Featured Post

CCM MANISPAA YA IRINGA YATEKELEZA AHADI YA MBUNGE MSIGWA KATIKA SOKO KUU LA MANISPAA YA IRINGA

Mwenyekiti wa chama cha mapindizi (CCM) manispaa ya Iringa Said Rubeya akimkabidhi TV na king'amuzi mwenyekiti wa masoko ya manispaa ya iringa Starmi Mathew akiwa sambamba na viongozi na wanachama wa chama hicho.
Mwenyekiti wa chama cha mapindizi (CCM) manispaa ya Iringa Said Rubeya akimkabidhi king'amuzi mwenyekiti wa masoko ya manispaa ya iringa Starmi Mathew akiwa sambamba na viongozi na wanachama wa chama hicho
Mbunge wa viti maalumu ritta Kabati akiwa na diwani wa kata ya Mshindo Ngwada pamoja na matha walipokuwa wakikabidhi TV na king'amuzi cha Azam kwa viongozi wa soko kuu la manispaa ya Iringa
Wananchama wa chama cha mapinduzi pamoja na baadhi ya wafanyabiashara walipohudhuria hafla ya kukabidhiwa kwa TV na king'amuzi cha Azam TV kwa viongozi wa soko kuu manispaa ya Iringa.

Na Fredy Mgunda, Iringa
CHAMA cha mapindizi (CCM) manispaa ya Iringa kimetekeleza ahadi ilikuwa imeahidiwa na chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) wakati wa kampeni za mwaka 2015 ya kuwatafutia TV wafanyabiashara wa soko kuu la manispaa ya Iringa chini ya mgombea wake wa ubunge mchungaji Petter Msigwa ambaye kwa sasa ndio mbunge wa jimbo la Iringa mjini 
 
Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa CCM manispaa ya Iringa Said Rubeya alipokuwa anakabidhi TV nchi 58 na king’amuzi kwa kiongozi wa masoko hapa manispaa.

Rubeya alisema kuwa wametoa TV hiyo kwa lengo la kuhakikisha kuwa wananchi na wafanyabiashara wa soko hilo wanapata habari kwa wakati.

“Mimi nimekuja jana hapa mkaniambia kero hii nikaichuklua na chama change kimeifanyia kazi haraka iwezekanavyo na saizi tumekuja kukabidhi” alisema Rubeya

Rubeya alisema kuwa chama cha mapinduzi kinaamini kwenye utendaji na sio kulalamika na kuandamana hivyo kuna tumia vizuri falsafa ya Rais Dr John Pombe Magufuli ya hapa kazi tu ndio maana tupo hapa kufanya kazi kwa vitendo kwa wananchi.

“Chama cha mapinduzi manispaa ya Iringa kinafanya kazi kwa vitendo pale tunaposikia kero za wananchi tunatafuta njia za kutatua changamoto hizo ndio maana leo tunaleta hii TV na king’amuzi ili wafanyabiasha mpate habari mkiwa hapa kazini” alisema Rubeya

Rubeya alisema kuwa alipokea malalamiko kutoka kwa wafanyabiasha ya kutekelezwa kwa ahadi ambazo zilizotelewa na mbunge wakati kampeni na imepita miaka mingi haijatekelezwa hivyo wakaamua kuichua na kuitatua ili kuwapa haki wananchi na wafanyabishara wa soko hilo.

“CCM tukitoa ahadi tunatekeleza kwa wakati lakini wenzetu wamekuwa wanapiga propaganda tu za maneno hivyo wananchi mnatakiwa kuchagua viongozi ambao wanaweza kutekeleza ahadi zao kwa maendeleo ya wananchi wanaowangoza” alisema Rubeya

Kwa upande wake mbunge wa viti maalumu ritta Kabati alisema kuwa kitendo cha leo walichokifanya chama cha mapinduzi manispaa ya Iringa kinaonesha kuwa chama hicho ni chama cha wananchi wote ndio maana leo wametoa TV na king’amuzi kwa ajili ya kupata habari kwa wananchi wanaopata huduma katika soko hilo.

“Kupata habari ni haki ya kila mwananchi wa mtanzania anapata habari kwa wakati hivyo kutoa TV hii kutasaidia kuongeza wigo kwa wananchi kupata habari kwa wakati” alisema Kabati

Kabati aliwataka viongozi wa soko hili kuandaa mkutano wa kusikiza kero ili kuzitafutia ufumbuzi kwa lengo la kuendelea kukuza uchumi na kuleta maendeleo kwa haraka zaidi na kuendana na kasi ya Rais wa awamu ya tano Dr Johh Pombe Magufuli.

“Mwenyekiti naomba mniandalie mkutano nije kuwasikiliza kero zenu kwa kuwa ni haki yenu na msipofanya hivyo mtakuwa mnajinyima haki yenu ya msingi ya kutatuliwa kero zenu” alisema Kabati

Naye mwenyekiti wa masoko ya manispaa ya iringa Starmi Mathew aliwashukuru chama cha mapinduzi kwa msaada walioutoa kwa kuwa wamerahisisha wafanyabiashara kupata habari wakiwa kazini.

Mathew alikiomba chama hicho kuongezea nguvu kwenye masoko mwengine ya manipsaa ya Iringa kupata hata TV ndogo hata kama sio kuwa kama ambayo imetolewa leo katika soko kuu la manispaa ya Iringa

“Naomba nimbe kama hapo mbe mtapa nguvu nyingine basi tunaomba mtukumbuke tena maana kuna soko hilo hapo chini nalo linahitaji kuwa na Tv nao wewe kupata habari kama haki yao ya msingi kujia nini kinaendelea duniani” alisema Mathew

Aidha Mathew akawamba viongozi wa chama cha mapinduzi kuwasidia kuiomba SUMATRA kutengeneza njia ya daladala ipite katika soko hilo ili kuongeza mzunguko wa kibiashara kama ilivyo mikoa mingi hapa nchini.

Comments