Featured Post

MAKAMU WA RAIS AHUDHURIA MAHAFALI YA 34 YA CHUO KIKUU HURIA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki matembezi ya mahafali ya 34 ya Chuko Kikuu Huria pamoja na Mkuu wa chuo hicho Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda (kulia) kuelekea kwenye uwanja wa Halmashauri ya  Bariadi kwenye sherehe za mahafali ya 34 ya Chuo Kikuu Huria Tanzania. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Huria Tanzania Profesa Rwekaza Mukandala wakati wa mahafali ya 34 ya chuo hicho yaliyofanyika kwenye uwanja wa Halmashauri ya Bariadi mkoani Simiyu. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Sehemu ya Wanafunzi waliohitimu katika Chuo Kikuu Huria wakiwa kwenye sherehe za mahafali ya 34 ya chuo hicho. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewakumbusha wahitimu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kuwa Vyeti walivyotunukiwa  ni tuzo halali kwa juhudi na jitihada walizoonesha darasani.
Makamu wa Rais aliyasema hayo wakati wa sherehe za mahafali ya 34 ya Chuo Kikuu Huria yaliyofanyika kwenye uwanja wa Halmashauri Bariadi mkoani Simiyu.
Makamu wa Rais alisema “ Jamii inategemea mtaipatia tuzo ya utendaji bora na ufanisi katika fani zenu utakao akisi viwango vilivyoainishwa kwenye vyeti vyenu”.
Makamu wa Rais aliupongeza uongozi wa chuo kwa jitihada zake katika kutekeleza maelekezo ya Mhe. Rais hasa katika sula la Uchumi wa Viwanda ambapo chuo hicho kimefanya Kongamano kubwa la Elimu ya Juu na Uchumi wa Viwanda mjini Bariadi lakini pia chuo hicho kipo kwenye mchakato wa Kigoda cha kiprofesa cha Viwanda na Maendeleo.
Makamu wa Rais aliwakumbusha uongozi wa chuo katika jitihada zake za kutekeleza majukumu ya chuo , uendelee kujikita kwenye kauli mbiu yake Elimu Bora na Nafuu kwa Wote .
Katika Mahafali hayo ambayo zaidi ya wanafunzi 941 wamehitimu kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar pamoja na nchi za jirani ambapo wanafunzi saba (7) walihitimu Shahada ya Uzamivu ya Udaktari wa Falsafa ya Chuo Kikuu Huria.

Comments