Songea – Namtumbo (67km);
Tunduma – Ikana (63.2km); Mkuranga – Kibiti (60km); na Bagamoyo – Msata (64km).
Hivi sasa kuna miradi mingine ya barabara ambayo
inaendelea kufanyiwa pembuzi yakinifu na nyingine zimekwishapata wakandarasi
kwa ajili ya ujenzi.
Tunafahamu kuhusu ujenzi wa barabara za juu pale
Tazara na Ubungo ambao unaendelea na kukamilika kwake kutasaidia kubadili sura
ya Jiji la Dar es Salaam pamoja na kupunguza msongamano wa magari.
Hakuna shaka
yoyote kwamba mafanikio haya ni makubwa na tunahitaji kuunga mkono jitihada
hizi za serikali kwa maendeleo ya Watanzania wote.
0656-331974
Comments
Post a Comment