- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Katibu Mtendaji wa TATO, Siriri Akko akichangia mada katika kikao kazi hicho juu ya maazimio ya kuondoa kero na changamoto wakutanazo watoa huduma za utalii nchini. |
Add caption |
Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro(NCAA) na Chama cha Mawakala wa Utalii(TATO), wamefikia makubaliano ya kuondoa vikwazo baina yao na hivyo kushirikiana katika kukuza utalii hapa nchini.
Makubaliano hayo, yalifikiwa jana katika kikao kazi kilichofanyika Arusha katika hotel ya New Arusha, baina viongozi NCAA,TATO na Kampuni za Utalii ambazo hivi karibuni zilitajwa kuwa huenda zingezuiwa kuingiza watalii katika hifadhi ya Ngorongoro.
Akizungumza katika kikao hicho, Naibu mhifadhi wa NCAA anayeshughulikia Huduma za Shirika Asangye Bangu alisema,NCAA imejipanga kuboresha huduma kwa watalii na kuondoa changamoto zinazowakabili wenye makampuni ya Utalii.
"Kikao chetu kimekwenda vizuri, NCAA tutaendelea kuboresha mifumo ya malipo, kuboresha mawasiliano baina yetu na mawakala wa utalii lakini pia kutatua changamoto kadhaa, ikiwepo barabara ndani ya hifadhi"alisema
Alisema katika kukabiliana na kero ya barabara, NCAA inatarajiwa mwezi wa nane mwaka huu, kuanza ujenzi wa barabara ya kutoka geti la kuingia Ngorongoro hadi geti la kuingia Serengeti yenye urefu wa kilomita 83 kwa kuweka tabaka gumu juu.
"hii ni kero ya muda mrefu ya makampuni ya Utalii lakini sasa Shirika la umoja wa mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni(UNESCO)limetukubalia kuijenga barabara hii na ikikamilika tunaimani barabara itadumu kwa zaidi ya miaka 40"alisema
Awali Katibu Mtendaji wa TATO, Siriri Akko alisema, katika siku za karibuni kuliibuka taarifa za kuwachanganya baadhi ya wanachama wao juu ya kuzuiwa kuingia ngorongoro kupeleka watalii.
Hata hivyo, alisema baada ya kupata maelezo kutoka NCAA wamefikia makubaliano ambayo lengo lake ni kuboresha sekta ya utalii nchini na pia kuondoa changamoto zinazowakabili.
"kikao chetu kimekwenda vizuri na ile hofu ya kampuni kuzuiwa sasa haipo na tunaimani kampuni zote zitafuata sheria na taratibu za kufanya biashara ya utalii hapa nchini"alisema
Akizungumza katika kikao hicho,Mkurugenzi wa kampuni ya Utalii wa Shidolya, Lazaro Mafie alisema ni muhimu kuwepo na mawasiliano ya mara kwa mara baina ya NCAA na makampuni ya utalii ili kutatua kero.
Mafie alisema wao kama wamiliki wa makampuni ya Utalii, wateja wao ni watalii sawa na NCAA ambayo uwepo wao unategemea watalii hivyo ni lazima kuwepo na mawasiliano mazuri baina yao.
"kuna changamoto kadhaa ambazo tunakabiliana nazo lakini tunaimani sasa zitafanyiwa kazi ili kuboresha sekta ya utalii hapa nchini"alisema.
Comments
Post a Comment