Featured Post

JUMIA YAKUA KWA ASILIMIA 42



IDADI ya watu milioni 550 barani Afrika walitembelea Jumia mwaka 2017

Mizigo zaidi ya milioni 8 ilisafirishwa kupitia mtandao wa Jumia


Jumia, kampuni inayoongoza kwa biashara ya mtandaoni Afrika, imetoa ripoti yake ya kifedha ambayo inaonyesha ukuaji kwa asilimia 64.5 na kufikia kiasi cha EURO milioni 197.9 (kiasi ambacho ni sawa na ongezeko la asilimia 113) katika robo ya mwisho ya mwaka 2017, ukilinganisha na kiasi cha EURO milioni 120.2 katika robo ya mwisho ya mwaka 2016. 

Jumia imeongeza kiwango cha mauzo katika mtandao wake kwa ukuaji wa asilimia 94 katika robo ya mwisho ya mwaka 2017.

Jumia imeshuhudia ongezeko la mauzo kwa asilimia 41.8 mwaka baada ya mwaka kutoka EURO milioni 357.5 katika mwaka 2016 na kufikia EURO milioni 507 mwaka 2017 (kiasi ambacho ni sawa na ongezeko la asilimia 79), hali iliyochangiwa na mabadiliko ya hali ya uchumi, pamoja na kuendana na mahitaji ya soko, kikubwa zaidi ni ongezeko la wafanyabiashara pamoja na bidhaa na huduma zinazopatikana. 
Jumia inaendelea kubainisha mahitaji ya kila siku ya wateja katika masoko yake, na kupelekea ongezeko thabiti la idadi ya mauzo yanayofanyika na kuongezeka kwa wateja.


Sacha Poignonnec na Jeremy Hodara, ambao ni Wakurugenzi Wakuu wa Jumia wamebainisha kwamba: “Tumefanya jitihada muhimu za kimaendeleo kwa mwaka 2017 hususani kwenye ukuaji wa biashara, zikichochewa na uvumbuzi wa kiteknolojia na kuboresha utoaji wa bidhaa na huduma zinazohitajika sokoni. Ukuaji huu unadhihirsha kasi kubwa katika biashara na masoko yetu ya msingi, pamoja na kuongezeka kwa ueneaji wa matumizi ya huduma za mtandaoni miongoni mwa Waafrika. Pia tunaona matokeo mazuri kutokana na mikakati yetu ya kuendeleza mifumo ya uendeshaji wa shughuli kwenye mtandao na mfumo wetu wa malipo. Wateja wetu wanaendelea kunufaika na upatikanaji wa huduma nzuri, bidhaa bora, maboresho ya huduma kwa wateja, na urahisi mkubwa wa kuweza kufanya huduma kwa njia ya mtandao.”



Mambo Muhimu kwa mwaka 2017



Idadi ya watu milioni 550 barani Afrika walitembelea Jumia mwaka 2017. Mafanikio mengine kwa mwaka 2017 yanajumuisha kuongezeka kwa kasi kwa bidhaa kwenye mtandao wake kutoka 50,000 mwaka 2012 na kufikia zaidi ya milioni 5 mwaka 2017.



Jumia imeshuhudia mafanikio makubwa katika kampeni yake ya ‘Black Friday’ ambapo wateja zaidi ya milioni 100 walitembelea kwenye mtandao wake, na kuvunja rekodi zote za kipindi cha nyuma katika nyanja zote zikiwemo: wateja wapya, idadi ya mauzo, bidhaa zilizouzwa, na watu waliotembelea mtandao.



Kampuni ilizindua mfumo wake wa malipo, ‘JumiaPay’, ili kuwezesha zaidi shughuli za uuzaji na ununuaji baina ya wafanyabiashara na wateja, pamoja na kutoa suluhisho kutokana vigezo na mahitaji maalum ya eneo husika.



Jumia ilizindua mfumo wa malipo kwa wateja kwa kutumia simu za mkononi (‘Jumia One’), unaowawezesha wateja kupata huduma kwa urahisi kwa njia ya kidigitali kama vile kulipia muda wa maongezi, vifurushi vya intaneti, luninga, na huduma nyinginezo. Hatua kwa hatua, ‘Jumia One’ inaiunganisha mifumo mingi ya mtandaoni na kifedha ili kuwasaidia wateja kuokoa muda na fedha pamoja na kuzifikia idadi kubwa ya huduma tofauti kwenye programu moja ya simu.



Mizigo zaidi ya milioni 8 ilisafirishwa kupitia mtandao wa Jumia, mafanikio ya kipee kabisa. Kampuni inaendelea kudhibiti mifumo ya uendeshaji na usafirishaji kupitia mtandao uliojumuisha watoa huduma wa maeneo husika, kwa kutumia teknolojia ya Jumia pamoja na takwimu na taarifa mbalimbali

Comments