- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Mkuu
wa Idara ya Masoko wa Benki ya Exim Tanzania, Stanley Kafu kushoto akimkabidhi
sehemu ya vitanda 40 magodoro 40 na Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa
Tanga, Dkt. Clemence
Marcel ikiwa mpango wao kupitia kampeni
ya benki ya exim ya miaka 20 ya kujali jamii wa pili kulia ni Kaimu Mganga
Mfawidhi wa
Hospitali ya
Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Dkt Mohamed Abdallah kushoto ni Meneja wa Benki ya
Exim Mkoa wa Tanga, Emanuel Mwamkinga.
Kaimu
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Dkt Clemence Marcel akiwa na Mkuu wa Idara ya
Masoko wa Benki ya Exim Stanley Kafu wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada
ya kukabidhi vitanda na magodoro 40 kwa
hospitali ya rufaa ya mkoa wa Tanga Bombo.
Muuguzi
mfawidhi wa Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Tanga Bombo Beatrice Rimoy
akizungumza kuishukuru benki ya Exim kwa kuwapatia msaada huo wa vitanda na
magodoro 40
Sehemu ya vitanda na magodoro vilivyotolewa
Sehemu ya watumishi wa Hospital ya Rufaa ya
Mkoa wa Tanga Bombo wakifuatilia matukio hayo
BENKI ya Exim
Tanzania imetoa msaada wa vitanda 500 na magodoro kwa hospitali za rufaa kwenye
mikoa 13 hapa nchini ikiwa ni sehemu ya kampeni yake yenye lengo la
kusheherekea miaka 20 ya kuitumikia jamii.
Hayo yalibainishwa
leo na Mkuu wa Idara ya Masoko wa Benki hiyo, Stanley Kafu wakati akikabidhi
vitanda na magodoro 40 kwa ajili ya hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo
inayolengo la kusaidia upungufu wa vitanda
katika hospitali nchini.
Alisema ili
kukabiliana na hali hiyo ndio maana waliamua kutoa msaada ili kuweza kusaidia
tatizo la ukosefu wa dawa, vifaa na vitanda hasa katika hospitali za
rufaa katika
kukabiliana na uhaba unaosumbua Taifa.
“Benki ya Exim
Tanzania iliadhimisha miaka 20 ya huduma mwezi wa Agosti mwaka jana,kwa
kuzindua kampeni ya mwaka mzima uuitwao ‘Miaka 20 ya kujali jamii”ambao benki
hiyo itawekeza katika sekta ya Afya Tanzania…Sisi kama Benki ya Kitanzania
iliyoanzishwa mwaka wa 1997 hivyo benki hiyo inafafanua mafanikio yake jinsi
inavyoleta mabadiliko kwa wateja na jamii kwa ujumla
“Alisema.
“Hospitali ya
rufaa mkoa wa Tanga ni hospitali ya saba kupokea mchango huu, baada ya
hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mbeya mwezi uliopita, Hospitali ya Mount Meru
mkoani Arusha mwezi Desemba, Hospitali ya rufaa Dodoma mwezi Novemba, Hospitali
ya rufaa Ligula mkoani Mtwara mwezi Octoba,Hospitali ya Mnazi mmoja Unguja
Visiwani Zanzibar mwezi Septemba na hospitali ya rufaa ya Temeke mkoani Dar es
Salaam mwezi wa nane mwaka huu”Alisema
Katika halfa
hiyo tukio hilo la makabidhiano ya msaada huo yalifanyika kwenye ukumbi wa
mikutano na mgeni rasmi alikuwa ni Afisa Matibabu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa
wa Tanga Bombo Dkt Clemence Marcel pamoja na Kaimu Mganga mkuu wa hospitali Dkt
Mohamed Abdallah.
“Katika kipindi
cha miaka 20 benki imetambua umuhimu wa jamii zinazozunguka eneo la biashara
yetu na ndio maana shughuli za kijamii ni muhimu sana kwa kwa benki ya
Exim…..Tunaamini
kwamba tuna nafasi kubwa katika kuchangia mabadiliko chanya katika sekta
mbalimbali kwa jamii zetu “Alisema
“Lakini pia
benki iliamua kusheherekea miaka hiyo kwa kusaidia jamii kwa njia ya kampeni
inayoitwa “Miaka 20 ya kujali Jamii” kuonyesha jinsi tunavyowashukuru kwani
benki hiyo imekwisha kutoa vitanda na magodoro ya hospitali kwa hospitali
nchini kote kila mwezi kwa mwaka mzima”Alisema
Kwa upande wake,
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Dkt Clemence Marcel aliipongeza Exim benki
kwa juhudi zake za kusaidia kukabiliana na upungufu wa vitanda kwenye hospitali
ambao umekuwa ukijitokeza mara kwa mara.
Alisema upungufu
wa vitanda katika hospitali umekuwa ni changamoto kubwa hivyo kukabidhiwa
vitanda 40 na magodoro utasaidia sana kupunguza vikwazo vya namna hiyo kwa
jamii.
Benki ya Exim
inatambuliwa kama Mwajiri bora wa kitanzania mwaka 2017 na taasisi ya The
Banker ya Afrika mashariki na sasa inasheherekea miaka 20 ya mafanikio,ukuaji
na kuwa kiongozi katika kuingia katika masoko mapya barani
Afrika.
“Exim Benki
iliyoanzishwa mwaka 1997 na imetanua soko lake kwa kufungua kampuni tanzu
katika nchi za Comorro(2007),Djibouti(2010) na Uganda (2016) lakini pia benki
hiyo inajuivunia kuwa benki ya kwanza kubwa ya kitanzania nay a kwanza kuingia
katika masoko ya nje ya nchi.(Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya
Tanga Raha)
Comments
Post a Comment