- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
WAFADHILI WARIDHISHWA NA MRADI NA MAENDELEO YA MRADI WA MAJARIBIO WA KUTUMIA TEKNOLOJIA KWA WATOTO WALIO NA FURSA NDOGO
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Katibui Tawala wa Mkoa wa
Tanga,Mhandisi Zena Saidi kulia akiwaonyesha mmoja ya sehemu
zinazotunzwa tablets ambazo zinatumiwa kufundishia wanafunzi akiwa na
wafadhili wa mradi huo.
Katibui Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi kushoto akiwa na wafadhili wa mradi huo wakiangalia namna wanafunzi wanavyojifunza kutumia teknolojia ya Tablets
Katibui Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi kulia akiteta jambo na wafadhili wa mradi huo |
Wadau
wa mradi wa miaka mitano wenye lengo la kutumia teknolojia ya kisasa kuwawezesha watoto waliona fursa
ndogo ya kupata elimu katika umri wa miaka tisa hadi kumi na mmoja, kujifunza wenyewe
stadi za msingi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) wameeleza kuridhishwa kwao
na maendeleo ya majaribio hayo.
Wadau ambao walikuwa na ziara ya siku moja kutembelea
vijiji mbalimbali vya nradi huo katika wilaya za Muheza na Pangani wadau aho
ambao walikuwa pamoja na Mwakilishi wa Mpango wa Chakula Duniani (WFP) nchini
Tanzania, Michael Dunford, Mkurugenzi wa Ofisi ya Shirika la Umoja wa Mataifa
la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) ya Kanda ya Afrika Mashariki, Anne
Ndong-Jatta wakiambatana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Mhandisi Zena Said.
Wakitoa maoni wakati wakipewa maelezo walisema ni wazi mradi umeanza kuonyesha uwezo wa teknolojia kuamsha ari ya
kujifunza na kusoma.
Taarufa za awali za mradi na ushuhuda tuliouona
inaonyesha kuwa mpango huu wa kiteknolojia una uwezo wa kuwasha mwamko wa elimu
miongoni mwa watoto na wazazi na unapaswa kutiliwa maanani,” alieleza Mhandisi Said wakat wa
ziara hiyo.
Pia Mhandisi Said alisema kuwa ni wazi pia kuwa
kuwatambulisha wananchi katika teknolojia ya kisasa wakiwa na umtri mdogo
kunawahakikishia watoto hao kuwa
hawawezi kunyanyaswa hapo baadaye wakiwa wakubwa.
Naye Ndong-Jatta alisema kuwa mradi unaonyesha haja ya
kuangalia uwezekano wa kupunguza tatizo la kutojua kusoma na kuandika kwa
wazazi kama njia mojawapo ya kuamsha mwamko wa elimu miongoni mwao na
kuwawezesha kuwasukuma watoto kwenda shule.
Zaidi ya watoto 2,500 kutoka
katika vituo 142 vilvyopo katika wilaya za Handeni,
Korogwe, Lushoto, Mkinga, Muheza na Pangani walipewa tablet mpya aina ya Google
Pixel C, zilizotolewa
kwa hisani ya Google. Tableti hizo zimewekewa mifumo ya elimu kutoka kwa washindi
watano wa mwisho wa Global Learning XPRIZE. Washindi hawa walichaguliwa kutoka katika
timu 198 napaneli ya majaji 11 wa kujitegemea na walio wataalamu na kutangazwa mwezi
September, 2017 wakati wa wiki ya BarazaKuu la Umoja wa Mataifa
Mradi huo wa miaka mitano uliotokana
na mashindano duniani yenye thamani ya Dola za Mareka ni milioni 15. Mradihuu
wa dunia unatoa changamoto kwa timu za wa bunifu kubuni na kuandaa zana za
kusaidia kuondoa ujinga duniani na kuwasaidia watoto ambao hawajapata fursa ya
kwenda shule kujifunza wakiwa nyumbani (Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)
Comments
Post a Comment