- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Na Blandina
Manyanda (Wakili)
Watoto
wanahaki nyingi katika jamii wakili, Blandina Manyanda anatueleza baadhi ya haki za kisheria
za watoto.
Kabla hatujaendea mbele, msomaji nakuomba
uzingatie mambo mawili muhimu ambayo ni falsafa itakayokuongoza maishani:
(i)
Hakuna mtu yeyote awe tajiri ama masikini, wa
kike ama wa kiume, mwenye ajira asiye na ajira na mwenye akili timamu ama
punguani, ambaye wakati fulani hakuwahi kuwa mtoto kwa hiyo utoto ni sehemu ya
maisha ya mwanadamu awaye yoyote yule, na yale yanayofanywa na watoto leo
yakatuchukiza ama yakatufurahisha ni muendelezo tu wa yale tuliyoyafanya sisi
tukayaacha mahali fulani. Hakuna kinachofanywa na watoto ambacho hakina
chimbuko katika jamii na hasa katika familia zetu.
(ii)
Hakuna mtoto hata mmoja ambaye anakuja
ulimwenguni humu kwa ridhaa yake mwenyewe, kwa kila mtoto anayezaliwa ulimwenguni,
wenye maamuzi mazito ya kwamba azaliwe ama la ni wazazi wake wawili.
Msisitizo wangu hapa ni kwamba wote
tunapozaliwa, hatuwaombi wazazi kwamba tunaomba tuzaliwe.
Ni mipango tu ya wazazi, ama hata wakati
mwingine ni utaratibu wa kukidhi tamaa za miili yao ambao mwishowe unamleta
kila mmoja wetu duniani kama mtoto.
Kwa msingi huo hao waliomleta mtoto
ulimwenguni iwe ni kwa mipango yao ama kutokana na kukidhi tamaa zao za mwili,
basi wana wajibu mkubwa sana wa kuhakisha watoto wanapata haki yao ya msingi ya
malezi na matunzo mema.
Mtoto
ni nani
Kuna sheria nyingi ambazo kwa kiasi fulani
zinajaribu kuelezea mtoto ni nani.
Sheria hizi ni kama Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971, Sheria ya Mikataba, Sheria ya
Ushahidi, Kanuni ya Adhabu n.k.
Sheria hizi kila moja inajaribu kuainisha
mtoto ni nani na akitambuliwa hivyo asifanye nini, lakini mimi kwa ajili ya makala
haya, nitamchukulia mtoto kama anavyofafanuliwa na sheria ya mtoto hapa nchini
yaani ‘’The Law of the Child No. 21 of
2009. sheria hii katika kifungu cha 4(i) inatamka bayana kwamba, mtoto ni
mtu yeyote ambaye yu na miaka 18 kwenda chini, inasema “A person below the age of 18 years shall be known as a child’’.
Ikumbukwe hapa hii sheria haikuainisha
huyo mtu awe yuko wapi na anafanya nini kwa hiyo mtu yeyote ambaye ni mwanafunzi,
ama mfungwa, ama ni mgonjwa kitandani, ama ni mtaalamu wa jambo flani ama hata
ni mke wa mtu, kama hajafikisha umri wa miaka 18 basi huyo ni mtoto.
Sheria ya Umri wa Utu Uzima (yaani the Age of Majority Act) inatamka bayana
kwamba mtu akifikisha miaka 18 basi atahesabika kwamba ameingia utu uzima,
vilevile sheria inatamka bayana kwamba utu uzima unaanza siku ambayo mtu
anaadhimisha siku ya 18 ya kuzaliwa kwake, yaani siku hiyo ndiyo anaachana na
utoto.
Siku ya pili yake yaani akiwa na umri wa
miaka 18 na siku moja, huyo ni mtu mzima.
Hata hivyo, sheria hii imeaacha baadhi ya
mashimo pasipo kuyafukia, kwa mfano haikuelezea kalenda itakayotumika katika
kuhesabu miaka ni kalenda ipi, ama hata iwapo siku mtu anapotimiza miaka 18 je
kama mtu kama huyo alizaliwa saa 4 asubuhi je inapofika saa 5 asubuhi anakuwa
mtu mzima tayari ama bado?
Katika Tanzania kwa mujibu wa utafiti
uliyofanywa mtoto ni nguzo muhimu ya taifa kwa sababu zaidi ya asilimia 46 ya
wananchi wote wa Tanzania ni watoto. Mtu mwingine anaweza kusema sasa mbona
asilimia inayosalia ndio nyingi yaani
karibu 54%.
Ni sawa vilevile kuna asilimia (tena
kubwa tu) ya watu ambao akili yao imeisharudia kuwa ya kitoto.
Hawa ndio wenye umri mkubwa sana na labda
hawana tena uwezo wa kujitegemea kiakili. Mnamo mwaka 1996 wastani wa watoto
katika familia walikuwa ni watoto 6. (Takwimu hii ni ya 1996 kwa hiyo sasa hivi
kunaweza kukawepo mabadiliko kidogo hasa ukizingatia kwamba kwa sasa wanajamii
wanakazania kupunguza uzao)
Taifa kama taifa limefanya mambo kadhaa
kwa ajili ya kuhakikisha kwamba watoto hawa wanapata matunzo na malezi bora,
sera na mipango ya taifa iliyochukuliwa kwa ajili ya malezi na makuzi ya mtoto
ni pamoja na ‘huduma za mama na mtoto, huduma za chanjo mbalimbali miladi
kadhaa ya maji safi vijijini, kampuni za usafi wa mazingira, uanzishwaji wa
vituo vya kulelea watoto wachanga (Yaani feeding and day care centre)
uanzishwaji wa shule za awali yaani pre-shools, uanzishwaji wa viwanja vya
michezo kwa ajili ya watoto na uanzishwaji wa sera ua elimu ya msingi kwa wote.
