|
Mkurugenzi
Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Masha Mshomba (kulia), akipokea tunzo na cheti kutoka kwa Bw. Eric
Shitindi katibu Mkuu Wizara ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu baada ya
MFuko kushinda nafasi ya pili katika masuala ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi
katika maadhimisho ya Siku ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi Duniani tarehe 28
Aprili katika Uwanja wa Kichangani Iringa.
NA
MWANDISHI WETU, IRINGA
MFUKO
wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) umeibuka mshindi wa pili katika masuala ya
usalama na afya mahala pa kazi katika maadhimisho ya siku ya usalama na afya
mahala pa kazi nchini ambayo huadhimishwa duniani kote tarehe 28 Aprili kila
mwaka.
Maadhimisho
haya huratibiwa na Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA) nchini na
kwa mwaka huu yamefanyika Mkoani Iringa yakitanguliwa na maonyesho kutoka kwa
wadau kuanzia tarehe 26 Aprili na kufikia kileleni leo tarehe 29.
Mgeni
Rasmi katika kilele cha Siku ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi Duniani Mhe.
Jenista Mhagama (Mb) Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi,
Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu ameipongeza WCF kwa ushindi walioupata na
kuwasihi kuendelea kutoa elimu kwa wadau wake.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mkuu wa WCF Masha Mshomba, amefafanua kuwa moja ya
malengo ya uanzishwaji wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi ni kukuza na kuendeleza
mbinu za kuzuia ajali, magonjwa ama vifo mahala pa kazi.
Mshomba
ametoa ufafanuzi huo leo katika viwanja vya Kichangani mkoani Iringa baada ya
kupokea tuzo na cheti cha Mshindi wa pili katika masuala ya afya ya usalama
mahala pa kazi.
Aidha,
akikabidhi tunzo hiyo kwa niaba ya Mgeni Rasmi, Katibu Mkuu Wizara ya Kazi,
Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Bw. Eric Shitindi ameupongeza Mfuko kwa
kuendelea kufanya kazi vizuri katika nyanja tofauti tofauti pamoja na kwamba
hauna miaka mingi sana toka uanzishwe. “Tunajivunia sana kuona ya kwamba Mfuko
umeweza kulipa fidia stahiki kwa wakati, kitu ambacho kilikuwa changamoto hapo
awali” Aidha, pongezi zangu ziwafikie kwa kuanzisha mifumo inayoboresha huduma
kwa waajili na waajiliwa wote ikiwemo mifumo ya ki- electroniki inayowazezesha
waajili kujisajili, kulipia michango na kufuatilia michango yao.
Mfuko
umehitimisha maadhimisho ya siku ya usalama na afya mahala pa kazi katika Mkoa
wa Iringa na unajiandaaa na semina ya wadau itakayofanyika tarehe 30 Aprili na
hatimaye kushiriki katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani Tarehe 01
May 2018.
|
|
Katikati
Bw. Eric Shitindi Katibu Mkuu Wizara ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu
akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Mfuko baada ya kupokea tunzo na
cheti katika maadhimisho ya Siku ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi katika
Uwanja wa Kichangani Iringa. (Akishikilia kombe pamoja na Bw. Shitindi ni
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi Bw. Masha Mshomba
|
Bw.
Ibrahim Mussa Afisa Madai Mwandamizi –
WCF akimhudumia mteja aliyetembelea banda ya WCF katika maonyesho
yaliyofanyika katika viwanja vya
Kichangani Iringa.
Bw. Masha Mshomba akionyesha tuzo na cheti ambavyo Mfuko umetunukiwa.
Mkurugenzi wa Tiba na Tathmini wa WCF, Dkt. Abdulsalaam Omar (wapili kushoto), Mkurugenzi wa Uendeshaji Bw. Anselim Peter wakiwa ameshika tuzo hiyo huku, Meneja Tathmini ya Usalama na Afya mahala pa Kazi wa Mfuko huo, Bi. Naanjela Msangi, (kulia) na Afisa Mkuu wa Matekelezo, Bi. Amina Likungwala, wakionyesha vyeti vya ushindi wa pili na cha ushiriki.
Mkurugenzi wa Tiba na Tathmini wa WCF, Dkt. Abdulsalaam Omar (katikati), akiwa ameshika tuzo hiyo huku, Meneja Tathmini ya Usalama na Afya mahala pa Kazi wa Mfuko huo, Bi. Naanjela Msangi, (kulia) na Afisa Mkuu wa Matekelezo, Bi. Amina Likungwala, wakionyesha vyeti vya ushindi wa pili na cha ushiriki.
|
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa WCF, Bw. Fulgence Sebera, akizungumza |
Comments
Post a Comment