Featured Post

UNIDO TAYARI KUSAIDIA TANZANIA YA VIWANDA


Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Viwanda (UNIDO) limesema litasaidia Watanzania kutimiza ndoto za kuwa taifa lenye uchumi wa kati linalotegemea viwanda kwa kuunga mkono utendaji wa pamoja wa sekta ya umma na binafsi.

Kauli hiyo imetolewa katika hafla ya chakula cha mchana iliyoandaliwa na Sekta Binafsi kwa Mkurugenzi Mkuu wa UNIDO Li Yong ambaye alikuwa katika ziara ya kwanza nchini Tanzania na pia ya kwanza nje ya makao makuu ya Shirika hilo baada ya kuchaguliwa kwake kwa mara ya pili mwaka jana.
Alisema katika hotuba yake kwamba moja ya majukumu makubwa ya shirika hilo ni kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) hasa lengo namba tisa la maendeleo na teknolojia kwa ajili ya ustawi wa nchi hizo.
Aidha alisema ili kufanikisha hilo kumesisitizwa ushirikiano ambao ni lengo namba 17 la SDGs.
Alisema sekta binafsi ikishirikiana vyema na serikali ndiyo inayoendesha uchumi hasa katika kutoa fursa za kazi kwani asilimia 80 ya kazi kila mwaka hutolewa na sekta binafsi.
Alisema katika hotuba yake hiyo kwamba amefurahishwa na malengo ya Tanzania na nia ya Shirika hilo kuona kwamba malengo hayo kuelekea uchumi wa kati wa viwanda yanatekelezwa kwa kuangalia vionjo muhimu.
Aidha alisema kwamba wataendelea kushirikiana na sekta binafsi kupitia TSPF kuhakikisha kwamba wananchi wanashirikishwa katika malengo ya maendeleo ili kuwa na malengo endelevu na yanayozingatia mazingira.
Naye Mwenyekiti wa Sekta Binafsi nchini- TPSF Dr. Reginald Mengi akizungumza katika hafla hiyo aliitaka UNIDO kusaidia kutengeneza utajiri nchini Tanzania.
Dr. Mengi alisema kwamba ziara ya kiongozi huyo imekuja wakati muafaka, wakati ambapo Tanzania inaelekeza macho yake katika uchumi wa kati na hivyo kuwa na nafasi ya kusaidia ndoto hiyo kufanikiwa.
Alisema wakati nchi nyingi zimekuwa zikipiga maendeleo, zimekuwa na msingi dhaifu wa uchumi wa viwanda kutokana na kusafirisha zaidi bidhaa ambazo hazijasindikwa au zinazotokana na uziduaji.
Alisema hali hiyo pamoja na kuipa utajiri nchi imekuwa haitawanyi utajiri uliopo.
Alisema kutokana na hali hiyo, UNIDO ina kazi kubwa ya kusaidia Tanzania kufikia lengo lake la viwanda hata kusaidia kuanzishwa kwa maeneo ya viwanda (Industrial Park).
Aidha aliishukuru UNIDO kwa kuwezesha sekta binafsi na serikali kukaa pamoja kupitia Baraza la Taifa la Biashara ambako kunakuwa na mazungumzo yenye tija kuhusiana na maendeleo ya biashara na uchumi nchini Tanzania.
Alifafanua kwamba UNIDO ina nafasi kubwa ya kuisaidia Tanzania hasa katika mipango mikakati yake kwa kuunganisha sekta binafsi na umma ili kuiharakisha Tanzania kuelekea uchumi wa kati wenye kutegemea viwanda.
Wakati huo huo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda pamoja na Kimataifa Dr Augustine Mahiga, ambaye wizara yake ndiye ilimwalika Mkurugenzi mkuu huyo, pamoja na kumshukuru kwa kuitikia wito huo aliitakabkusaidia kuchagiza maendeleo ya viwanda.
Alisema kwamba viwanda vya Tanzania bado vichanga na vinahitaji kusaidiwa na kupewa nguvu ya kuendelea mbele kwani pamoja na uchanga wake mchango wake katika kuelekea uchumi wa kati ni mkubwa.
Awali kabla ya hafla ya chakula cha mchana UNIDO ilitiliana saini na serikali ya Tanzania waraka wa kusaidia kuitoa Tanzania katika mipango ya kitaifa kwenda kwenye mipango ya nchi na washirika ili kufikia uchumi wa kati.
Makubaliano hayo yalisainiwa jijini Dar es Salaam kati ya Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa UNIDO, Li Yong huku yakishuhudiwa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan.
