Featured Post

WCF YAWAELIMISHA MAAFISA WAAJIRI KUHUSU MISINGI YA KULINDA USALAMA NA AFYA ZA WAFANYAKAZI MAHALA PA KAZI


 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Anselim Peter, (aliyesimama), akitoa hotuba ya ufunguzi wa semina juu ya masuala ya msingi ya kulinda usalama na afya mahala pa kazi na Fidia kwa wafanyakazi kwenye ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, (JNICC), jijini Dar es Salaam Machi 22, 2018. Wengine pichani  I Mkurugenmzi wa Huduma za Tiba na Tathmini wa WCF, Dkt. Abdulsalaam Omar, (katikati), na Meneja wa Tathmini ya hatari mahala pa kazi, (Workplace Risk Assesment Manager), Bi. Nanjela Msangi.



NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

NIWAJIBU wa mwajiri kutoa taarifa kwa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), ya kuumia kwa mfanyakazi wake ikiwa ni pamoja na kifo.

Hayo yamesemwa leo Machi 22, 2018, na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Anselim Peter, wakati akifungua semina ya siku moja iliyowaleta pamoja mameneja na maafisa waajiri kutoka sekta ya umma na binafsi jijini Dar es Salaam kwenye ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Wafanyakazi, (JNICC), jijini Dar es Salaam.

Pia ni wajibu wa mwajiri kumpatia vifaa vya kujilinda (protective gears), mfanyakazi wake,  kulingana na kazi anayofanya ili kumlinda na madhara yatokanayo na kazi anayofanya.

“Lengo la Mfuko sio tu kusajili waajiri na kupokea michango lakini pia ni kukuza mbinu za kuzuia ajali, magonjwa ama vifo katika maenmeo ya kazi na ndio msingi mkuu wa seemina yetu ya leo, katika kutekeleza jukumu letu hili ni kujenga uelewa wa kutosha kwa mwajiri ili kuhakikisha kwamba tunajenga mazingira ya kuzuia ajali sehemu za kazi.” Alisema na kuongeza.

Nia ya Mfuko ni kuona tunakinda nguvu kazi ambapo tunahakikisha kwamba wafanyakazi hawa wawapo kazini hawaugui au kuumia au kufariki kutokana na kazi, alissisitiza Bw. Peter.

Alisema washiriki watapatiwa mafunzo mbalimbali yanayolenga kujenga mazingira mazuri kwa wafanyakazi wawapo kazini. “Mtaelimishwa kuhusu masuala muhimu kuhusu Mfuko kupitria mada mbalimbali zitakaziowasilishwa na wataalamu, kutekeleza vyema jukumu la kuhamasisha na kusisitiza wafanyakazi kuzingatia kanuni za kulinda usalama mahala pa kazi, masuala ya fidia kwa wafanyakazi, wanaoumia, kuugua au kufariki kutokana na kazi.” Alifafanua.
Alisema, uwepo wa Mfuko umeleta faraja kubwa kwa waajiri na wafanyakazi ambapo leo hii, endapo Mfanyakazi atapata madhara kutokana na kazi, anao uhakika kuwa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, utatoa fidia stahili kulingana na mikataba ya kazi na mwajiri husika.
“Yote haya yanawapa wafanyakazi utulivu wawapo kazini kwani wanajua kuwa lolote likitokea ipo taasisi ambayo itasimamia na kunifidia nah ii inaondoa migogoro sana sehemu za kazi.” Alisema.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini wa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), Dkt. Abdulsalaam Omar alisema Mwajiri anao wajibu wa kumuwekea mazingira bora, salama na yana afya ili aweze kufanya kazi kwa ufanisi. “Sio tu kupewa mazingira mazuri lakini pia apewe vifaa kinga kitaalamu vinaitwa personal protective equipmentskwa kufanya hivyo utakuwa unalinda usalama wake na afya yake.” Alisema Dkt. Omar.
“Mfanyakazi anayo haki ya kumdai mwajiri wake kumpatia vifaa vya kujilinda na mwajiri haruhusiwi kumfukuza kazi au kumwadhibu mfanyakazi anayedai mazingira bora toka kwa mwajiri wake ili aweze kuwa amekingwa.” Alifafanua.
Pia alisema mfanyakazi naye anao wajibu kuvitumia vifaa vya kujikinga katika mazingira yake ya kazi kwa usahihi na wakati wote awapo kazini.
Kwa upande wake mmoja wa washiriki wa semina hiyo, BwAlly Kinga Shamte, Meneja Rasilimali watu wa Kampuni ya Badri East Africa Enterprises, mesema tayari kampuni yake imeanza kufaidika na kujiunga na Mfuko huo ambapo mmoja wa wafanyakazi wake, aliyepata shoti ya umeme ameweza kushughulikiwa na Mfuko na tayari anahudumiwa.
“Hii imekuwa ni kama Bima kwa wafanyakazi wetu, sisi hatushughuliki tena na madhara anayopata mfanyakazi, tulichofanya ni kujaza fomu zao za taarifa ya ajali hiyo na mara moja walianza kumshuhhulikia.” Alisema.

 
 Mshiriki akisoma machapisho yenye taarifa za WCF
 Dkt. Abdulsalaam (katikati), akifafanua baadhi ya hoja. Wengine, ni Bi. Naanjela Msangi, (Kushoto), na Bw. Faustine George
 Bi. Naanjela Msangi.
 Bw. George Faustine, Afisa Matekelezo-WCF
George Faustine, Afisa Matekelezo-WCF
  Bi. Naanjela Msangi(kulia), akibadilishana mawazo na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano WCF, Bi. Laura Kungenge
 Baadhi ya washiriki wakijadiliana jambo
 Baadhi ya washiriki wakipitia vipeperushi vyenye maelezo kuhusu kazi za Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF).
 Baadhi ya washiriki wa semina.
 Washiriki wakijiandikisha
 Washiriki wa semina wakifuatilia mada mbalimbali kutoka kwa wataalamu wa WCF.
 Robert Duguza, Afisa wa usalama na afya mahala pa kazi, akizungumza wakati wa semina hiyo.




Bi. Tumaini J.Kyando, Afisa Mwandamizi wa Afya na Usalama mahala pa Kazi kutoka Mfuko w aFidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), ambao ndio walioandaa semina hiyo, akinakili baadhi ya hoja zilizojitokeza.
Baadhi ya washiriki

Comments