Na Richard MwangulubeOfisi ya Waziri Mkuu imeupongeza Uongozi wa Serikali wa Mkoa wa Arusha
kwa kuwa Wabunifu katika kutekeleza kwa Vitendo maelekezo ya Serikali ya
kuyawezesha makundi maalum.
Pongezi hizo zimetolewa jana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mjini Arusha Jenista Mhagama
(MB) alipokabidhi mikopo kwa Wanawake 600.
Mikopo hiyo imetolewa na Serikali ya Mkoa wa Arusha kupitia mradi maalum
uliobuniwa na kuanzishwa na Serikali ya Mkoa wa Arusha kwa kushirikiana
na Wadau mbalimbali wa maendeleo katika Mkoa huo kwa ajili ya
kuyawezesha makundi maalum wakiwemo Wajasirimali wadogo wadogo wa ngazi
ya chini.
Waziri Mhagama amesema Viongozi wa Mkoa wa Arusha chini ya Mkuu wa Mkoa
huo Mrisho Meshaki Gambo na Katibu Tawala wa Mkoa (RAS) pamoja na Mkuu
wa Wilaya ya Arusha Gabriel Dagarro wanastahili pongezi kutokana na
kuwa wabunifu kwa ajili ya kuwawezesha wajasiriamali wadogo wadogo.
Waziri Mhagama amesisitiza kwamba Viongozi hawa wamestahili pongezi
hizo kutokana na kutafsiri kwa Vitendo maelekezo ya Rais Dkt John POMBE
Joseph Magufuli ya hapa kazi tu.
Amesisitiza kwamba Viongozi hawa pia wameisaidia Serikali inayoongozwa
na Rais Magufuli ya kuleta mageuzi makubwa ya kiuchumi katika jamii kwa
kuwasaidia wananchi wanyonge wa ngazi ya chini kuwawezesha kiuchumi.
Waziri Mhagama amesemaMkoa wa Arusha umekuwa Mkoa wa mfano nchini katika
kutekeleza maelekezo ya Rais Magufuli kwa kushirikisha Wadau
mbalimbali wa maendeleo wakiongozwa na Kamanda wa Mkoa Kijana mchapa
Kazi na Jemedari Mkuu wa Mkoa huo Mrisho Meshack Gambo katika mapambano
haya.
Waziri huyo Ofisi ya Waziri Mkuu amefafanua kuwa Viongozi hawa kwa
kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo wameongoza safari ndefu ya
mabadiliko katika Jamii ya Wananchi wa Mkoa wa Arusha.
Ujenzi wa uchumi na maendeleo ya Mkoa wa Arushana Tanzania unachangiwa
na ushiriki kikamilifu wa Wananchi wote bila kujali Itikadi zao za
Kisiasa ama dini.Amesisitiza Waziri Mhagama.
Umoja uliopo katika Mkoa wa Arusha baina ya Chama cha Mapinduzi,Serikali
na Wananchi umejenga nguvu ya pamoja katika kufikia mafanikio
yanayotarajiwa na Serikali ya awamu ya tano.Amesisitiza Waziri Mhagama.
Waziri huyo amesema kutokana na umoja uliopo hivi sasa katika Mkoa wa
Arusha Watanzania katika kona zote wanshuhudia Makundi
yaliyosahaulika wakiwemo Vijana (boda boda, Walemavu na Wanawake)
Wanawezeshwa mikopo hivi sasa kupitia mradi huu maalum uliobuniwa na
Serikali ya Mkoa,Wilaya, Jiji l Arusha n Washirika mbalimbali wa
Maendeleo katika Mkoa huu.
Hata hivyo Waziri Mhagama amesisitiza kuwa mafanikio yanayoonekana
hivi sasa yanatokana na hali ya Utulivu, amani na hali ya Usalama
uliosimamiwa kikamilifu na Viongozi wa Mkoa.
