Featured Post

SERIKALI YA SWEDEN YATOA BILIONI 66 KUKABARATI KITUO CHA KUZALISHIA UMEME CHA HALE HYDRO SYSTEMS WILAYANI KOROGWE

 Mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza na Balozi wa Sweden nchini Tanzania Katarina Rangnitt kulia wakati alipomtembelea ofisini kwake kufanya mazungumzo naye pia  alitembelea Kituo cha kufufua umeme kwa njia ya Maji kilichopo Hale wilayani Korogwe.

 Balozi wa Sweden nchini Tanzania Katarina Rangnitt akitembelea maeneo mbalimbali kwenye kituo hicho
 Balozi wa Sweden nchini Tanzania Katarina Rangnitt wa pili kutoka kulia akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella kushoto wakiangalia kitu wakati walipotembelea kituo hicho
  Balozi wa Sweden nchini Tanzania Katarina Rangnitt wa pili katikati akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella kushoto wakiangalia mitambo iliyopo kwenye kituo cha Kuzalisha Umeme Hale wilayani Korogwe Mkoani Tanga  wakati walipotembelea kituo hicho kulia ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Korogwe,Rehema Bwasi
 Balozi wa Sweden nchini Tanzania Katarina Rangnitt wa pili katikati akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella kushoto wakitembelea mitambo iliyopo kwenye kituo cha Kuzalisha Umeme Hale wilayani Korogwe Mkoani Tanga  wakati walipotembelea kituo hicho
 Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella katika akiteta jambo na Meneja wa Pangani Hydro Systems Mhandisi Stephen Mahenda kulia ni  Balozi wa Sweden nchini Tanzania Katarina Rangnitt kulia
Meneja Mwandamizi wa Uzalishaji Umeme kutoka Tanesco Makao Makuu Bakaya Mtamakaya akizungumza wakati ziara hiyo ya Balozi wa Sweden nchini Tanzania Katarina Rangnitt kushoto kulia ni Meneja wa Uzalishaji wa Kituo cha Pangani Hydro Systems
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella akizungumza kwenye kikao cha pamoja mara baada ya Balozi huyo wa Sweden kutembelea kituo hicho cha Uzalishaji wa Umeme kulia Balozi wa Sweden nchini Tanzania Katarina Rangnitt

Meneja Uzalishaji wa Pangani Hydro Systems Mhandisi Stephen Mahenda kushoto akiteta jambo na  na Balozi wa Sweden nchini Katarina Rangnitt

Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella katika akiteta jambo na Balozi wa Sweden nchini Katarina Rangnitt kushoto
Balozi wa Sweden nchini Katarina Rangnitt akitembelea maeneo mbalimbali kwenye kituo hicho.
SERIKALI ya Sweden imetoa kiasi cha fedha Bilioni 66 za kitanzania sawa na  dola za Marekani milioni 30 ambazo zitatumika katika kukarabati mitambo katika Kituo cha Kuzalishia Umeme cha Hale Hydro System wilayani Korogwe mkoani Tanga.

Hayo yamebainishwa na Balozi wa Sweden nchini Tanzania Katarina Rangnitt wakati alipotembelea mgodi huo ambapo upo Hale wilayani Korogwe Mkoani Tanga.

Amesema kuwa Tanzania na Sweden zina historia za muda mrefu katika uhusiano wa kidplomasia na nyanja mbalimbali za uchumi na kijamii.

Amesema kuwa nishati ni jambo muhimu kwa maendeleo ya viwanda hivyo kwa kuona umuhimu wa jambo hilo kwa nia moja serikali ya Sweden imetoa kiasi hicho cha fedha katika kukarabati mgodi huo.

" Nishati ni jambo muhimu katika maendeleo ya viwanda na Tanzania tayari imeweka mikakati mizuri katika maendeleo ya viwanda hivyo,serikali ya Sweden imetoa kiasi hicho cha fedha kwa kukarabati mgodi huo "alisema.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigella amemshukuru balozi huyo kwa serikali ya Sweden kufadhili mradi huo,pia amemkaribisha balozi huyo kuwekeza katika sekta mbalimbali za kijamii na uchumi.

" Nawashukuru serikali ya Sweden kwa kufadhili mradi huo na mheshimwa Rais ameweka mazingira mazuri ya uwekezaji mkoani Tanga haswa katika sekta ya viwanda hivyo karibuni Tanga mje kuwekeza" alisema.

Kwa upande wake Meneja wa Mtambo wa Uzalishaji Umeme wa Hale Mhandisi Steven Mahemba amesema kuwa mtambo huo umepunguza uzalishaji kutokana na changamoto mbalimbali zikiwemo uchakavu wa mitambo.

" Kituo hiki kimejengwa kuanzia mwaka 1962 na kumalizika mwaka 1964 na kina muda wa takribani miaka 52 hivyo pia kutokana na uchakavu wa miundombinu take imepunguza uzalishaji kutoka megawati 21 mpaka 4 hadi 8" alisema.

Ukarabati huo unatarajiwa kukamilika kwa muda wa miaka mitatu.(Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

Comments