|
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), Charles Kichere akimkabidhi Mfanyabiashara Mshamu Nakukwa kitambulisho wakati wa uzinduzi wa zoezi la utoaji vitambulisho Dar es Salaam Machi 27, 2018.
|
UZINDUZI WA UTOAJI WA VITAMBULISHO KWA
WAFANYABIASHARA WADOGO
27 Machi, 2018 - Dar es Salaam.
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imezindua rasmi utoaji wa vitambulisho vya Wafanyabiashara wadogo walio kwenye sekta isiyo rasmi ikiwa ni pamoja na Wamachinga.
Utoaji wa vitambulisho kwa wafanyabiashara hao unatokana na marekebisho ya Sheria ya Usimamizi wa Kodi ya Mwaka 2015 yaliyofanywa na Kikao cha Bunge la Bajeti la Mwaka wa Fedha 2017/2018 ambapo moja ya marekebisho hayo ni kuwatambua na kuwapatia vitambulisho maalum wafanyabiashara wadogo walio kwenye sekta isiyo rasmi.
Zoezi hili linatekelezwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa kushirikiana na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) pamoja na Idara ya Uhamiaji.
TRA kwa kushirikiana na wadau husika hapo juu, ilianza kutekeleza jukumu hilo kwa kuutambua Umoja wa Wamachinga wa Kariakoo jijini Dar es Salaam na kufanikiwa kuwapatia vitambulisho vya Taifa na Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) ambapo leo hii baadhi yao wamepatiwa vitambulisho maalum vya wafanyabiashara wadogo kama ishara ya uzinduzi wa utoaji wa vitambulisho hivyo.
Baada ya mafanikio haya, zoezi la kutambua vikundi mbalimbali vya wafanyabiashara wadogo na kuwapatia kitambulisho cha Taifa na Namba ya Utambulisho wa Mlipa kodi linaendelea kufanyika nchi nzima.
Aidha, Ili wafanyabiashara wadogo waweze kupata vitambulisho hivyo maalum wanatakiwa:-
Kujiunga katika vikundi maalum vinavyotambuliwa kisheria na Serikali,
Kuwa na Kitambulisho cha Taifa,
Kuwa na Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi ya kikundi alichojiunga nacho na
Kuchangia shilingi 10,000/=.
Vitambulisho hivyo maalum kwa wafanyabiashara wadogo walio kwenye sekta isiyo rasmi vitadumu na kutumika kwa kipindi cha miaka mitatu (3) na vitakuwa na maelezo ya mfanyabiashara husika kama vile:-
Jina na picha ya mfanyabiashara,
Jina la eneo analofanyia biashara,
Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi na
Sahihi ya mfanyabiashara.
Imetolewa na:
Charles E. Kichere
KAMISHNA MKUU
|
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akimkabidhi mmoja wa wafanyabiashara kitambulisho na Namba ya Utambulisho ya Mlipakodi (TIN) wakati wa uzinduzi wa zoezi la utoaji vitambulisho Dar es Salaam Machi 27, 2018. Pamoja naye ni Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), Charles Kichere (mwenye miwani) na viongozi waandamizi wa Mamlaka hiyo. |
|
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), Charles Kichere (wa pili kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema wakipata maelezo kutoka kwa Afisa wa Kodi, Dina Kaka jinsi ya kuandaa risiti ya kitambulisho cha Mfanyabiashara wakati wa uzinduzi wa zoezi la utoaji vitambulisho. |
|
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), Charles Kichere akimkabidhi mmoja wa wafanyabiashara kitambulisho na Namba ya Utambulisho ya Mlipakodi (TIN) wakati wa uzinduzi wa zoezi la utoaji vitambulisho Dar es Salaam Machi 27, 2018. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema na viongozi waandamizi wa Mamlaka hiyo. |
|
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), Charles Kichere akizungumza na baadhi ya wafanyabiashara wakati wa uzinduzi wa zoezi la utoaji vitambulisho na Namba ya Utambulisho ya Mlipakodi (TIN) Dar es Salaam Machi 27, 2018. Kulia (kwake) ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, Kamshna wa Kodi za Ndani, elijah Mwandumbya na Naibu Kamishana wa Kodi za ndani, Abdul Zuberi. |
|
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akimkabidhi mmoja wa wafanyabiashara kitambulisho na Namba ya Utambulisho ya Mlipakodi (TIN) wakati wa uzinduzi wa zoezi la utoaji vitambulisho Dar es Salaam Machi 27, 2018. Pamoja naye ni Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), Charles Kichere (mwenye miwani) na viongozi waandamizi wa Mamlaka hiyo. |
|
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), Charles Kichere akimkabidhi Mwenyekiti wa Wafanyabiashara (Machinga) Steven Lusinde kitambulisho na Namba ya Utambulisho ya Mlipakodi (TIN) wakati wa uzinduzi wa zoezi la utoaji vitambulisho Dar es Salaam Machi 27, 2018. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema na viongozi waandamizi wa Mamlaka hiyo. (Imeandaliwa na ROBERT OKANDA BLOGS)
|
|
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema na baadhi ya wafanyabiashara wakati uzinduzi wa zoezi la utoaji vitambulisho na Namba ya Utambulisho ya Mlipakodi (TIN) kwa wafanyabiashara (Machinga) Dar es Salaam Machi 27, 2018. Kushoto (kwake) ni Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), Charles Kichere na viongozi waandamizi wa Mamlaka hiyo. |
|
Sehemu ya wafanyabiashara (Machinga) wakishiriki katika uzinduzi huo. |
|
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), Charles Kichere (kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema wakipata maelezo kutoka kwa Afisa Kodi Msaidizi, Mordekai Kibona jinsi ya kuandaa kitambulisho cha Mfanyabiashara wakati wa uzinduzi wa zoezi la utoaji vitambulisho.
|
|
Mwenyekiti wa Wafanyabiashara (Machinga) Steven Lusinde akiongea kushukuru TRA na Serikali kwa ujumla kwa kuwatambu na kuahidi kutoa ushirikiano kwa serikali kwani imedhihirisha inawajali na kuthamini mchango wao kwa maendeleo ya nchi. |
|
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), Charles Kichere na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi waandamizi wa Mamlaka hiyo, viongozi wa Machinga, Manispaa ya Ilala na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA). |
|
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), Charles Kichere na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi waandamizi wa Mamlaka hiyo, viongozi wa Machinga na Manispaa ya Ilala. |
Comments
Post a Comment