Featured Post

MWENYEKITI WA MTAA WA BUNGONI ATOA BATI 150 KUSAIDIA UJENZI WA ZAHANATI ILALA

Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam ambaye ni Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Bungoni Ilala, Barua Mwakilanga akikabidhi bati 150 kwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema, leo jijini Dar es Salaam. Ametoa bati hizo kuitikia mwito ulitoalewa hizi karibuni na Waziri Mkuu majaliwa Kassim Majaliwa kumwagiza Mkuu wa Wilaya ya Ilala kuchangisha fedha kwa wadau ili kupatikana fedha kwa ajili ya ujenzi wa zahanati Ilala.

"Asante sana" Sophia Mjema akimshukuru Barua wakati akipokea bati hizo
Sophia Mjema akizungumza baada ya kupokea bati hizo
"Bati hizi pelekeni kuzihifahdhi kuleee", Sophia Mjema akiwaelekeza vijana baada ya kupokea bati hizo
Mkuu wa Wilaya ya Ilala mkoani Dar es Salaam, Sophia Mjema akizungumza na Waandishi baada ya kupokea mabati hayo. Katikati ni Ndugu Barua. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

Comments