Amesema siku ya nyuma Vijana na Wanawake walitumika na baadhi ya
Wanasiasa katika maandamano na vurugu hususani katika Jiji hili la
Arusha mambo ambayo hivi sasa hayapo tena.
Wananchi waliishi maisha ya hofu, amani katika Mkoa huu ilitoweka
kulikuwa hakuna utulivu, mali ziliharibiwa na baadhi ya watu walipoteza
maisha mambo ambayo hivi sasa hayapo kutokana na kuwepo na Viongozi
imara na wenye msimamo.
Waziri Mhagama amesisitiza kuwa Wanawake ndiyo nguzo muhimu katika masuala ya maendeleo na ujenzi wa uchumi wa taifa hili.
Amesifu Viongozi wa Mkoa wa Arusha wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa Gambo kwa kuguswa na maisha ya Wananchi wa ngazi ya chini.
Amesisitiza kwamba Serikali ya awamu ya tano itahakikisha Wananchi wote
wananufaika na matunda yanayopatikana bila kujali Itikadi zao za
Kisiasa.
Amesema Serikali ya awamu ya tano imedhamiria kufanya mageuzi na
kutafsiri kwa Vitendo Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2015 kwa
lengo la kupunguza kwa kiasi kikubwa kiwango cha umaskini kwa kukuza
uchumi wa wananchi kupitia mpango wa uwezeshaji wananchi Kiuchumi.
Waziri Mhagama amesisitiza kuwa mikopo inayolewa na mradi huu maalum na
Mkoa wa Arusha imelenga kuleta mabadiliko makubwa katika Jamii.
Amewambia Wanawake hao kutoka Kata zote 25 za Jiji la Arusha Mikopo hii
inayotolewa na Serikali ya Mkoa itumike kufanya mageuzi ya Kiuchumi
katika familia zenu.
Amewataka Wanawake hao kutumia Mikopo hiyo kwa nidhamu,Uaminifu na
uadilifu wa hali ya juu na kutadharisha kuwa mikopo hii isitumike akwa
shughuli za anasa.
Hivyo amewataka Wanawake waliobahatika kupata mikopo hiyo waonyeshe
mabadiliko katika Jamii.Hata hivyo amesisitiza umuhimu wa Wanawake hao
kujenga tabia ya kurejesha mikopo hiyo haraka ili makundi mengi yaweze
kunufaika.
Waziri Mhagama amesisitiza kwamba Wanawake ni Jeshi kubwa katika Jamii
linaloongoza mapambano ya maendeleo na Kiuchumi katika nchi. Hata hivyo changamoto kubwa inayowakabili wanawake ni uwezo wa
kujitengenezea ajira kwa njia ya biashara ndogondogo.Hivyo mradi huu ni
Mkombozi mkuu kwa Wanawake wa Mkoa wa Arusha. Mikopo hii haina dhamana wala riba hivyo itumike ipasavya katika
kuwakomboa wanawake wa Mkoa wa Arusha .Amesisitiza Waziri Mhagama.
Amesema utafiti unaonyesha kuwa ukosefu wa ajira hapa Tanzania ni
asilimia 12.3 na kundi kubwa linalokabiliwa na kukosa ajira ni Wanawake.
Hata hivyo Waziri Mhagama ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Peramiho
Mkoani Ruvuma amesisitiza kwamba Mikopo hii siyo Zawadi kutoka kwa Mkuu
wa Mkoa huo Mrisho Gambo bali ni moja ya Mkakati wa Serikali ya Mkoa
huo wa kuwakomboa Wanawake,Vijana na Walemavu Kiuchumi.
Serikali ya awamu ya tano inafahamu kuwa kazi iliyopo mbele ya Serikali
bado ni kubwa kutokana na makundi mengi ngazi ya chini bado yanakabiliwa
na changamoto nyingi.
