Featured Post

SBL YATANGAZA MPANGO KABAMBE WA KUWASAIDIA WAKULIMA

Mkurugenzi wa Mahusiano wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) John Wanyancha, akiwasilisha mada ya utendaji na changamoto za kampuni hiyo kwa wajumbe wa  Kamati ya kudumu ya Bajeti, walipotembelea kiwanda cha Mwanza jana.


Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti Hawa Ghasia(katikati) akiongozwa na mwenyeji wake  Mwanzilishi wa kiwanda cha bia Serengeti tawi la Mwanza Christopher Gachuma(kushoto), walipotembelea kujionea utendaji na changamoto,jana, kulia ni mjumbe wa kamati hiyo Albert Obama.



Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji Prof Elisante Ole Gabriel(katikati) akifurahia jambo na Mwanzilishi wa kiwanda cha bia Serengeti tawi la Mwanza Christopher Gachuma(kushoto) na Mjumbe wa Kamati ya kudumu ya Bajeti Albert Obama, wakati wa ziara ya kamati hiyo katika kiwanda cha bia cha Setrengeti  jijini Mwanza jana kujionea utendaji mapema wikiendi hii.



Mwanza Machi 17, 2018 – Mpango maridhawa wa kuwasaidia wakulima unaoendeshwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti(SBL), umeiwezesha kampuni hiyo kuongeza wigo wa upatikanaji wa malighafi kutoka vyanzo vya ndani ya nchi kufikia tani 15,000, sawa na asilimia 80 ya mahitaji ya kampuni hiyo kwa mwaka.
Mpango huo unaojulikana kama Kilimo-biashara, unatekelezwa katika mikoa mbali mbali  hapa nchini ambapo wakulima wanaolima mazao kama mahindi, mtama na ulezi hupewa misaada inayowawezesha kuongeza uzalishaji.
Akiongea wakati wa ziara ya Kamati ya Bunge ya Bajeti iliyotembelea kiwanda cha SBL kilichopo jijini Mwanza mwishoni mwa wiki, Mkurugenzi wa Mahusiano kwa Umma wa kampuni hiyo John Wanyancha alisema, SBL inawasaidia wakulima 300 waliopo sehemu mbali mbambali nchini huku lengo likiwa ni  kuongeza idadi na kufikia 450 katika kipindi cha miaka 2 ijayo.
Mpango wa kuwasidia wakulima unahusisha kuwapatia bure mbegu bora, kuwaunganisha na taasisi za fedha ili kupata mitaji kwa ajili ya kuongeza uzalishaji wao pamoja na kuwapatia huduma za pembejeo. SBL hununua mazao yao na kuwawezesha kulipa mikopo pamoja na kuboresha masha yao kupitiua kipato wanachokipata.
Ili mpango huo uweze kuendelea kuwa endelevu na kuiwezesha SBL kuwafikia wakulima wengi zaidi, kampuni hiyo imeiomba Serikali kuendelea kuacha kiwango cha ushuru wa bidhaa kwa bia zinazozalishwa na malighafi za ndani kubakia asilimia 40 ambacho ni chini ukilinganisha na zile zisizotumia malighafi za ndani.
“Zaidi ya nusu ya vinywaji vinavyozalishwa na SBL zikiwamo bia kama Pilsner Lager, Kibo Gold, Kick Lager, Pilsner King and Senator Lager, zinazalishwa kwa asilia 100 na malighafi zinazotoka hapa nchini,” alisema Wanyancha
SBL pia imeishauri Serikali kutoongeza ushuru kwenye bia na pombe kali katika bajeti ijayo. Wanyancha alisema, kutoongezwa kwa ushuru kutasaidia kutafanya bei za bidhaa hizo zibaki kama zilivyo kwa sasa.
“Kwa kutobadilika kwa bei za vinywaji, Serikali itakuwa na uhakika wa mapato Zaidi kutokana na watumiaji kumudu kununua Zaidi,” alisema
Mkurugenzi huyo alitahadharisha kuwa, ongezeko la ushuru litasababisha ongezeko la bei huku likiathiri mauzo, jambo ambalo litapelekea kushuka kwa mapato ya serikali na kuongezeka kwa biashara ya pombe haramu.  

Ziara hiyo pia ilihudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Profesa Elisante Ole Gabriel ambaye alisema Serikali itaendelea na dhamira yake ya kuiwezesha sekta binafsi kukuwa na kustawi

Comments