Mwenyekiti wa Sekta Binafsi nchini- TPSF Dr Reginald Mengi (wa tatu kulia) akifurahi jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuendeleza Viwanda – UNIDO Bw. Li Yong (kushoto), Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage (wa pili kushoto) pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Kikanda na Kimataifa Dr Augustine Mahiga (kulia) katika chumba maalum mara baada ya kuwasili kwenye hafla ya chakula cha mchana iliyoandaliwa na sekta binafsi kwa Mkurugenzi Mkuu huyo wa UNIDO iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye akitoa utambulisho wakati wa hafla ya chakula cha mchana iliyoandaliwa na Sekta Binafsi kwa Mkurugenzi Mkuu wa UNIDO Li Yong (hayupo pichani) ambaye alikuwa katika ziara ya kwanza nchini Tanzania iliyofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Sekta Binafsi nchini- TPSF Dr Reginald Mengi akisalimia wadau wa sekta binafsi na wageni waalikwa wakati wa hafla ya chakula cha mchana iliyoandaliwa na Sekta Binafsi kwa Mkurugenzi Mkuu wa UNIDO Li Yong (wa pili kulia) ambaye alikuwa katika ziara ya kwanza nchini Tanzania iliyofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Wengine ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage (kulia), Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuendeleza Viwanda nchini (UNIDO), Stephen Kargbo (wa pili kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) Leodegar Tenga (kushoto) wakiwa meza kuu.
Mwenyekiti wa Sekta Binafsi nchini- TPSF Dr Reginald Mengi akitoa neno la ukaribisho kwa Mkurugenzi Mkuu wa UNIDO Li Yong (hayupo pichani) na wadau walioshiriki hafla ya chakula cha mchana iliyoandaliwa na Sekta Binafsi kwa Mkurugenzi Mkuu huyo wa UNIDO ambaye alikuwa katika ziara ya kwanza nchini Tanzania iliyofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akizungumza ambapo alisema Tanzania inategemea kunufaika na ujio wa mgeni huyo, katika uendelezaji wa viwanda nchini wakati wa hafla hiyo ya chakula cha mchana iliyoandaliwa na Sekta Binafsi kwa Mkurugenzi Mkuu wa UNIDO Li Yong (hayupo pichani) ambaye alikuwa katika ziara ya kwanza nchini Tanzania iliyofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Kikanda na Kimataifa Dr Augustine Mahiga akizungumza katika hafla hiyo ambapo alisema ujio huo unatokana na mwaliko wa wizara yake uliofanywa kimkakati wakati huu ambapo serikali imedhamiria kuigeuza Tanzania kuwa ya viwanda iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuendeleza Viwanda – UNIDO Bw. Li Yong akitoa salamu za UNIDO wakati wa hafla ya chakula cha mchana iliyoandaliwa na Sekta Binafsi kwa Mkurugenzi Mkuu huyo ambaye alikuwa katika ziara ya kwanza nchini Tanzania iliyofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Sekta Binafsi nchini- TPSF Dr Reginald Mengi (kulia) akiteta jambo na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuendeleza Viwanda nchini (UNIDO), Stephen Kargbo wakati wa hafla ya chakula cha mchana iliyoandaliwa na Sekta Binafsi kwa Mkurugenzi Mkuu wa UNIDO Li Yong (hayupo pichani) ambaye alikuwa katika ziara ya kwanza nchini Tanzania iliyofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Viongozi wa meza kuu wakifanya ‘Cheers’ ishara ya kutakiana afya njema na ushirikiano mwema katika maendeleo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuendeleza Viwanda – UNIDO Bw. Li Yong wakati wa hafla ya chakula cha mchana iliyoandaliwa na Sekta Binafsi kwa Mkurugenzi Mkuu huyo ambaye alikuwa katika ziara ya kwanza nchini Tanzania iliyofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Pichani juu na chini ni sehemu ya wadau wa sekta binafsi na serikali walioshiriki kwenye hafla ya chakula cha mchana iliyoandaliwa na Sekta Binafsi kwa Mkurugenzi Mkuu wa UNIDO Li Yong (hayupo pichani) ambaye alikuwa katika ziara ya kwanza nchini Tanzania iliyofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuendeleza Viwanda – UNIDO Bw. Li Yong katika picha ya pamoja na wadau wa sekta binafsi na viongozi wa serikali mara baada ya hafla ya chakula cha mchana iliyoandaliwa na Sekta Binafsi kwa Mkurugenzi Mkuu huyo ambaye alikuwa katika ziara ya kwanza nchini Tanzania iliyofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Sekta Binafsi nchini- TPSF Dr Reginald Mengi na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuendeleza Viwanda – UNIDO Bw. Li Yong wakiagana kwa furaha mara baada ya zoezi la picha ya pamoja wakati wa hafla ya chakula cha mchana iliyoandaliwa na Sekta Binafsi kwa Mkurugenzi Mkuu huyo ambaye alikuwa katika ziara ya kwanza nchini Tanzania iliyofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Comments