Featured Post

MAFUNZO YA MADAKTARI WA KANDA YA KASKAZINI YALIYORATIBIWA NA WCF YAMALIZIKA

  NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, MOSHI

MADAKTARI na watoa huduma kutoka Kanda ya Kaskazini, waliokuwa wakishiriki mafunzo ya siku tano (5), ya kufanya tathmini ya mfanyaakzi aliyepata ulemavu uliotokana na ajali na magonjwa yatokanayo na kazi amesema wamepata nyezo muhimu itakayowasaidia kutekeleza majukumu hayo kwa usahihi na haraka.

Akizungumza kwa niaba ya washiriki wenzake wakati wa kufunga mafunzo hayo yaliyokuwa yakifanyika mjini Moshi, Februari 23, 2018, Dkt. Peter Mabula kutoka Arusha Lutheran Medical Centre alisema, wengi wao walikuwa hawafahamu nini cha kufanya wanapomuhudumia mfanyakazi aliyepata madhara yatokanayo na kazi, ili kumfanyia tathmini kwa ajili ya kulipwa Fidia stahiki bali walitumia uwezo wao wa kawaida wa kidaktari.

“Mafunzo yametuwezesha ni jinsi gani daktari utafanya tathmini na ukadiriaji wa matatizo mbalimbali yatokanayo na kazi mbalimbali aliyopata mfanyakazi, kuelewa mgonjwa wa aina fulani anapofika kupatiwa huduma utamuhudumia kwa kutumia vigezo vilivyopo kisheria, lakini pia usahihi wa kujaza takwimu zake katika kumbukumbu za kitabibu.” Alisema.


Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Moshi, Katibu Tawala  Msaidizi wa Manispaa hiyo, Bw. Sebastian Masanja

Aliupongeza Mfuko kwa kuandaa mafunzo hayo kani yatawezesha kuwepo na madaktari ambao wamepatiwa mafunzo maalum ya kufanya tathmini ili kutoa fidia inayostahili.

“Tulikotoka jamani hatukuwa na utaratibu maalum unaoeleweka kwamba ukiumia kazini unaenda kumuona nani na huyo mtu unaeenda kumuona hujui ni lini atakufidia kulingana na ulemavu ulioupata.” Alisema Bw. Masanja.

Lakini pia, aliwaasa madaktari na watoa huduma hao, kutumia elimu waliyopata ili kutoa tathmini sahihi na hatimaye mgonjwa aliyeumia aweze kupata haki stahiki na kwa haraka.

Naye Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, wa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), ambao ndio waandaaji wa mafunzo hayo, Dkt. Abdulsalaam Omar alisema, jumla ya washiriki 66 kutoka mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Manyara na Tanga walishiriki mafunzo hayo, chini ya wataalamu wa WCF na wawezeshaji waliobobea kwenye maswala ya usalama mahala pa kazi kutoka taasisi ya Mifupa MOI.

Alisema mafunzo haya ni mundelezo wa mafunzo kama haya ambayo yamekuwa yakifanyika kwa awamu kwenye kanda mbalimbali nchini, ili kujenga mtandao wa wataalamu wa kufanya tathmini ya ulemavu uliotokana na ajali au magonjwa yatokanayo na kazi kwa mujibu wa mkataba.

“ Idadi ya madaktari ambao wamepatiwa mafunzo haya nchi nzima hadi sasa ni 655 na tunatarajia kutoa mafunzo zaidi ili wafanyakazi waweze kupata huduma kwa ukaribu lakini kwa haraka na usahihi.” Alifafanua Dkt. Abdulsalaam.

Baadhi ya Madaktari na watoa huduma za afya wakionyesha stika, watakazobandika kwenye milango ya ofisi zao ili kumrahisishia mfanyakazi anayehitaji kufanyiwa huduma ya tathmini. Stika hizo zimetolewa na WCF kwa washiriki wa mafunzo ya siku tano ya kufanya tathmini ya mfanyaakzi aliyepata ulemavu uliotokana na ajali na magonjwa yatokanayo na kazi yaliyomalizika Februari 23, 2018 mjini Moshi.
Katibu Tawala  Msaidizi wa Manispaa hiyo, Bw. Sebastian Masanja, kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Moshi, akitoa hotuba ya kufunga mafunzo hayo

 Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, wa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), ambao ndio waandaaji wa mafunzo hayo, Dkt. Abdulsalaam Omar, akizungumza.
Bi. Naanjela S.Msangi, Meneja tathmini ya hatari mahala pa kazi wa WCF, (mbele), akiwa na washiriki
 
Dkt. Peter Mabula kutoka Arusha Lutheran Medical Centre, akizungumza kwa niaba ya washiriki wenzake
 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano, WCF, Bi. Laura Kunenge, akionyesha stika hizo za utambuzi wa ofisi ya mtoa huduma ya tathmini.
 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano, WCF, Bi. Laura Kunenge, akimkabidhi stika ya utambuzi wa ofisi ya mtoa huduma ya tathmini, DktJosephine Rogate, kutoka Hospitali ya Mawenzi.
 Mmoja wa washiriki Dkt. Theresia Temu
 Mgeni rasmi, Katibu Tawala  Msaidizi wa Mkoa wa Kilimanjaro, kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Bw. Sebastian Masanja, akimkabidhi cheti Dkt. Theresia Temu, cha ushiriki wa mafunzo ya siku tano ya kufanya tathmini ya mfanyaakzi aliyepata ulemavu uliotokana na ajali na magonjwa yatokanayo na kazi,  yaliyowaleta pamoja madaktari 66 kutoka mikoa ya Kaskazini, 


 Baadhi ya washiriki

Meneja tathmini ya madai, (Claims Assessment Manager), wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Dkt. Ali Mtulia, akitoa mada ya namna ya kufanya tathmini na ukadiriaji(Assessment and evaluation)


Meneja tathmini ya madai, (Claims Assessment Manager), wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Dkt. Ali Mtulia, akitoa mada ya namna ya kufanya tathmini na ukadiriaji(Assessment and evaluation)
 

Meneja tathmini ya madai, (Claims Assessment Manager), wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Dkt. Ali Mtulia, akitoa mada ya namna ya kufanya tathmini na ukadiriaji(Assessment and evaluation)

 Daktari bingwa wa uchunghuzi wa vijidudu na madawa,(Medical Microbiology and Immunology), Profesa John Shao, (kulia), akiteta jambo na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, wa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), Dkt. Abdulsalaam Omar.
  Daktari bingwa wa uchunghuzi wa vijidudu na madawa,(Medical Microbiology and Immunology), Profesa John Shao, (kulia), akipongezwa na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, wa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), Dkt. Abdulsalaam Omar, kwa kuwapa uzoefu wake wa kazi katika sekta ya afya na tiba washiriki hao.
 Profesa Shao, (kulia), akiagana na Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Kilimanjaro Bw. Sebastian Masanja baada ya kufungwa kwa mafunzo hayo.
 Profesa Shao, (kushoto), akibadilishana mawazo na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano, WCF, Bi.Laura Kunenge, katikati), na Bi. Naanjela S.Msangi, Meneja tathmini ya hatari mahala pa kazi 
 Wawezeshaji (watoa mada), kutoka kushoto, Dkt. Hussein, Dkt. Mshashu na Dkt. Mhina.
Afusa mwandamizi kutoka WCF, Dkt. Pascal Magesa,  akigawa fomu za tathmini ya mafunzo
 Picha ya kwanza ya pamoja 
Picha ya pili ya pamoja


Comments