Ni bahati mbaya kwamba mipango na
mikakati hii haitekelezeki kama inavyopasika si kwa sababu taifa halina uwezo
bali kwa sababu ya uzembe na kutokuwajibika kwa wanapokadhiwa madaraka.
Tuchukulie kwa mfano suala la viwanja vya
michezo kwa watoto kila mtaa unapaswa kuwa na kiwanja cha michezo kwa watoto wa
mtaa huo.
Kila kijiji na kitongoji kinapaswa kuwa
na viwanja vya michezo kwa ajili ya watoto wa maeneo hayo.
Lakini kusema ukweli viwanja hivyo havipo
na hata viongozi hawajui kwa nini havipo.
Jibu la haraka utakalopewa iwapo utauliza
juu ya uwepo wa viwanja, ni mara hakuna fedha, mara mtiskisiko wa uchumi
duniani n.k.
Lakini ukweli mbona hii mitikisiko
haitikisi misafara mikubwa ya magari wanayoambatana nayo viongozi wetu
wanapokuwa katika ziara za mikoa? Kutokuwa na fedha pamoja na mtikisiko wa
uchumi duniani, kwangu mimi naona ni kama visingizio ama, ‘scapegoat’’ upande
wa viongozi.
Haki
za watoto kwa mjibu wa sheria za Tanzania ni zipi?
Sheria ya mpya ya mtoto iliyoanzishwa
hivi karibuni yaani The Law of the Child
No. 21 of 2009, ambayo imefuta sheria zote zilizokuwa na upungufu kuhusu haki
za watoto inaainisha haki mbalimbali ambazo watoto wamepewa kwa mjibu wa
sheria.
Kwa mjibu wa sheria ya mtoto ya mwaka
2009 haki za mtoto zimeainishwa sehemu ya pili(II) ya sheria hiyo na haki hizo ni pamoja na:
(a) Haki ya kuishi kwa uhuru bila kubaguliwa.Haki hii
imeanishwa katika kifungu namba 5(1) na(2) cha seria ya mtoto ambacho
kiafafanua zaidi kuwa mtoto ana haki ya kuishi bila kubaguliwa kwa sababu ya
jinsia, tabaka/rangi, umri, dini,lugha, ulemavu,hali ya kiuchumi, mahali
anapoishi(mjini au kijijini),kuzaliwa hali ya ukimbizi nk.
(b) Haki ya kuwa na jina, utaifa na kuwajua wazazi
wake na ndugu wengine. Haki hii imeanishwa katika kifungu namba 6 cha
sheria ya mtoto na kinasema kuwa mtoto yoyote
ana haki ya kuwa na jina, utaifa na kuwajua wazazi wake na ndugu
zake,pia kinazidi kuelezea kuwa niwajibu wa mzazi au mlezi kuhakikisha anasajili
kuzaliwa kwa mtoto huyo.
(c) Haki ya kuishi na wazazi au walezi wake na .Hii imeainishwa
katika kifungu namba 7 cha sheria ya mtoto.Kifunu kinaelezea zaidi kuwa mtu yoyote
hapaswi kumnyima mtoto haki ya kukua na kulelewa na wazazi wake katika mazingira salama ispokuwa kama
imeamuliwa na mahakama.
(d)
Haki ya kupata
matunzo na mahitaji ya lazima kutoka kwa wazazi, walezi au mtu yoyote mwenye
mamlaka juu ya mtoto huyo. Kifungu cha 8 cha sheria ya mtoto kinatamka
bayana kwamba ni jukumu la mzazi, mlezi ama mtu mwingine yeyote mwenye mamlaka
juu ya mtoto huyo, kumpa matunzo yanayostahiki hasa: chakula, malazi, mavazi, huduma ya afya na kinga, elimu na malezi, Uhuru
(yaani liberty) na haki ya kucheza na kustarehe.
(e) Haki ya kuishi, utu, kuheshimiwa. Hizi
zimeanishwa kaitka kifungu namaba 9 cha sheria ya mtoto na kinampa wajibu mzazi
au mlezi wa kumlinda mtoto dhidi ya unyanyasaji,udhalilishaji kwa namna yoyote
ile.
(f) Haki ya kutumia na kufurahia mali za wazazi
wake,
hii imeainishwa katika kifungu namba
10 cha sheria ya mtoto.
(g) Haki ya kutoa mawazo na maoni yake, kusikilizwa na
kushiriki katika maamuzi mbalimbali.
(h) Haki ya kupewa adhabu inayositahili pale
anapokosea. Adhabu
hiyo isiwe yenye kuhatarisha afya, kumnyanyasa kisaikolojia,kumdhalilisha utu
mtoto na kumnyanyasa.
Pamoja na haki zote alizopewa mtoto kwa
mjibu wa sheria, mtoto pia ana wajibu wa kuheshimu wazazi wake na wakubwa zake,
kusaidia kazi za nyumbani zisizo na madhara kwake, kutumikia jamii na taifa
kulingana na uwezo wake na umri wake, kulinda na kuhifadhi mila chanya na
utamduni nk.
Comments
Post a Comment