Hata hivyo Serikali imeanzisha mifuko 19 inayosimamiwa na Ofisi ya
Waziri Mkuu kwa ajili ya kutoa mikopo kwa ajili ya kuwawezesha wanawake,
Vijana na makundi maalum wakiwemo walemavu.
Kwa upande wake Naibu Waziri katika Ofisi hiyo Antony Mavunde amesema ushindi wa Chama cha Mapinduzi katika chauzi
mbalimbali unatokana mchango mkubwa unaotolewa na Jeshi kubwa la
Wanawake.
Mavunde amesisitiza kwamba Wanawake wanao mchango mkubwa katika masuala ya maendeleo na ukuaji wa uchumi wa Taifa la Tanzania.
Aidha Naibu Waziri Mavunde amesisitiza kamba lengo la Serikali ya awamu
ya tano ni kuyaweaeaha makundi mbalimbali kiuchumi bila kujali Itikadi
zao za Kisiasa.
Mbunge wa Viti Malum CCM Mkoa wa Arusha Catherine Magige amewataka
Wanawake waliobahatika kupata mikopo hiyo waepuke kutumia fedha hizo
kwa ajili ya kununua Vitenge. Magige amesema akina mama hawana uwezo kiuchumi wa kukopa katika taasisi za fedha ambazo zinatoza riba kubwa na dhama.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Meshack Gambo ameeleza
kwamba Serikali Mkoani humo itahakikisha Arusha inaendelea kuwa tulivu
na Watu wanaisi kwa amani bila vurugu. Serikali ya Mkoa imejipanga kuendelea kuwezesha makundi mbalimbali ili makundi hayo yajikomboe kiuchumi.
Amesisitiza kuwa mikopo hii itakuwa imetengeza ajira nyingi kwa makundi
hayo na watu wengi.hivyo fedha iliyotolewa leo kama mkopo itumike na
wanawake hao kama mbegu kwa lengo la kuwabadilisha maisha yao.
Gambo ameeleza kwamba Mkoa wa Arusha kwa mwaka wa fedha 2017/2018 ulitoa
mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni moja kwa makundi mbalimbali
katika Mkoa huo kwa lengo la kubadilisha maisha na ustawi wa Jamii.
Mkuu huyo wa Mkoa wa Arusha ameeleza kuwa kutokana na Wananchi wengi
hasa wa kada ya chini na wajasiriamali wadogo wadogo kushindwa kupata
mikopo katika taasisi za fedha kutokana taasisi hizo kuw ana masharti
magumu na riba kubwa Mkoa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ulibuni
mradi maalum kwa ajili ya kuwawezesha wajasirimali Kiuchumi.
Amesema awali mradi huo ulikusanya fedha zaidi ya milioni 400.2. Fedha ambazo zilitumika kutoa mikopo kwa Vijana waendesha boda boda
200 ambapo asilimia 75 ya mikopo hiyo imerejeshwa na Vijana hao.
Mkuu huyo wa Mkoa wa Arusha amesisitiza kuwa Serikali Mkoani humo
itaendelea kujenga mazingira rafiki na mazuri kwa ajili ya kuwawezesha
wajasiriamli wadogo kuendesha biashara zao bila bugudha.
Gambo amesisitiza kuwa mikopo hii haingalii mkopaji anatoka chama gani
ama dini gani ama kabila gani bali ni kwa ajili ya Wajasiriamli wote
wadogo.
Mkuu huyo wa Mkoa wa Arusha amesisitiza kuwa Mikopo hii imelenga
kuwakwamua Kiuchumi Wajasiliamali wadogo na kwamba mikopo hii haina
riba wala dhamana.
Gambo amesisitiza kuwa suala la maendeleo na ujenzi wa uchumi wan chi
halina Itikadi za Kisiasa.hivyo amewataka Viongozi mbalimbali wa Vyama
vya Siasa katika Mkoa huo kushirikiana na Serikali katika masuala
mbalimbali ya Maendeleo.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Dagarro amesisitiza
kuwa Wanawake ndio wajenzi wakuu wa uchumi na maendeleo ya Tanzania.
