Featured Post

RC MASENZA AWAPONGEZA RDO KWA KUTATUA TATIZO LA MAJI KWENYE BAADHI YA VIJIJI VYA WILAYA YA MUFINDI NA KILOLO


 Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Nandala alipokuwa ameenda kuzindua mradi wa maji ambao utasaidia kupunguza changamoto ya maji na kuchochea maendeleo kwa wananchi ambao watakuwa wananufaika na mradi huo ulifadhiliwa na shirika lisilo la kiserikali la Rural Development Organization (RDO) Tanzania ambao makao makuu yao yapo Mdabulo Mufindi.


 Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akimtusha ndoo ya maji mmoja ya wananchi walihudhulia uzinduzi wa mradi maji ulifadhiliwa na shirika lisilo la kiserikali la Rural Development Organization (RDO) Tanzania

 Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akiwa na mkurugenzi mtendaji wa shirika lisilo la kiserikali la Rural Development Organization (RDO) Tanzania Fidelis Filipatali wakibadilisha mawazo juu ya mradi huo ambao umegharibukiasi cha shilingi milioni tisini na tano,laki tano na elfu tatu mia moja ( 95,503,100)


 Hapa ndio tank kubwa la mradi wa maji unaofadhiliwa na shirika lisilo la kiserikali la Rural Development Organization (RDO) Tanzania na 
umegharibukiasi cha shilingi milioni tisini na tano,laki tano na elfu tatu mia moja ( 95,503,100)

Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Nandala alipokuwa ameenda kuzindua mradi wa maji ambao utasaidia kupunguza changamoto ya maji na kuchochea maendeleo kwa wananchi ambao watakuwa wananufaika na mradi huo ulifadhiliwa na shirika lisilo la kiserikali la Rural Development Organization (RDO) Tanzania ambao makao makuu yao yapo Mdabulo Mufindi.

 Na Fredy Mgunda, Iringa
 
MKUU wa mkoa wa Iringa Amina Masenza amelipongeza shirika lisilo la kiserikali la Rural Development Organization (RDO) Tanzania kwa kufanikisha kupatikana kwa maji katika baadhi ya vijiji vya wilaya ya Kilolo na Mufindi ambayo itakuwa njia moja wapo ya kuchochea maendeleo kwa wananchi.

Akizungumza wakati wa kuzindua mradi wa maji katika kijiji cha Nandala’ Masenza alisema kuwa amefurahishwa na mfumo ambao unatumiwa na shirika hilo kwa kutoa huduma ya maji kwa kushirikiana na wananchi wa maeneo husika.

“Mradi wowote ule ukiwa na ushirikiano mkubwa na wananchi mara nyingi wananchi wanautunza mradi huo kwa kuudhamini na kuulinda,hivyo nawapongeza RDO kwa kufanya maamuzi sahihi ya kubuni mradi huo pamoja na wananchi” alisema  Masenza

Masenza alisema kuwa mradi huo wa maji utatoa huduma kwa wananchi wengi na taasisi binafsi nyingi hivyo wananchi wanatakiwa kuutunza na kuudhamini ili udumu kwa muda mrefu na kuondoa tatizo la maji ambalo limekuwa kero ya muda mrefu.

Nimesikia kwenye risala yenu kuwa mradi huu utahudumia kata zifuatazo Ifwagi,Mdabulo,Ihanu,Luhunga,Mtitu na Kising’a na vijiji vitakavyopata huduma hiyo ni Igonongo,Ludilo,Kidete,Ikanga,Nandala,Ibwanzi,Isipii,Mkonge,Lulanzi,Luhindo,Barabara mbili na Isele hivyo ukiangala utagundua kuwa mradi huu ni mkubwa na upaswi kupuuzwa kwa maendeleo kwa wananchi wa maeneo ambayo mradi huo umepita.

“Jamani wananchi ambao mmepata bahati ya kupitiwa na mradio huu mkubwa wa maji mnapaswa kuulinda na kuudhamini kwa kuwa ni mmoja ya mradi mkubwa ambao unapunguza adha ya upatikanaji wa maji ambayo hapo awali ilikuwa kero kubwa” alisema Masenza

Kwa upande mkurugenzi mtendaji wa shirika lisilo la kiserikali la Rural Development Organization (RDO) Tanzania Fidelis Filipatali alisema kuwa mradi huo umegharibukiasi cha shilingi milioni tisini na tano,laki tano na elfu tatu mia moja ( 95,503,100) ambao ndani yake kuna pesa zilizochangwa na wananchi kwa ajili ya kusaidia kupata huduma ya maji.

“Sisi kama RDO ambao ndio wafadhili namba moja wa mradio huu wa maji tumechangia kiasi cha shilingi milioni themenini na sita,laki nane ishirini na moja elfu (86,821,000) na wananchi walichanga kiasi cha shilingi milioni nane,laki sita themenini na mbili na mia moja (8,682,100)” alisema Filipatali

Filipatali  alisema kuwa mradi huo wa maji  utazaliza ujazo wa lita 776  kwa vijiji vyote ambazo vinatumia huduma hiyo ya maji na pia wananchi watakao pata huduma hiyo ni 10,874 kwa vijiji vyote vilivyopitiwa na mradi huo na jumla ya taasisi 18 nazo zitanufaika na huduma hiyo.

“Mkuu wa mkoa sasa ukiangalia kwa ujumla ndio utagundua kuwa ni mradi ambao utakuwa unakomba wananchi wengi waliokuwa wanapata tabu juu ya kupata maji hivyo naomba pia nisisitize wananchi kuutunza na kuchangia kwa malipo kidogo kwa ajili ya ukarabati wa mashine na mitambo mingie inayosukuma maji hayo ili isihalibike” alisema Filipatali

Filipatali alisema kuwa mradi huo unakabiliwa na changamoto zifuatazo baadhi ya watumiaji maji kutochangia, viongozi kutotimiza majukumu yao kama kutohudhuria mikutano ya mapato na matumizi,watumiaji maji kutotilia mkazo elimu wanayopewa na wataalamu wa maji,siasa kuingia mfumo mzima wa mradi huu na baadhi ya serikali za vijiji kuchukulia mapato ya miradi ya maji kama sehemu ya mapato ya serikali  kitu ambacho sio kweli mfano kjiji cha Lidilo

“Hizi changamoto zimekuwa kero sana kwenye miradi ambayo imekuwa inatekelezwa kwenye maeneo husika hivyo niwaombe viongozi wa kiasa wawe wa kwanza kutoa elimu juu ya miradi ambayo inafaida na kutatua changamoto za wananchi kwenye maeneo yao” Filipatali

Comments