Featured Post

TANGA UWASA YADAI BILIONI 3 WATEJA WANAOTUMIA HUDUMA YA MAJI TANGA



Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafiri wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Fares Aram akizungumza kulia ni Meneja wa Fedha na Utawala wa Mamlaka hiyo Agnes Lukindo.
  Meneja Huduma kwa Wateja wa Mamlaka hiyo,Mohamed Pima akijibu maswali ya waandishi wa habari wakati wa mkutano wake na vyombo vya habari kuelekea maadhimisho ya wiki ya maji ambayo hudhimishwa mwezi machi kila mwaka hapa nchini kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafiri wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Fares Aram
   Meneja Huduma kwa Wateja wa Mamlaka hiyo,Mohamed Pima akijibu maswali ya waandishi wa habari wakati wa mkutano wake na vyombo vya habari kuelekea maadhimisho ya wiki ya maji ambayo hudhimishwa mwezi machi kila mwaka hapa nchini kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafiri wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Fares Aram
 Mwandishi wa ITV na Radio One Mkoani Tanga William Mngazija kulia akiwa kwenye mkutano huo akifuatia jambo
 Waandishi wa Habari mkoani Tanga wakifuatilia mkutano huo leo kushoto ni Mbonea Hermani wa Startv ,Mbaruku Yusuph wa Gazeti la Tanzania Daima na Blandina Lukindo wa TK FM wakifuatilia matukio mbalimbali
  Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoani Tanga (Tanga Press Club) Lulu George kushoto akiwa kwenye mkutano huo leo
 Mwandishi wa Gazeti la The Guardian mkoani Tanga Amina Kingazi akiuliza swali kwenye mkutano huo kushoto ni Mwandishi wa Gazeti la Citizen Mkoani Tanga Paskal Mbunga
 Mwandishi wa Gazeti la Citizen Mkoani Tanga,George Sembony kushoto akichukua dondoa kwenye mkutano huo kulia ni Mashaka Kibaya wa Gazeti la Jambo Leo
 Waandishi wa Habari mkoani Tanga wakifuatilia mkutano huo leo kushoto ni Mbonea Hermani wa Startv ,Mbaruku Yusuph wa Gazeti la Tanzania Daima na Blandina Lukindo wa TK FM wakifuatilia matukio mbalimbali
 Mwandishi wa Gazeti la Mtanzania Mkoani Tanga,Amina Omari akisikiliza kwa umakini mkutano huo
 Mwandishi wa Habari wa TBC Joachim Kapembe akiuliza swali kwenye mkutano huo
 Mwandishi wa gazeti la Majira Mkoani Tanga,Mashaka Mhando akiuliza swali katika mkutano huo
 Mwandishi wa Gazeti la Citizen Mkoani Tanga,Paskal Mbunga katika akiwa na Amina Kingazi wa Guardian wakiwa kwenye mkutano huo wa pili kulia ni Mwandishi wa ITV na Radio One Mkoani Tanga William Mngazija
 Sehemu ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakifuatilia mkutano huo
 Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoani Tanga (Tanga Press Club) Lulu George akifuatilia matukio mbalimbali kwenye mkutano huo leo
Mwandishi wa TBC Mkoani Tanga Bertha Mwambela kulia akifuatilia matukio mbalimbali kwenye mkutano huo leo uliofanyika kwenye ukumbi wa YDCP Jijini Tanga kushoto aliyenyoosha mkono ni Mbaruku Yusuph Mwandishi wa Gazeti la Tanzania Daima


MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga(TANGA UWASA) inawadai wateja wao bilioni 3 zinazotokana na malimbikizo ya madeni yao katika utumiaji wa huduma ya maji safi na majitaka jambo ambalo linaweza kuathiri utendaji wake.

Hayo yalisemwa jana na Meneja Huduma kwa Wateja wa Mamlaka hiyo,Mohamed Pima wakati wa mkutano wake na vyombo vya habari kuelekea maadhimisho ya wiki ya maji ambayo hudhimishwa mwezi machi kila mwaka hapa nchini.

Alisema kati ya fedha hizo kiasi cha Bilioni 1.5 wanadaiwa wateja wa majumbani huku taasisi za serikali nazo zikidaiwa bilioni 1.5 hivyo kuwataka kuzilipa fedha hizo kwa wakati ili kuwasaidia mamlaka hiyo kupanga mambo yake ya kimaendeleo.

“Labda niwaambie kuwa pamoja na kutoa huduma bora kwa wananchi lakini hivi sasa bado kuna changamoto kubwa ya ulipaji wa madeni ya wateja wetu hali iliyosababisha deni hilo kuongezeka na hivi sasa kufikia bilioni 3 “Alisema.

“Hali hii inaweza kusababisha usumbufu mkubwa kwetu kwani hatuwezi kuweka mipango ya kimaendeleo wakati kiasi kikubwa cha fedha kipo mikononi mwa wateja wetu hivyo tunawaomba walipe madeni yao kwa wakati“Alisema.

Awali akizungumza katika mkutano huo,Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Jijini (Tanga Uwasa) Mhandisi Farles Aram alisema miongoni mwa mikakati waliojiweka ili kuweza kufikia lengo la ukusanyaji wa madeni hayo ni kutoa msamaha wa gharama za tozo ya urejeshaji wa huduma ya maji kwa wateja waliokatiwa maji majumbani na taasisi.

Alisema kuwa katika kuelekea kuadhimisha wiki ya maji na kufikia malengo ya ukusanyaji wa madeni yalioko nje kwa wananchi na taasisi mbalimbali Mamlaka hiyo imeamua kusamehe tozo hizo ambazo zinatokana na mteja kukatiwa maji pindi anaposhindwa au kuchelewa kulipia.

Alisema wananchi wengi wanashindwa kuendelea na huduma hiyo kutokana na kushindwa kulipia gharama za urudishaji maji hivyo kupelekea deni lao kubakia mikononi na kuingizia hasara Mamlaka.

“Tumegundua mbali ya uwepo wa deni kubwa kwa wateja wetu  lakini wameshindwa kulilipa kutokana na kukosa gharaza za urejeshaji hivyo tumewasamehe na tupo tayari kukusanya madeni hayo kwa makubaliano”Alisema Mhandisi Aram.

Hata hivyo alisema msamaha huo utadumu ndani ya mwezi mmoja tangu kuanza kwa maadhimisho ya wiki ya maji ambayo imeanza leo Machi 16

Comments