Aidha Mkuu wa Mkoa Gambo aliwachimba mkwara wanasiasa katika Jiji hilo
wanaodhani mradi huu hautafanikiwa na kueleza kuwa wao walie tu.
Amesema alipotoa mkopo kwa vijana waendesha boda boda wanasiasa hao
walisema mradi huo utakwama na hivi sasa mradi huo umeonyesha mafanikio
makubwa vijana hao wamerejesha mikopo kwa asilimia 75 na bado
waliobakia wanaendelea kurejesha alisisitiza Gambo.
Gambo alisema wanasiasa hao hivi sasa wamekwama hawana hoja ya kuongea
mbele ya wananchi na amesisitiza kuwa hakuna maandamano wala vurugu za
kisiasa katika Jiji hilo wala Mkoa wa Arusha kwa vile viongozi
tumejipanga.
Dagarro pia amesema Wanawake ndiyo washiriki wakuu katika masuala ya uzaalishaji katika sekta ya Kilimo na Sekta nyingine.
Hata hivyo Mkuu huyo wa Wilaya amesisitiza kuwa Serikali itaendelea
kuimarisha elimu ya biashara kuanzia ngazi ya mtaa, Kata na tarafa kwa
Wajasiriamali wadogo ili kuwawezesha kuendesha biashara zao kwa tija na
ufanisi zaidi.
Mkuu huyo wa Wilaya ya Arusha amewahakikishia akina mama hao kwamba
wataendesha biashara zao bila kubugudhiwa bali kwa amani na utlivu kwani
Serikali haitaruhusu vurugu za kutimua timua wajasiriamali wadogo
mitaani.
Kwa upande wake Mke wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mwalimu Margreth Muro
Gambo amewataka Wanawake hao kutumia mikopo waliyopata kuwa chachu ya
kuwaleta mageuzi kwa lengo la kuwakwamua kiuchimi.
Mwalimu Margreth Muro Gambo pia amesema mikopo hiyo itumike kujenga amani na utulivu katika familia.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Kinachosimamia masuala ya Utalii
Mkoani Arusha (TATO), Willy Chamburo amesema Mkoa wa Arusha ni Mkoa wa
Utalii ambapo unapokea asilimia 80 ya Watalii wote wanaotembelea
Tanzania.
Amesisitiza kuwa amani na utulivu vikiendelea kuwepo hali ya utalii
itanedelea kukua.hivyo wajasiriamali wadogo hawa ni muhimu sana katika
kukuza sekta ya Utalii Mkoani Arusha.
Kutokana na Kutambusa hilo Mwenyekiti huyo wa TATO alitoa Shilingi
milioni 20 kama mchango kwa ajiili ya kuwapatia Wengine 100 mikopo.
Mbali na Mkopo huo pia Chamburo alitoa Vitanda 10 kwa ajili Kituo cha Afya Murriet kwa ajili ya akina mama wanaojifungua.
Pia alitoa Vitanda 30 kwa ajili ya Kituo hicho kwa ajiri ya akina mama
wanaolazwa katika hospitali hiyo na Kampuni ya Tanzanite ilitoa
shilingi milioni nane(mil 8) kuunga mkono juhudi za Chamburo.
Pia Kampuni nyingine ya Utalii ilitoa Gari aina ya Ambulance kwa ajili ya Kituo hicho cha Afya cha Murriet.
Dkt Phillemon Mollel ambaye ni Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya
MONABAN akizungumza katika hafla hiyo alisema Mkoa wa Arusha umeanza
kutekeleza kwa mafanikio dhana ya Rasi Dkt John Pombe Joseph Magufuli
ya hapa Kazi tu.
Dkt Mollell amesema Arusha kama Mkoa umejikita katika kufanikisha
maelekezo mbalimbali ya RaisDkt Magufuli yakiwemo maelekezo ya Dhana ya
Viwanda.
