Featured Post

DIAMOND PLATNUMZ AITWA NA NYOTA YAJAHA GOMS


Na Richard Mwaikenda, Goms
MSANII chipukizi wa muziki wa kizazi kipya Bakari Omari Bwere 'Nyota Yajaha' amesema anatamani akutane na msanii nguli Abdul Naseeb 'Diamond Platnumz' ampige tafu ili asonge mbele kimuziki kama alivyo yeye.

Nyota ya Yajaa ambaye yuko mbioni kuibua kibao chake kipya cha Nisharizia , amesema anafanya mipango ya kumuona Diamond ili amsaidie kumvusha katika hatua aliyopo kwenda kwenye mafanikio.

Msanii huyo ambaye makazi yake yako Gongo la Mboto (Goms) ana ndoto ya siku za mbeleni kuwa mmoja wasanii maarufu Tanzania na nje ya nchi, kama alivyo Diamond.


Hivi sasa yupo mbioni kuachia video ya wimbo wa Nimerizia aliofanya pamoja na PNC wenye vionjo vya mapenzi baada ya kuachia audio siku ya Valentine Day.


Nyota Yajaa ambaye yupo chini ya usimamizi wa NYOTA ENTERTAINMENT, ambayo ipo chini ya umiliki wa nyota yajaa mwenyewe,


Ameahidi makubwa kupitia video hiyo inayokuja akiamini italeta ushindani mkubwa kwenye soko la muziki nchini Tanzania, Pia amezungumzia ujio wa wimbo wake mpya utakayofuata baada ya Nisharizia.


Nyota yupo mbioni kufanya Kolabo wasanii wakubwa wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini Tanzania, Nyota alidai nimapema sana kuzungumzia kolabo hiyo na Mkali huyo wa miondoko ya Bongo fleva nchini Tanzania. 


kikubwa alisema mashabiki wakae mkao wa kula kwani hata waangusha.


Mbali na muziki NYOTA ENTERTAINMENT pia inasimamia kazi za maigizo za nyota yajaa na wasanii wengine chipukizi waliopo ndani  ya Lebo hiyo.


Nyota yajaa amefanikiwa kuachia filamu kama NIPE RISITI,MAPENZI MAJINI,KUTEKWA KWA ROMA,KABAKA KUKU, JINSIA GANI, N.K.


Akishirikiana na wasanii wakongwe kama Mzee Majanga, Ringo, Dula Matenda,N.k.


Kutazama Kazi za NYOTA ENTERTAINMENT BONYEZA HAPA https://www.youtube.com/channel/UCWFfp-FHOkG5rUaFWSotRbg


Comments