Dkt Mollel ambaye ni mmoja wa Makampuni yake katika kuanzisha mradi huo
maalum wa kuwawezesha wanawake Kiuchumi katika Mkoa wa Arusha. Amesisitiza kuwa hivi sasa Mkoa huo umejikita na kujipanga kuhakikisha
Wajasirimali wadogo wanawezeshwa Kiuchumi kwa kupatiwa Mikopo kupitia
mradi huo Maalum ulioanzishwa na Mkoa.
Dkt Mollel amesisitiza kwamba lengo la mradi huu kuanzishwa na Mkoa ni
kuwainua Wanawake wa Mkoa huo hususani katika Jiji la Arusha Kiuchumi
na kuwaodoa katika matatizo ya kukopa fedha kutoka taasisi za fedha
ambazo hutoza riba kubwa.
Pia lengo la mradi huu ni kuwasaidia wanawake na familia zao kuboresha
maisha yao ili waondokane na Umaskini unaowakabili.amesisitiza Dkt
Phillemon Mollel.
Mradi huu unatekelezwa na Mkoa kutokana na kuwepo na Sera Safi, AMani na Utulivu katika Jiji la Arusha n mkoa Mzima.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha (RAS) Richard Kwitega
ambaye ndiye msimamizi Mkuu wa mradi huu amesisitiza kuwa nafasi ya
akina mama katika uhai wa Mwandamu ndiyo tegemeo kubwa kuanzia motto
akiwa tumboni hadi makuzi yake yote.
Kwitega amesema Wanawake ndiyo wanaolea familia katika masuala
mbalimbali ya Kijamii.hivyo ndiyo tegemeo kuu katika maisha ya Mwandamu.
Hivyo jamii kamwe haitaacha kuwaenzi Wanawake kutokana na umuhimu wao
katika Jamii .Amesisitiza Richard Kwitega Katibu Tawala wa Mkoa wa
Arusha.
RAS Kwitega amesisitza kuwa Wanawake ndio wanaoingarisha familia na
taifa katika masuala mbalimbali huku akiwataja akina Mama Anna
Abdallah,Anna Makinda na Getrude Mongela kuwa ni miongoni mwa Wanawake
Viongozi walioingarisha Tanzania katika Mataifa ya nje
Wajasiriamali hao kila mmoja alipata mkopo wa shilingi laki
mbili(200,000) ambazo kila mmoja aliingizwa katika akauti yake zilizoopo
benki ya NMB Arusha.
Fedha hizo ni kati ya shilingi milioni 400.2 ambazo ni mtaji katika
mradi huo maalum ulioanzishwa na Serikali ya Mkoa wa Arusha kwa ajili
ya kuwawezesha wajasiriamali wadogo wanaoendesha biashara ndogondogo
katika Jiji la Arusha.
Kwitega amesisitiza kuanzishwa kwa mradi huu maalum na serikali ya Mkoa
huo imelenga kujaribu kutatua kero na matatizo yanayowakabili wananchi
wa kada ya chini wanaoendesha biashara ndogondogo katika Mkoa huo.
RAS Kwitega amesema mradi huu haueneshwi Kisiasa kama ambavyo baadhi ya
wanasiasa katika Wilaya hivyo wanavyodhani bali ni kutekeleza
maelekezo ya JPM.
Katibu Tawala huyo wa Mkoa wa Arusha amesisitiza kuwa Serikali ya Mkoa
huo itatekeleza maelekezo yote ya Rais DKT Magufuli ya kuhakikisha
Wananchi katika kada zote wanaondokana na kero zinazo wakabili bila
ubaguzi wa kiitikadi za kisiasa kwa kutambua kuwa Serikali iliyopo
madarakani ni kwa ajili ya kuwahudumia wananchi wote wa Mkoa huo
Comments
Post a Comment